NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANAUME wa shehia za Kibokoni na Vitongoji
wialaya ya Chake chake, wamesema wakati umefika sasa, wa kuanzishwa kwa dawati
la siri la kundi lao, ili kutoa malalamiko, wanapopewa kichapo na wanawake.
Ushauri huo wameutoa Septemba 5, 2024 kwenye kongamano la kujadili njia za
kutokomeza ukatili na udhalilishahaji wa kijinsia, lililoandaliwa na Mwemvuli
wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ na kufanyika skuli ya sekondari ya Vitongoji
wilayani humo.
Walisema wapo baadhi yao, wanaopokea vipigo kutoka kwa wake
zao, ingawa wamekuwa hawajui wapi wakaripoti madhila hayo.
Walieleza kuwa, wapo wanawake wamekuwa wakatili kwa waume zao,
ingawa wanapokumbumbwa na changamoto hizo, hushindwa wapi wakaripoti.
Mmoja kati ya wanaume hao, Salim Ayoub, alisema wanaoa aibu
kwenda moja kwa moja kituo cha Polisi kuripoti matukio hayo, hivyo kama
wataanzishiwa dawati lao, watejenga uthubutu wa kuziripoti kesi hizo.
Alifahamisha kuwa, kama serikali inataka kujua njia sahihi ya
kupunguza matendo wanayofanyiwa, kwa sasa ni kwepo kwa dawati la wanaume, la kushughulikia
malalamiko yao.
"Wakati umefika sasa kuwapa haki ya faragha wanaume
wanaopigwa na wanawake, ili nao kuwa huru kuziripoti kesi za udhalilishaji
ikiwemo kipigo,’’alishauri.
Nae Haji Yussuf Khamis, alisema sio sahihi panapozungumziwa ukatili
na udhalilishaji, wanaume kuachwa nyuma, kama vile hawakumbani na changamoto
hizo.
‘’Hata sisi wanaume tunadhalilishwa na wanawake, sasa lazima
sheria ituangalie na ikiwezekana ituwekee mahakama ya siri, ili kufikisha
malalamiko yetu,’’alisema.
Kwa upande wake Jokha Abdalla Ali, alishauri kuwa, watoto
wanaofanyiana udhalilishaji, lazima kwe na adhabu mbadala, ili waingie woga.
Mwanasheria Aziza Suleiman Mohamed, alisema rushwa muhali ni
miongoni mwa sababu, inayochangia kuendelea kwa metendo hayo.
‘’Sheria ziko wazi, kuwa hawezi kutiwa hatiani mtu yeyote,
pasi na ushahidi usio kuwa na shaka, lakini kama hatutoshirikiana na vyombo vya
sheria, tusitegemee mabadiliko,’’alifafanua.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mratibu wa miradi kutoka ‘PACSO’
Mohamed Najim Omar, alisema lengo la kongamano hilo, ni kuwapa nafasi wanajamii
kutoa mawazo yao, nini kifanyike ili kutokomeza udhalilishaji.
Alisema, PACSO imeona kutumia njia hiyo, kwa vile wakosaji wa
makosa hayo, wanatoka ndani ya jamii yenyewe.
‘’Makongamano haya ya wazi, yatakuwa endelevu kila tunapopata
nafasi, na lengo lake hasa ni jamii kutoa fikiria zao ni namna gani, matendo
haya yatakoma ndani ya vijiji vyetu,’’alifafanua.
Akifunga kongamano hilo, sheha wa Kobokoni Khalef Othman Khamis,
alisema hata tafsiri ya umri wa mtoto, kwa sasa ni shangamoto.
‘’Kisheria hadi miaka17 bado ni mtoto na anakinga, lakini
makosa anayoyafanya ni makubwa, ni zaidi ya mtu mzima, na huu umri napendekeza
upunguzwe,’’alifafanua.
Katibu Mkuu wa ‘PACSO’ Sifuni Ali Haji, alisema kinachofuata
kwa sasa ni kuanzisha kamati za maadili zenye mfumo wa polisi jamii, ili kuwakinga
watoto na udhalilishaji.
‘’PACSO kama muungano wa asasi za kiraia, imefanya wajibu
wake, kilichobakia sasa ni jamii kukaa chini na kuwa na sheria ndogo ndogo, ili
kuwalea watoto wetu,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, amwataka watoto kutoa taarifa za haraka
kwa wazazi, waalimu, masheha na watu wingine watapoona dalili za kufanyiwa
ukatili.
MWISHO
Comments
Post a Comment