Skip to main content

UN-WOMEN YAAHIDI KUENDELEA KUFANYAKAZI NA FAWE-ZANZIBAR

 

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

SHIRIKA la Umoja wa mataifa la UN-Women, limesema litaendelea kufanyakazi na taasisi ya FAWE Zanzibar, kwa maslahi ya kuwasaidia wajasiriali wa mazao, yanayolimwa baharini na nchi kavu.

Hayo yameelezwa jana Febuari 17, 2026 na Mwakilishi wa shirika hilo upande wa Tanzania Emile Kivugo Mwakafundu, alipokuwa akiwasalimia wajasiriamali, wanaoendelea na mafunzo ya mnyonyoro wa thamani, yanayofanyika kituo cha elimu mbadala Wingwi Micheweni Pemba.

Alisema UN-Women ni mdau mkuu wa maendeleo ya jamii, wakiwemo wajasiriamali wa uzalishaji muhogo, majongoo bahari, mwani pamoja na wakulima wa migomba, ili kuziongezea thamani biadhaa hizo.

Alisema, shirika hilo linawajali wajasiriamali hao, ili kuhakikisha wanaziongezea thamani bidhaa zao kwa lengo la kukuza pato lao.



Alieleza kuwa, haiwezekani kwa mkulima, baada ya kuvuna mazao yake, kwenda kuyauza sokoni kama yalivyo, bali ni kuyachakata, ili aongeze pato lake.

‘’UN-Women inaendesha maradi huu wa pamoja kwa lengo la kuhakikisha sasa mkulima ama mjasiriamali, anakuza pato lake,’’alifafanua.

Aidha mwakilishi huyo wa UN-Women alisema mradi huu unaendeshwa mkoa wa kaskazini Pemba na kaskazini Unguja, ili kuwafikia wajasiriamali walioekeza kwenye vilimo hivyo.





Mkufunzi wa mafunzo hayo Shadrack Kikoti, alisema mnyororo wa thamani kwa wajasiriamali wa migomba, mwani, majongoo bahari na muhogo ni muhimu kwa ajili ya kuongeza pato lao.

‘’Muhogo ukilimwa na kisha kuuza kama ulivyo, hauwi na thamani kwa mkulima na hatopata kipato kikubwa, na ndio maana tupo kwenye mafunzo haya kuelekezena hilo,’’alifafanua.

Hata hivyo alisema, zipo njia kadhaa za kuuchakata mwani, ndizi na muhogo ili uwe na thamani na kuongeza pato.

Kwa upande wake Afisa Miradi kutoka FAWE- Hija Hamad Issa, alieleza kuwa washiriki wa mafunzo hayo ni wale wenye mawazo ya biashara, ambao wameshaanza ama bado, ili kujifunza.




Alifafanua kuwa, FAWE imegundua wajasiriamali waliowengi wanawekeza kwenye uzalishaji, ingawa upatikanaji wa kipato chao, uko chini.

Alieleza kuwa, FAWE inayomatumani makubwa, baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, ikiwemo jamii ya wakulima kuongeza pato lao.

‘’FAWE imewaalika wajasiriamali wanaolima muhogo, ndizi, majongoo bahari na mawani, ili kuona mnyororo wa thamani unaongezeka kwao,’’alifafanua.



Hata hivyo aliwataka washiriki hao kuhakikisha, wanakuwa makini darasani, ili kufahamu wanachoelekeza mataalamu, kwa maslahi hayo hapo baadae.

Mapema Afisa Kilimo wilaya ya Micheweni Is-hak Khamis Shaame, alisema ardhi ya Micheweni iliyojengeka ya mawe, haina madhara ya upandaji wa migomba.



‘’Hata kama ardhi ya Micheweni imeumbwa kwa mfano wa mawe, lakini kama ukipata maji kwa kilimo cha migomba ndio pahala pake,’’alifafanua.

Nae mshiriki wa mafunzo hayo Katija Mbaoruk alisema, mafunzo hayo ni mazuri, maana wamekuwa wakitumia nguvu, katika uzalishaji na kupata pato dogo.

Mjumbe wa kikundi cha upandaji migomba cha ‘tujitegemee’ cha shehia ya Majenzi wilaya ya Micheweni Fatma Juma Abdalla, alisema sasa wanakwenda kuongeza pato lao.



Alisema, walidhani wai hawawajibiki kuzichakata na kuzisarifu ndizi, kwa ajili kuongeza pato lao, ingawa baada ya mafunzo hayo, amepata uwelewa.

‘’Mafunzo haya yaliyotayarishwa na FAWE-Zanzibar, kwetu sisi wakulima wa zao la ndizi, yametusaidia mno, maana sasa tumeshaelewa namna ya uchakataji na usarifu,’’alifafanua.

 Mafunzo hayo ya siku nne kwa wajasiriamali hao 20, yanalenga kuimarisha na kuzipandisha thamani bidhaa zao, ikiwemo ya mwani, majongoo bahari, muhogo na indizi.  

                             Mwisho

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...