UPO usemi maarufu kuwa, uchumi wa mwanamme ni wake pekee, lakini
wa mwanamke ni wa jamii
Wacha tuone,
ushahidi wa hili, maana Mwanaisha Haji Makame (78) wa shehia ya Mchanga mdogo,
anasema huo ndio ukweli.
‘’Haikuwa
ni methali tu hizi za watu wa kale, bali ukweli wake upo na unanafasi hadi kwa
wanawake na jamii ya leo.
Anafafanua
kuwa, mwanamke anapokuwa na mali, huwa ni jamii, kutokana na huruma na upeo
wake wa maisha ya sasa na baadae.
Hili linaungwa
mkono na Mchanga Said Shamisi (55) nae wa Mchanga mdogo wilaya ya Wete, akisema
ukitaka jamii isiishi na umaskini, wawezeshe wanawake.
Makame
Ussi Makame (40), nae wa eneo hilo, ijapokuwa mitheli hiyo haikuikubali kwa asilimia
100, lakini haikatai kwa asilimia hizo pia.
Aisha
Hassan Mohamed (19), anasema misemo ya watu wa zamani, ilikuwa na ukweli, na na
hiyo inaendelea kuishi hadi sasa.
‘’Kwa
mfano Chama cha waandishi wa habari Tanzania TAMWA-Zanzibar, ilipoendesha
mafunzo ya kilimo msitu, nilipata posho, nilijumuika na wanafamilia,’’anafafanua.
Kassim
Mohamed Kassim (22), yeye hakubaliana na hilo, alisema mali ya mwanamme ndio huwa
ya jamii, kwa kule kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.
‘’Mimi
pesa yangu kwa mfani huenea kwa wake zangu wanne, na wao kama wanafamilia
wanaweza kupata, kupitia yangu, jee,’’anahoji.
Mkurugenzi
wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, anakubali moja kwa moja, kuwa mali ya
mwanamke inaweza kuwa ya familia.
Anasema
kwani, wanawake ni nyenzo Madhubuti na kiunganishi cha familia moja na
nyingine, na kwa kule kuwa madbubuti na imara wa uchumi, jamii hula kupitia yeye.
‘’Ndio
maana fedha ya mwanamke, ikipatikana inaweza kuzaa mali nyingine, kuliko ya
awali,’’anasema.
Pamoja na kuwepo mafanikio na juhudi za
wanawake katika sehemu kadhaa, ikiwemo za kiuchumi, na kijamii bado inaonekana
suala la mabadiliko ya tabianchi, linaendelea kuwa na madhara makubwa kwa
wanawake.
Wanawake
wanazidi kuonekana kama watu walio katika hatari zaidi ya kuathirika na
mabadiliko ya tabianchi, kuliko wanaume, kwani wengi wao ndio wategemezi.
Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wanawake pia ni watu wa kwanza kuhisi
madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Kwa
mfano chini Kenya, baadhi ya wanawakewanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 10,
kutafuta kile wanachohitaji, ili kulisha familia zao pamoja na kutafuta
maji.
Matumaini
ya wanawake wa kisiwa cha Pemba shehia ya Chwale Wilaya ya Wete ni kukabiliana
na mabadiliko ya tabia ya nchi, kwa kujikita katika kilimo msitu.
Wanawake
hawa, wameweka matumaini makubwa juu ya umuhimu wa kilimo msitu huku wakiamini
ndio mkombozi mkubwa wa maisha yao.
Ingawa
wanawake hao ni wale waliomo kwenye mradi unaoendeshwa na Jumuiya ya Uhifadhi
wa misitu Pemba ‘CFI’ na ‘CFP’ wanaofanyakazi kwa karibu na TAMWA Zanzibar, na
hasa baada ya serikali ya Canada kutoa fedha na Serikali ya Zanzibar
kuridhia.
Pamoja
na kwamba mradi huo imeanza kwa shehia nane kwa Unguja na Pemba, ikiwemo
wanawake wa shehia za Mchanga mdogo, Kambini, Kiuyu minungwini na Chwale kwa
Pemba.
Sasa
wanawake wa maeneo hayo wameshaamka na kujikita katika harakati za kilimo
hicho, ambacho wanasema iwapo watakiendeleza watakuwa na uhakika wa kuyamudu
maisha yao.
Kilimo
msitu amabacho ni mchanaganyiko wa mazao mbalimbali kama migomba, minanasi,
mbazi, michikichi, njugu, mahindi na miembe.
Rehema
Salim Issa wa Chwale Weete anasema, kilimo msitu kinawapa uhakika wa chakula
katika maisha yake.
Ingawa
kilimo hicho kimekabiliwa na athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi bado
wanaendelea nacho.
Anaona
pamoja na kuonesha juhudi, kubwa katika kilimo hicho bado mabadiliko ya
tabianchi yanawaathiri, ikiwemo jua kali na kupelekea kilimo chao kuharibika.
Anasema
suala la jua kali limechangia kutokuwa na maji na vipando kupotea kwa haraka,
jambo ambalo hukabiliwa na ongezeko la umaskini.
"Kilimo
hichi tunakitegemea kujikwamua na umaskini kwani tunapata chakula, ila jua kali
limetukosesha kupata maji na imechangiwa miti kufa,’’anasema.
Mkulima
kiongozi Hadia Omar Haji wa kijijini hapo, anasema kilimo hicho kinawanufaisha
kwa muda tofauti ikiwemo muda mfupi, kati na mrefu.
Kumbe,
ili waweze kunufaika kama ilivyo maumbile ya kilimo hicho, huduma ya maji ya
kumwagilia ni muhimu.
“Kusema
kweli tatizo la mabadiliko ya tabianchi yanatuweka katika hali ngumu, kwani
sasa ni jua hatujui ikija mvua itakuwaje,’’anaeleza.
Kwa
vile wanawake ndio wakaaji wa nyumbani kuliko wanaume, hutumia muda mkubwa
kuwashughulikia watoto kwenye mambo mengi, ikiwemo kula.
"Wenzetu
wanaume si sana kuteswa na njaa kwani wao si wakaaji wa nyumbani, kama tulivyo
wanawake na watoto wetu yeye akitoka hupata cha
kujitafunia,"anasema.
Bikombo
Khamis Hamad anasema kuwekeza kwa wanawake na wasichana, kunaleta matokeo
makubwa ambayo yanaigusa jamii, na maarifa waliyonayo wanawake yanahitajika
sasa kuliko wakati mwingine.
WANAUME WANAMCHANGO UPI KUSIAIDA WANAWAKE KUPATA ARADHI
Ali Khamis Juma wa shehia ya Mchanga mdogo, anasema baada kumuona mke wake, anahangaika kusaka ardhi ya kilimo, alikopa fedha na kumnunulia.
''Nilimnunulia mke wangu ardhi na nimemuandikia yeye, na sasa ameshaanza kilimo mseto, akiwa na ardhi yake, ingawa ni upana wa uwanja wa mpira nusu,''anasema.
Khalid Juma Makame wa Kambini, anasema mradi wa ZANADAPT, umekuja kuwakumbusha wajibu wao, na sasa baada ya kufariki baba yao miaka mwili, wameamua kurithi.
''Ni kweli sasa tumsharithi na mdogo wangu Aisha amepata ardhi yake na ameshalima miparachichi 10 na migomba ya mkono 20,''anasema.
Nae Hija Khamis Khamis anasema, ijapokuwa hawajakamilisha taratibu za kurithi, lakini kwa sasa wako mbioni ili kuhakikisha dada yake anapa haki yake ikiweko ardhi.
Kassim Juma Hemed na Haji Makame Haji, wanasema ijapokuwa hawana ardhi za kurithi wala uwezo wa kununulia wake zao ardhi, lakini wamewapa ushauri.
''Kwa mfano mimi mke wangu, tumepanga mwakani tukodi mikarafuu, na fedha tutakayoipata tununune ardhi kwa ajili ya kilimo,'amasema Haji.
FAIDA
YA KILIMO HICHO
Mkulima
anaweza kunufaika na kilimo msitu kwa kumpatia mahitaji yake ya msingi kama
vile kuni, matunda, kurutubisha udongo malisho ya mifugo, dawa za asili.
Nyingine
ni usindikaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya misitu kama vile juisi, jamu na
asali.
Mkurugenzi
wa Jumuiya ya uhifadhi wa misitu Pemba Mbarouk Mussa, anasema
kutopatikana kwa mvua, kukata miti ni jambo jingine linaloendelea kuathiri.
Anasema
athari mbalimbali za ukataji wa miti kwa shughuli za kijamii, zimekuwa
zikijitokeza katika maeneo tofauti, huku jumuiya hiyo
ikiendelea kutoa elimu.
Afisa
kilimo kutoka CFP Saada Juma, anasema kupitia mradi huo haujabaguwa,
ingawa lengo ni kuwainuwa wanawake katika shughuli za kujitafutia
kipato.
Afisa
mdhamini Wizara ya kilimo, umwagiliaji Maliasili na Mifugo
Muhandisi Idriss Hassan Abdulla, anafafanuwa kuwa,
wameandaa mpango maalum wa kuhakikisha wanazalisha kupitia kilimo msitu.
WANAUME WANASEMAJE
Hamad
Ali Suleiman, anasema wanatambua mchango mkubwa wa wanawake, katika kukiendesha
kilimo msitu kwani hawako nyuma katika kuhakikisha kinaendelea.
Juma
Omar Hassan, anawashauri wanaume kuwaruhusu wanawake, kujiingiza katika kilimo
hicho na ili waweze kujikwamua na maisha.
Chama
cha waandishi wa Habari wanawake TAMWA Zanzibar, nao husimamia kidete
haki za upatikanaji wa usawa wa kijinsia na kuwashirikisha wanawake.
Mkuu
wa mawasiliano na Habari TAMWA Sofia Ngalapi anawataka wakulima hao, wasikae
kimya, katika kueleza changamoto zinazowakwaza katika kilimo chao.
mwisho





Comments
Post a Comment