NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
TUPO
katika ulimwengu ambao mara nyingi mafanikio ya mtu kimaisha huhusishwa na
elimu.
Sio
tu ya utambuzi wa mazingira, bali na ile ipatikanayo darasani.
Kupata elimu hiyo kwa Zanzibar si changamoto hasa
baada ya kufanya mapinduzi yake mwaka 1964, na kuanza kujitawala.
Kwani katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu 10 (f),
kinasisitiza kuwa Serikali inawajibu wa kutoa
fursa za kielimu kwa watu wote
katika madaraja yote.
Katika hili, hakuna aliebaguliwa kwa sababu yeyote ile, lengo likiwa ni kumjumuisha
kila mtu wakiwemo wenye ulemavu.
Kwani baadhi ya watu, walidhani kwa watu wenye
ulemavu kusoma ni anasa na sio muhimu.
Ndipo mikataba ya kimataifa na kikanda, sheria, pamoja
sera mbali mbali zikazungumzia haki ya elimu kwa watu hawa.
Mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu wa mwaka
2006, katika ibara ya 24 imezitaka nchi wanachama kuhakikisha watu wenye
ulemavu wanapata elimu.
"Nchi wanachama zihakikishe mfumo wa elimu
hauwatengi watu wenye ulemavu na watoto wenye ulemavu hawabaguliwi kwa misingi
ya ulemavu wao", kimeeleza kifungu cha 2 (a) cha ibara hiyo.
Sheria ya watu wenye ulemavu ya Zanzibar nambari 8 ya
2022 kifungu cha 28 (1) (a) kimeeleza,
watu wenye ulemavu wanastahili haki zote za msingi za kibinaadamu, kama ilivyo
kwa wingine ikiwemo ya elimu.
Aidha, sera ya elimu ya Zanzibar ya 2006 inasisitiza
Wizara ya Elimu itahakikisha haki na fursa za elimu inazotoa kwa wazanzibari
wote, zinatolewa kwa misingi ile ile kwa watu wenye ulemavu.
“Ulemavu kwa kadri itakavyowezekana hautakua kikwazo
wala sababu ya kumnyima mwanadamu haki ya elimu, " imeeza sehemu ya sera
hiyo.
Kwa bahati nzuri haki hii haikutolewa kwa mtu mwenye
aina fulani ya ulemavu, ikiwa na maana ulemavu wa aina yeyote si kikwazo cha
mtu kupata elimu.
Je?
utekelezaji wa hili ukoje kwa wanafunzi wenye ulemavu wa uoni?
Said Salum Khamis mwanafunzi wa skuli ya Elimu Mjumuisho
Pujini mwenye ulemavu wa uoni hafifu anasema, haki ya elimu kwasasa wanaipata.
Anasema ipo skuli anayosoma inamiundombinu rafiki kwao,
ikiwa ni waalimu wenye taaluma, vifaa na miundombinu rafiki ya majengo.
Nasria Ali Salim mwanafunzi mwenye ulemavu wa uoni
katika skulini hapo, anasema anafursa ya kujifunza kwa uhuru, kama ilivyo kwa
wanafunzi wingine wasio na ulemavu.
Anaeleza kuwepo kwa skuli hiyo inayowajumuisha kunawawezesha
kujifunza na kutimiza ndoto na malengo
waliyojiwekea.
“Wenye ulemavu wa uoni tunafaraja kwani
tunajifunza kama ilivyo kwa wingine
wasio na ulemavu, na naamini ni fursa ya
kutimiza ndoto tulizojiwekea”, alieleza.
Anaipongeza serikali kwa kuanzisha skuli hiyo kwani
inaonyesha kujali kwao umuhimu wa upatikanaji wa elimu kwa kila mtoto katika
jamiii.
WAZAZI
Salim Kassim wa Tasini Mkoani Pemba ni mzazi wa mwanafunzi
mwenye ulemavu wa uoni anasema, ujumuishaji watu wenye ulemavu katika elimu umekuja
kuwakomboa watoto wao.
Maana kabla walikua na hofu ya kutopatikana haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu wa uoni, kwa
kutokuwepo miundombinu rafiki ya kujifunzia katika skuli za kawaida.
Sabiha Issa Mohamed wa Mjimbini ni mzazi wa mwanafunzi mwenye ulemavu wa uoni anasema, juhudi za kuwajumuisha watoto wenye ulemavu
katika elimu zinafanyika na zimewapa
faraja.
Kwa sasa watoto wanapata fursa ya kujifunza bila
kujali hali zao na maeneo wanayoishi, kutokana na kuanzishwa skuli ya elimu
mjumuisho.
"Kwa sasa watoto wetu wenye ulemavu wa uoni
wanayo fursa ya kusoma, hii inaleta faraja kwetu wazazi, kwani elimu ndio urithi
pekee wa kuwaachia watoto", anaeleza.
WAALIMU
Hanifa Abeid Ali mwalimu wa wanafunzi wenye ulemavu wa
uoni skuli ya Elimu Mjumuisho Pujini anasema, uanzishwaji skuli hiyo, ni
miongoni mwa juhudi za utekelezwaji sera ya elimu mjumuisho.
Anasema katika kuhakikisha wenye ulemavu wa uoni
wanapata haki yao ya elimu, skuli imekua ikisajili wanafunzi wenye ulemavu huo,
kila mwaka tokea kuanzishwa kwake.
Hadi sasa skuli
ina wanafunzi 17 wenye ulemavu wa uoni , nane kati yao ni wasioona
kabisa na tisa ni wenye uoni hafifu.
Tamima Mohamed Said mwalimu wa wanafunzi wasiiona katika
skuli hiyo anasema, vipo vifaa mbali mbali vya kufundishia na kujifunzia, kwa
ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa uoni.
Vifaa kama mashine za kuandikia, fremu za A4, vibao
maalumu vya kusomea vyenye nukta nundu,
vifaa vya kukuzia herufi (magnifier) pamoja na mashine za kutolea vivuli kwa ajili
ya kutayarishia mitihani.
CHANGAMOTO NI ZIPI
Moja ni uchakavu wa baadhi ya mashine hizo na upungufu
wa karatasi za rangi za kuandikia kwa wenye uoni hafifu.
"Upatikanaji elimu hapa unawazingatia wanafunzi
wasiiona na wenye uoni hafifu, na wanafursa ya kujifunza, tunavifaa vya
kufundishia na kujifunzia,’’anasema mwalimu huyo.
Nae Mwalimu Anipae Ameir Manallah wa skuli hiyo anasema, wanawekaweka uangalizi wa hali ya
juu wanapokua darasani wanafunzi hao, kwa kuingia waalimu wawili wawili, ili
kila mwanafunzi apate uwelewa wa kutosha.
Anasema katika ufundishaji wao huzingatia mahitaji ya kila mwanafuzi kwani
darasa lao ni jumuishi.
WIZARA
Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba Mohamed Nassor
Salim anasema, serikali imeweka mazingira wezeshi na vifaa kwa wanafunzi wenye
ulemavu wa uoni vya kujifunzia na kufundishia.
Anasema katika skuli zenye wanafunzi hao wameweka mashine za nukta nundu za kuandikia, vibao malumu
vyenye nuktanundu kwa ajili ya kujifunzia, fremu za A4 na vifaa vyengine
muhimu.
Wizara itahakikisha inatatua changamoto zilizomo
katika skuli hizo ikiwemo ya vifaa chakavu, maana elimu ni haki ya msingi kwa wote.
Hutuba ya bajeti ya wizra hiyo ya 2025/2026 iliyosomwa
katika baraza la wawakilishi na waziri wa wizara hiyo Lela Muhamed Mussa, anasema,
mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
yameimarika.
Sehemu ya hutuba hiyo inaeleza, idadi ya walimu
waliopatiwa mafunzo ya elimu mjumuisho na stadi za maisha kwa mwaka imeongezeka
kutoka 1,066 mwaka 2024/25 hadi 1,774 mwaka 2025/26.
JUMUIA
ZA WATU WENYE ULEMAVU
Mashavu Juma Mabrouk Mratibu wa Baraza la watu wenye
ulemavu anasema, upatikanaji haki ya elimu kwa wenye ulemavu unaendelea kumarika
hasa kwa skuli za elimu mjumuisho.
Anasema ni vyema serikali ikaongeza nguvu katika skuli
za kawaida, ili wenye ulemavu
wajumuishwe kwa kila kitu kinachofanyika
kupitia skuli wanazosoma.
MWISHO
Katika Makala haya tunawaangazia baadhi ya watu wenye
ulemavu ambao wamekuwa mashuhuri kwa kushinda changamoto ya ulemavu na kufikia
mafanikio ya hali ya juu katika Nyanja zao. Hawa ni baadhi yao.
Comments
Post a Comment