NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa Wete, Zuwena Mohamed Abdul-kadir, amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne, mshitakiwa Ali Mbarouk Suleiman mwenye (18) mkaazi wa Konde Chanjaani, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuvunja nymba usiku na kuiba.
Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung, yenye thamani ya shilingi 138,000 kwa kukisia mali ya Said Mohamed Salim.
Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja nyumba usiku atatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba simu atumikia kwa muda wa mwaka mmoja.
Mbali na adhabu hiyo, pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mmiliki ambapo, hapo awali wakati wa kuiendesha kaesi hiyo, ilikua ni kielelezo cha ushahidi mahkamani hapo.
Mwendesha Mashtaka wa serikali Mohamed Ali Juma, alieleza kuwa kwa vile Mahkama imemuona na hatia mshitakiwa huyo, ni vyema kutoa adhabu kali kwake.
Aliendelea kusema kuwa, masuala ya wizi hususani usiku ni masuala ambayo imekua ikisumbua jamii, hivyo isimuonee huruma impe adhabu kama sheria inavyoelekeza.
‘’Mheshimiwa, tunakuomba kwamba umpe adhabu kali kama sharia ilivyo elekeza, kwani wizi ni masuala ambayo imekuwa ni kero kwa jamii, na hata taifa kwa ujumla,’’alisema.
Baada ya maelezo hayo ya Mwendesha mashataka, ndipo Hakimu huyo alipomwamuru mshitakiwa, kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka minne.
Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 20 mwaka huu, majira ya saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku kijiji cha Chanjaani Konde, wilaya ya Micheweni Pemba.
Ilitambuliwa kuwa, mshitakiwa huyo, alivunja nyumba ikiwa ni kosa kinyume na kifungu cha 290 (1) na 291(1), ( a), ( 2) cha Sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Kosa la pili ni kuiba simu moja aina ya SUMSUNG yenye thamani ya shilingi 138,000 kwa makisio, ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 251( 1) na 258 vya sharia nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
MWISHO
Comments
Post a Comment