Skip to main content

KUCHELEWA KUHAMIA WAJASIRIAMALI KITUO CHA MICHAKAINI, WALIKOSESHA BARAZA LA MANISPAA MILIONI 100

 

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

SHILINGI milioni 107,190,000 zilizotarajiwa kukusanywa na Baraza la Manispaa Chake chake Pemba, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, hazikupatikana, baada ya wajasiriamali kugoma kukitumia kituo chao cha Michakaini, kwa wakati.  

Imebainika kuwa, kituo hicho kipya kilichojengwa kwa ajili yao, kina milango 63 ya maduka, ambapo kila mmoja Baraza lilikusudia kuukodisha kwa shilingi 50,000 ili lijipatie shilingi milioni 3,150,000 kwa kila mwezi mmoja.

Ingawa imebainika, baada ya wajasiriamali hao kukataa kuingia kituoni humo, Baraza hilo, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, limeshapoteza shilingi milioni 85,050,000.

Aidha mapato ya shilingi ya milioni 22,140,000 nayo hayakukusanywa na Baraza hilo kwa kipindi hicho, yaliokuwa yatokane na vizimba ‘vikuta’ 82, ambapo kila kimoja, kilitarajiwa kukukodishwa kwa shilingi 10,000 kwa wajasiriamali.

Ikafahamika kuwa, vikuta hivyo kama vyengepata wajasiriamali, kwa mwezi mmoja Baraza lingekusanya shilingi 820,000, sawa na jumla shilingi milioni 3,970,000 ijumuisha na kodi ya milango 63.

Ndani ya kituo hicho kilichofunguliwa mwezi Novemba mwaka 2023, Baraza la Manispaa lilitarajia wajasiriamali wa nguo za mtumba na wauza viatu, wakitumie kituo hicho, na kuanza kulipia vikuta 82 na milango 63.

Na ndio maana baada ya wajasiriamali hao wa mji wa Chake chake kugoma kikutimia kituo hicho, walilisababishia Baraza la Manispaa hilo, kupoteza mapato ya zaidi ya shilingi milioni 107.190 kwa fremu 63 za milango na vizimba 82.

Uchunguzi ulibaibi kuwa, baada ya kufunguliwa kwa kituo hicho mwezi Oktoba mwaka 2023, mwezi uliofuata Baraza hilo la Manispaa, lilianza kuwahamisha wajasirimali, hasa wauza mitumba na viatu kuhamia kituoni hapo.



Kwa wakati huo Askari na uongozi mzima wa Baraza la Manispaa, lilihamia ndani ya mji wa Chake chake, ili kuwasaka wajasiriamali, wanaopanga bidhaa zao chini na kuwaomba kuingia kituoni hapo.

Msaidizi Ofisa Mapato wa Baraza hilo, Said Mabrouk Juma, alikiri kuwa, kulikuwa na ugumu kwa wajasiriamali wa nguo za mtumba, viatu na urembo kukitumi kituo hicho.

’Pamoja na kuwatumia hata askari wa jiji na wakati mwingine na Mkurugenzi kuwapitia, lakini walikataa na sisi kuendelea kupoteza mapato,’’alifafanua.

Alieleza kuwa, baada ya kugoma kuingia kituoni hapo, waliwaomba tena kwa mara nyingine, kwa sharti la kuwaondolea kodi, na kuwaomba kuchangia fedha ya umeme shilingi 20,000 na kukubali.

‘’Wapo waliokubali kuingia kituoni hapo, ingawa walituomba na kukubalia nao, kwamba wasitozwe kodi na badala yake wachangia huduma ya umeme, na hadi sasa hilo linaendelea,’’alifafanua.

Mkurugenzi wa Baraza hilo Shida Kombo Mohamed, alisema kuanzia mwezi Januari mwaka 2025, rasmi walipokubaliana na wajasiriamali hao, kuchangia gharama za umeme, kwa kila aliyekodi mlango.

‘’Ni kweli wakati wanahamia kituoni hapo, hata biashara ilikuwa chini kwa kukosa wateja, na ndio maana tuliwaomba kuchangia huduma umeme, kwa shilingi 20,000 kwa mwezi,’’alifafanua.


Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema wanampango kuanzia mwezi ujao, kila mlango mmoja, kuuwekea mita yake ya umeme, ili kuondoa changamoto ya matumizi kama yaliyopo sasa.

‘’Kwa sasa mchango wa umeme uko sawasawa kwa kila mjasiriamali, ingawa baada ya kushauriwa kuhusu kila mmoja kuwa na mita yake, tumelikubali na harakati zimeshaanza,’’alifafanua.

Baadhi ya wajasiriamali waliopo kituoni hapo, walikiri kuwa walikosa uwelewa na kuchelewa kuhamia ndani ya kituo hicho, jambo lililochelewa kupanua biashara zao.

Hija Omar Khamis, alisema kwa sasa biashara eneo hilo imetononoka, baada ya wateja kuzoea kituoni hapo, tokea walipohamia mwezi Januari mwaka jana.

Kwa upande wake Khadija Sultan, alisema umaarufu wa bidhaa za nguo za mtumba kituoni hapo, kinaendelea kukua, kadiri siku zinavyosonga mbele.


‘’Ni kweli pale mwanzo, tulipokuwa tukiondolewa ndani ya mji wa Chake chake, tuliona kama tunaonewa, ingawa sasa biashara imechangamka kiasi,’’alieleza.

Kituo hicho cha wajasiriamalia Chake chake, ambacho kina milango 63 na vizimba 82, kilifunguliwa mwezi Okatoba mwaka 2023, kimejanga na serikali ya awamu ya nane, kwa lengo la kuwapa utulivu wajasiriamali.

                mwisho   

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...