Skip to main content

RC KUSINI PEMBA: WAANDISHI WA HABARI YAELEZENI MAFANIKIO YALIOPO

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

WADAU wa habari kisiwani Pemba, wametakiwa kutumia taaluma zao  katika kuelimisha jamii kuhusu maendeleo  yalioyopatikana ndani ya awamu ya nane ya Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini  ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Hayo yalielezwa jana Juni 21, 2025 na  Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid kwenye kongamano   la wadau wa habari, lililofanyika katika ukumbi wa "ZRA" Gombani Chake chake Pemba. 

Alisema ipo haja ya wanahabari  kutumia taaluma zao vizuri, ili  kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wananchi, hasa zinazohusu maendeleo, kutokana na umuhimu wa taarifa hizo.

Alieleza kua serikali ya awamu ya nane chini ya Raisi Dk. Mwinyi imepiga hatua kubwa za maendeleo katika kuwasogezea huduma bora wananchi wake, ya maeneo mbali mbali ya mjini na vijijini.

"Serikali ya awamu ya nane, imepiga hatua kubwa katika maendeleo nchini kwa kuwasogezea  huduma mbali mbali, hivyo ni vizuri waandishi kutumia taaluma zenu, kuieleza jamii mafanikio hayo, ili iwe na uwelewa wa kutosha," alisema.

Akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika jamii, Mkuu wa wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja alisema, waandishi wa habari wanawajibu wa kutoa taarifa zilizosahihi.



Alieleza kua ili waweze kutekeleza wajibu huo vizuri ni vyema kufuata maadili ya kazi zao pamoja na kuwashirikisha wahusika moja kwa moja,  katika kupata taarifa na takwimu sahihi watakazo zitumia.

"Uandishi ni taaluma muhimu sana kama taalima nyengine na inamiiko na maadili yake, hivyo ni muhimu kwenu, kufuata ipaswavyo kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla," alieleza.

Kwa upande wake Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango Pemba Abdul-wahab Said Abubakkar alisema, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekua akitoa kipaumbele kwa waandishi wa habari, kutokana na uwezo wao  wa kuisaidia serikali kwa kuonyesha mafanikio mbali mbali yaliofikiwa.



Akifunga kongamano hilo Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa pili wa Raisi Pemba Ali Salum Matta, alitoa pongezi kwa Afisi ya Raisi Ikulu Pemba, kwa kuandaa kongamano hilo, ambalo linaweza kuleta tija kwa jamii, kutokana na kujumuisha wadau mbali mbali wa habari.

Washiriki wa kongamano hilo  walisema, ni vyema kwa taasisi zenye jukumu la kutoa taarifa husika, kutoa ushirikiano wa kutosha, katika kufanikisha hilo ikiwemo kutoa takwimu sahihi.


                                                                MWISHO

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...