NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
MWENYEKITI wa Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar, 'ZAFELA' Hamisa Mmanga Makame, ameiomba jamii kuchukuwa hatua dhidi ya kupiga udhalilishaji wa kijinsia nchini kwa wanawake na watoto.
Ameleza hayo leo Novemba 26, 2024 katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupiga udhalilishaji wa kijinsia yaliyofanyika katika uwanja wa Majenzi wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
"Kujitokeza kwa wingi ili kupinga udhalilishaji na kupata elimu ya udhalilishaji kutoka ZAFELA na kuwahamasisha na wingine ili matendo ya udhalishaji yaweze kuondoka.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi tu inapotokea vitendo hivyo, ili sheria kuchukuwa hatua kali kwa mtuhumiwa wa makosa hayo.
Aidha alizishukuru tasisi na jumuiya za asasi binafsi na za kiserekali ambazo zina lengo la kupinga na kupeleka ujumbe katika jamii, ili kupambana na vitendo vya udhalilishaji visiwani hapa.
"Huwezi kuelewa athari na njia za kuondokona na ukatili katika jamii zetu, mpaka pale utapo pata tatizo hivyo wazee kuhakikisha mnalea watoto wenu, kuwatunza ili kuondokana na vitendo vya udhalilisha dhidi ya wananaweke na watoto kwa kuwalea katika Malezi bora,'' ufuatiliaji wa hali ya juu.
Mapema Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Khatibu Juma Mjaja, alieleza kuwa Serikali imewekeza nguvu ya kutosha katika Kuendelea kupambana dhidi za vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, kwan yanaharibu taswira, kuharibu mfumo wa kisaikolojia kwa muadhirika wa tukio hilo.
Mratibu masuala ya jinsia na wanawake Clara Maliwa kutoka UNDP. alisema kuwa kwa kushirikiana kwa pamoja inawezekana kutengezeza mazingira salama, ili kuhakisha upatikanaji haki sawa.
"
Alieleza kuwa, ni muhimu, kuendelea kupambania mafanikio na kila mtu ana jukumu la kuchangia upatikanaji wa haki na usawa wa kijinsia, ili kupinga udhalilishaji dhidi ya wanawake, watoto na hata wanaume, ili kupata zile haki za msingi na kujua sheria zao, " alisema Mwakilishi huyo.
Kupitia mradi huu una lengo la kuwawezesha wale ambao wamepitia katika hali ya udhalilishaji na kuwainua katika kujiendeleza katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo
Mkurugenz wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar 'ZAFELA' Jamila Mahamoud Juma amesema kufungua kampeni hiyo ya siku 16 ya kupiga udhalishaji inahamasisha jamii na hata asasi nyengine ili kupinga udhalilishaji wa kijinsia kwani imeonekana kuongezeka kwa kiasi kubwa katika jamii kwa sasa.
"Tasisi imeanda ziara katika mikoa yote na wilaya ambao ina lengo la kutoa msaada wa kisheria na kujua haki zao za msingi kwa kushirikiana na wadau wengine tasisi za wasaidizi wa sheria na asasi za kisheria.
Madhimisho hayo ya siku 16 ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia yana kauli mbiu isemayo 'Tokomeza ukatili wa Kijinsia chukua Hatua.
MWISHO.
Comments
Post a Comment