NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
MATUMAIANI huonekana
sehemu zenye bahari kwa kuwepo aina ya miti ya mikoko, pembezoni wa bahari.
Zanzibar, kwa
sasa kuna uhutaji wa elimu juu ya uwoto wa asili, kwani hupoteza twasira
ya mazingira na uharibifu ya bahari.
Matumaini
ya wanawake wa kisiwa cha Pemba shehia ya Mchangamdogo ni kukabiliana
na mabadiliko ya tabia ya nchi, kwa kujikita katika kilimo msitu cha
upandaji wa miti ya mikoko.
Mikoko
ni misitu inayopatikana katika nchi za joto sana na la kiasi, ambayo
inaweza kuota na kumea katika maeneo ya maji chumvi, ambayo yapo katika
ukanda unaofikiwa na maji kujaa na kutoka na kupwa.
Mikoko
inaweza kuishi kwa kufunikwa na maji kujaa na kutoka, imejiweka maumbile
maalum inayowezesha kustawi katika mazingira yenye changamoto.
Zanzibar
inayo karibu hekari 18,000 za msitu wa mikoko hekari 6,000 zipo katika kisiwa
cha Unguja na hakari 12,000 katika kisiwa cha Pemba.
Maeneo
makubwa kabisa ya mikoko katika kisiwa cha Unguja yapo katika Ghuba ya
Chwaka na kisiwa cha Pemba ni Ngezi na Micheweni.
Alisema
Afisa Program kutoka TAMWA Zanzibar Hairat Haji, kuwa mikoko ina
umuhimu kwa maisha ya binadamu na maisha ya viumbe vya baharini.
Maana
miti hiyo, hutoa makaazi ya uvuvi kwa kutumika kama vitalu vya samaki kwa hatua
ya awali,mabaki ya miti na bakteria wanaopatikana majini hurundika chini
ya mikoko na hua ni chanzo ya chakula na kimbilio la samaki wachanga.
Kimataifa
mikoko inathaminiwa kwa kiwango cha doola 200 -900 kwa hekari, kutokana
na huduma zao za kimaumbile.
Wale
waliopo katika jamii za pwani wana uhusiano wa karibu sana na utegemezijuu ya
mikoko kwa maisha yao na kujipatia fedha.
Mradi
wa miezi 30, unaoendeshwa na Juamuiya ya Uhifadhi wa misitu Pemba
‘CFI’wanaofanyakazi kwa karibu na TAMWA Zanzibar, na hasa baada ya serikali ya Canada
kutoa fedha na Serikali ya Zanzibar kuridhia.
WANUFAIKA
Asha
Haji Hussein mkaazi wa shehia ya Mjini kiuyu Wete, anajishughulisha
na kazi za uhifadhi wa mazingira, ili kujipatia kipato na kutarajia
kujiwezesha kiuchumi.
‘’Hatuhitaji
kuiua mikoko kutokana na faida zake za kiuchumi, jamii kuacha hii tabia ya
kukata na kuharibu maeneo ya pwani, kwani tunapoteza kitega iuchumi,’’anasema.
Wanyama
pori, katika eneo la hifadhi ya Jozani–Chwaka,wamejenga mabao kwa watembea
miguu, kwenye mikoko inayowawezesha wageni kutembea katika misitu kwa
kuona miti,ndege kaa na viumbe vyengine.
Mkurugenzi
wa Jumuiya ya uhifadhi wa misitu kisiwani Pemba (CFP) Mbarouk
Mussa, anasema athari mbali mbali za ukataji wa miti ya mikoko kwa
shuguli za kijamii zimekuwa zikijitokeza katika maeneo tofauti.
‘’Vipi jamii
itajipanga katika kukabiliana na mbadiliko ya tabia ya nchi yaliyopo kwa sasa
jitihada mbali mbali za kiserikali zinatuka kwa kushirikiana na
mabadiliko ya tabia ya nchi,’’anasema.
Kazi
ya ulinzi ya mizizi ya mikoko haiwezi kubadilishwa,na kutokuwepo kwao kunaweka
makazi ya pwani kwa hatari kubwa kutokana na kupanda kwa
viwango vya bahari, na matukio mabaya ya hali hewa.
Wanawake
hao wa shehia ya Mchangamdogo walieleza matarajio yao kupitia mradi
wa ZANADAPT wa uwoteshaji wa mikoko ni katika kujiongezea kipoto chao na
kujikomboa kiuchumi.
Mwajuma
Ali Hamad, anasema kupitia mikoko tunapata kuongeza pato la
kiuchumi, kwani mikoko ni chanzo cha mapato kwa jamii zinazozunguka eneo
la bahari.
Hussan
Mohamed Issa yeye ni mkazi wa Mchanga mdogo anaeleza kuwa kupitia
mikoko wana hakika na hasa baada ya kuelimishw akupitia mradi huo wa miezi
30, itawasaidia katika uhifadhi wa uvuvi.
Mradi
wa ZANADAPT ambao unahusisha upandaji wa mikoko utatusaidia katika kupunguza
umaskini, na kumudu mazingiara yao ya kipato.
‘’Mikoko
(Mikandaa), inasaidia kupunguza hewa ya kaboni dioksidi na kupata hewa safi ni
muhimu kuhakikisha tunapanda mikoko na uhufadhi wa mazingira,’’anafafanua.
Sera mbali mbali
ambazo Serikali zinahakikisha zinasaidia kukabiliana na mabadiliko ya mazingira
na tabia ya nchi,pamoja na kuimarisha usimamizi wa kodi na kuimarisha sekta ya
fedha na sera ya uchumi .
Serikali
imejipanga kuhakikisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) na Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) zinapata usajili
mfuko wa kuhimili mabadiliko Tabianchi (GCF).
Katika
harakati za kukabiliana na mabadiliko hayo, ipo miradi mbali mbali ya
ujenzi wa miundombinu ya kuzuiya mawimbi ya bahari, kuingia nchi kavu(
Sipwese) wilaya ya MkoaniPemba.
Makakati
mwingine ni mradi kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo Ikolijia
(EBARR) Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja na mradi wa kurejesha ardhi
iliyoharibika na kuongeza usalam wa Chakula (LDFS)unaotekelezwa katika
wilaya ya Micheweni Pemba.
Hayo
yalielezwa na aliyekuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na mazingira ) Dk.Suleiman Jafo, akijibu
swali la Mbunge wa viti Maalum Maryam Azani Mwinyi aliyeuliza wakati
wakiwa bungeni.
CFP
INASEMAJE?
Saada
Juma Afisa kilimo kutoka CPF, amesema mradi umelenga watu wote hauja bagua na
lengo ni kuwainua wanawake katika shughuli za kujitafutia kipato cha
halali.
‘’Shughuli
za ugawaji wa mbegu za kilimo msitu katika shehia( 4 ) hufanyika kika baada ya
wiki ama mwezi, ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa mbegu hizo kwa
walengwa,’’anaeleza.
Sheha
wa Kambini Ali Omar Ali, anaelezakuwa Serikali inachukuwa hatua mbali mbali za
kuhakikisha wananchi wanapata elimu na kuanda mikakati kazi ya kupambana na
mabadiliko ya tabianchi.
Jamii
hutumia rasili mali hiyo ya mikoko kwa mambo mengi ,baadhi ya matumizi
haya yanatokana na mila za miaka mingi na ni matumizi yanayosarifika ya makazi.
ZANADAPT wenye lengo la kuwafikia
wajasiriamali zaidi ya 4,000 sawa na kila wanaufaika 80 wakiwa
wanawake, kila 100 waliomo kwenye maradi
Mwisho




Comments
Post a Comment