NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
SERIKALI kwa kushirikirikiana na wadau wa ndani na nje,
wanayo mikakati ya kweli ya kuhakikisha, kilimo mseto kinawanufaisha wanawake
Pemba.
Kwa sasa mradi wa kuwawezesha wanawake kukabiliana na mabadiliko
tabia nchi, na kukidhi maisha yao, unaendeshwa na taasisi kadhaa na TAMWA ukiwemo
upo shehia nne kwa Pemba.
Kati hizo ni za Mchanga mdogo, Kambini zote zikiwa mkoa wa
kaskazini Pemba, ndani ya wilaya ya Wete.
Hili lilikuja baada ya tafiti kadhaa, kuonesha maeneo hayo
ndio makuu yalioathiriwa na mabadiliko tabia nchi, yawe yale ya asili au
yaliosababishwa na harakati za mwanadamu.
Kilimo mseto kilitajwa na wataalamu kuwa, ndio mwarubaini
wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi, kwa kule kuhifadhi mazingira na kujipatia
kipato.
KWANI KILIMO MSETO NI KIPI?
Mfumo huu waweza
kuandaliwa kwa zamu au hata kujumuishwa kwa pamoja bila kuzingatia msimu.
Ikaelezwa kuwa, mifugo
na mimea ya chakula hujumuishwa kama sehemu ya mfumo huo, ili kuhakikisha
mkulima anaendesha kilimo bila ya njaa.
Kumbukuka kuwa, ni muhimu kufahamu kwamba
hakuna njia moja ya kuimarisha na kufanikisha kilimo, bali mbinu za kila aina
zapaswa kutekelezwa.
Mbinu hizi zaweza
kujumuisha jamii nzima katika kupanda miti ya kienyeji, miti mingine yenye
manufaa, mbinu za kutunza udongo.
Na njia nyinginezo
za kuimarisha kilimo cha mseto, ambapo faida yake nyingine ni kunufaisha sehemu
kame, zile zisizotumika kwa kikamilifu au hata zile za tindikali au udongo wa
chumvi nyingi.
SERIKALI INAFANYA NINI
Afisa mdhamini wizara ya kilimo
Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Injinia Idriss
Hassan Abdulla anasema kilimo msitu kitawapa faida wanawake, kwani kitaifanya
ardhi kuwa na rutba na kupatikana mazao kwa wingi.
‘’Unapolima kilimo mchanganyiko kutasaidia kupatikana kwa
mvua, na kusaidia kupatikana kwa mazao kwa wingi,’’anaeleza.
Kama wizara wamekua wakitoa elimu kwa vikundi mbalimbali
ya utunzaji mazingira ili kuona wanawake wanapiga hatua kupitia kilimo msitu.
Aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbrouk Khatib amasema, kilimo msitu (mseto)
kitawainua kwa kiasi kikubwa wanawake kiuchumi.
‘’Ukilima tembere utapata mboga, ukipanda miembe utavuna
embe utauza utapata pesa za kununua mahitaji mingine ya
nyumbani,’’anafahamisha.
Juma Bakar Alawi mdau wa mazingira, anasema wanawake
ndio wathirika wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Anasema kupitia mradi huo wa uhifadhi mazingira
utawasaidia wanawake kujikwamua na umasikini.
‘’Kwakweli jambo wanalolifanya Jumuia ya uhifadhi wa misitu
Pemba ‘CFP’ na wenzao wa kimataifa wa ‘CFI’ la kuleta mradi huu, ni
jambo jema.
Kwani anasema wanawake watajipatia mahitaji ikiwemo kuni,
na fedha za kujikimu kimaisha, kwani ndio wahanga ya umaskini,’’anasema.
Rehema Abrahman Alawi ni Afisa
kutoka CFP anasema mradi wao umelenga zaidi
kwa wanawake kwani wao ndio waathirika
wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi.
Wamekuwa wakiwapatia elimu pamoja na
miche waweze kulima kilimo msitu, kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.
‘’Unapomwambia mama apande miti ya misitu katika
shamba lake, atajipatia mahitaji muhimu, ikiwemo fedha kidogo
anakuelewa,’’anafafanua.
Hashim Haji Omar,
anasema kilimo msitu kitawasaidia wanawake kujikomboa na umasikini, huku
wakiimarisha familia zao.
Wanapolima mazao mchanganyiko katika mashamba yao,
watapata chakula, pesa, pamoja na kupata hewa safi.
‘’Kwakweli kilimo msitu kitawafanya wanawake wapige hatua,
kwani watavuna mazao kwa ajili ya chakula, biashara, pamoja na kufahamu
umuhimu wa kutunza mazingira,’’anafafanua.
Kisiwa cha Pemba ni moja ya kisiwa ambacho kimekua ni
muhanga mkubwa wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Mkurugenzi wa Jumuia ya ‘CFP’ Mbarouk
Mussa Omar anasema kama hakutochukuliwa jitihada
zozote, juu ya mabadiliko ya tabianchi, itakuja
kusababisha baadhi ya vijiji kuhamwa kutokana na maji ya bahari kupanda kwenye
majumba.
‘’Katika kijiji cha Mjini kiuyu kila ifikapo mwezi 13,14,
na 15 maji ya chumvi yanaigia ndani ya majumba,’’anasema.
Nairat
Abdulla Ali Afisa kutoka Chama cha wandishi
wa habari wanawake TAMWA Zanzibar anashauri,
kwa wanawake walionufaika na taalum, kuiendeleza.
Anasema, kinyume chake watarudi tena kwenye umaskini, huku
wakipata msongo wa mawazo, kwa athari za mabadiliko tabia nchi.
Mradi ambao umefadhiliwa na
Serikali ya Canada na kuridhiwa na serikali ya Mapinduzi,
kuona wanawake wamepiga hatua.
Kwani lengo hasa la mradi ni kuwainua
wanawake kiuchumi, kupitia mradi huo wa
uhifadhi wa mazingira.
Kufikia Desemba
mwaka 2022, kumekuwa na kesi 2,180
zinazohusiana na mazingira, zilizowasilishwa kwa
taasisi za sheria 65 kote duniani:
Ripoti ya
Benki ya Dunia inasisitiza umuhimu wa
kuunganisha masuala ya tabianchi katika mipango
ya maendeleo ya Tanzania kupitia Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050
Ambapo moja ya mkakati wa ripoti hiyo ni kusaidia
jamii zilizohatarini, kuwa na uwezo wa kuhimili
mishituko ya tabianchi.
Aidha kunaweza kusababisha watu milioni 2.6
kuingia kwenye umasikini, na wengine milioni
13 kulazimika kuhama makazi yao nchini.
TAMWA, imekuwa na nafasi kubwa ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari, katika mradi huu ulioukingoni, na sasa wameshawiva.
Fatma Hamada wa blog ya Pemba ya leo na Habiba Zarali wa
Zanzibar leo, wanakiri kuongeza uweledi kwenye kuandika bahari za mabadiliko
tabia nchi.
mwisho
Comments
Post a Comment