NA
MWASHAMBA JUMA, (THBUB)@@@@
Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, THBUB ofisi ya Zanzibar, imewajengea
uelewa mpana wanakijiji wa Dunga Kiembeni kuhusu masuala ya uvunjifu wa haki za
binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.
Akizungumza na
wanakijiji hao kwenye mkutano wa pamoja baina ya Tume na wananchi wa Shehia ya
Dunga Kiembeni iliopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Afisa Sheria wa
THBUB Bw. Wilfred Msagati aliwahimiza wananchi hao kutambua haki zao na
kuzipambania pale zinapovunjwa.
Sambamba na
kuwaelekeza kufika Tume kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao endapo
watakupamba na masuala ya uvunjwaji wa haki na ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora.
Wilfred aliyasema
hayo wakati akiwasilisha mada ya “Majukumu ya THBUB” kwa wanajijiji hao pamoja
ya kuwaelimisha haki mbalimbali ambazo binaadamu zinamstahikia na kumuwajibikia
huku akiwafahamisha jinsi ya Tanzania ilivyoridhia mikataba ya kimataifa
kutekeleza haki za binadamu zikiwemo haki za watoto, haki za watu wenye
mahitaji maalumu wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.
Aidha, aliwaeleza wanakijiji hao, mbali na
majukumu mengi yanayotekelezwa na THBIUB pia Tume hiyo ina jukumu la kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za
binadamu, wajibu kwa jamii na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za
binadamu na utawala bora.
Katika mkutano huo
pia, Wilfred aliwaeleza wanakijiji hao jukumu la THBUB kutembelea maeneo
mbalimbali ambayo watu huzuiliwa kwa lengo la kutoa elimu ya haki za binadamu
na misingi ya utawala bora, vikiwemo vyuo vya mafunzo na magereza, maeneo
yanayohifadhiwa wazee kwa lengo la kutunzwa na vituo vya kulelea watoto yatima.
Naye, Afisa Uchunguzi
wa THBUB ofisi ya Zanzibar, Bw. Abdullatif Ali Sheha wakati akiwasilisha mada
ya “Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora” kwa wananchi wa kijiji hicho,
amesema lengo la mkutano huo ni kuwajengea uelewa wnanchi hao ili watambue
masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora.
Pia Bw. Abdul aliwahimiza
wananchi hao kufika Tume kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao pamoja na
kuwaelewesha jinsi ya kuwasilisha mamalamiko hayo Tume ili yapatiwe ufumbuzi.
Kwa upande wa wanchi
hao, waliishukuru THBUB na kuipongeza kwa jitihada zao za kuwafikia wananchi wa
vijijini pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Jumla ya malalamiko
manne ya wanakijiji cha Dunga Kiembeni yalipokelewa katika mkutano huo yakiwemo
matatu ya uvunjifu wa haki za binadamu na lalamiko moja lilihusu ukiukwaji wa
misingi ya utawala bora. Aidha, wananchi wengine waliahidi kufika Tume
kuwasilisha malalamiko yao.
MWISHO
Comments
Post a Comment