Skip to main content

WIZARA YATILIANA SAINI NA 'GWP' KUONDOA SHIDA YA MAJI ZANZIBAR

 

NA SALMA LUSANGI, WMNM-ZANZIBAR:::

WIZARA ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, imetiliana saini ya makubaliano (MoU)  na taasisi ya 'Global Water Partnership (GWP)'  kuhusu utekelezaji wa mpango mkuu wa maji safi na salama Zanzibar.

Hafla hiyo ya kutiliana saini imefanyika mjini, Zanzibar baina ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Joseph Kilangi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya GWP Dk. Victor Kongo na  kushuhudiwa na viongozi wakuu na watendaji wa taasisi mbili hizo.   


Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Katibu Mkuu huyo alisema kupitia makubaliano hayo Mpango Mkuu wa Maji Zanzibar wa mwaka 2022/2027 utaweza kutekelezeka kwa haraka na kuleta ufanisi ambao Wizara yake inahitaji katika utekelezaji wa huduma ya maji  Zanzibar.


Alisema  changamoto zilizopo katika masuala ya maji yanahitaji utafiti wa kina ikiwemo miundombinu ya maji, maeneo sahihi ya kuchimba visima na mambo mengine ya kitalaamu ili Wizara yake iweze  kutatua tatizo la maji  kwa wananchi.


“Taasisi ya Global Water Partnership itaweza kusaidia kufanya tafiti zinazohitajika ili tatizo la maji lipatiwe ufumbuzi kwani maeneo mengi yamekuwa yakikosekana maji kupitia mkutano huu tafiti za kitalamu zitafanywa “ Alisema Kilangi.




Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GWP Dr. Victor Kongo alisema makubaliyano hayo yataleta ufanisi katika kutekeleza Mpango Mkuu wa maji Zanzibar ambapo Taasisi yake imepanga kufanya tafiti mbali mbali pamoja na kutafuta miradi ya maji kwa Zanzibar.


Alisema kupitia Mkataba huo wa  makubaliano waliyosaini Agosti 17, 2022 Taasisi yake itaongeza juhudi za makusudi ili tatizo la maji Zanzibar lipatiwe ufumbuzi na maji yapatikane katika maeneo yote ya mjini na vijijini.




Kwa upande wake Waziri wa Maji, Nishati Na Madini Shaibu Kaduara alisema wananchi wengi Zanzibar wamekua wakilalamikia masuala ya maji, lakini kupitia tafiti zitakazofanywa baina ya Wizara yake kwa kushirikiana na GWP anaamini Wizara yake itafanikisha kuwaondolea shida ya maji katika mji wa Zanzibar.




Kwa upande wake mwenyekiti wa GWP mhandisi Ngwisa Mpembe ameahidi kuleta watalaamu wa utafiti katika masuala ya maji Zanzibar hivyo ameiomba Wizara ya Maji, Nishati na Madini kuingiza masuala ya utafiti katika Mpango Mkuu wa Serikali.


Mwisho alimshukuru  Waziri wa Maji , Nishati na Madini Shaib Kaduara, Katibu Mkuu Joseph Kilangi bila ya kumsahau Katibu Mkuu aliyeondoka Dkt Mngereza Miraji kwa kuwapokea na kuanzisha mashirikiano ya pamoja kwa ajili ya kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi huduma ya Maji Zanzibar.

Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch