Skip to main content

KIDUTANI CHUMBAGENI PEMBA WAPITISHA KANUNI ZA KUWALINDA

 


 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANANCHI wa kijiji cha Kidutani shehia ya Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamepitisha kwa pamoja, kanuni zitakazowaongoza wao na watoto wao, katika kufikia malezi na makuzi mema ya vijana wao.

Akizisoma kanuni hizo mbele ya mkutano mkuu wa wanakijiji hao, Katibu wa kamati ya maadili, taaluma na ushari Machano Ali Makame, alisema moja ya kanuni hizo kati ya 19, walikubaliana kuwa, mwisho wa kutembea iwe ni saa 4:00 usiku.

Alisema kanuni hiyo, itawahusu watu wote, na ikitokezea kuna kundi la watu au mtu mmoja ana dharura mfano ugonjwa, wavuvi, wafanyakazi wataieleza kamati hiyo.

‘’Inawezekana ukamkamata mtu saa 5:00 usiku, lakini kama ukitoa maelezo yenye ushahidi mbele ya kamati, unaweza kusameheka, maana lengo sio kukomoana,’’alisema.

Katib huyo alisema kanuni nyingine ambayo wanakikiji hao wamekubaliana ni, kupiga marfuku mikato ya nywele inayopongina na uislamu pamoja na nguo za mbano.

Alifafanua kuwa, kanuni nyingine ambayo wanaamini wakiifuata inaweza kuwa suluhisho la kwa vijana wao, ni kuwarejesha masomo waliokatisha.

‘’Wapo baadhi ya vijana wamekatisha masomo, iwe ni madrassa au skuli, wapo wasiotaka kufanya ibada wote hawa wataitwa na kamati na kufanya mazungumzo nao,’’alisema.

Katib huyo alisema kanuni nyingine walioipitisha ni kuwapa fursa vijana, kuangalia nyenendo za wazazi, na pindi akitokezea mmoja wao, anatabia hatarishi, wafikishe taarifa zake mbele ya kamati.

Mapema Mwenyekiti wa kamati hiyo, Saleh Abdalla Mohamed, alisema kanuni hizo na nyingine, anaona zitakuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Kidutani.

Alieleza kuwa, ijapokuwa zipo kanuni zilizomo ndani ya kitabu kitakatifu pamoja na hadithi za Bwana Mtume Muhammad (S.A.W), lakini walizozipitisha hazipingani na amri hizo.

‘’Kwa mfano tunafuatilia nyenendo za watoto masomoni, uvaaji wa nguo za stara, kupiga marufuku ngoma, ukataji wa nywele na kuacha wizi, yote haya yamepitishwa kama kanuni, ingawa hata uislamu umekataza mwanzo,’’alifafanua.

Msaidizi Katibu wa kamati hiyo Mariyama Mussa Khamis, alisema kamati inatarajia kuanzisha madarasa kadhaa, kwa ajili ya wananchi kujiendeleza.



Nae mwananchi Khamis Khatib Khamis, alishauri kuwa kamati iwe madhubuti, katika kusimamia kanuni hizo, ili kuwa na vijana wenye maadili mema.

Kwa upande wake mwananchi Time Pandu Makame, aliwasisitiza wazazi na walezi wenzake, kuwa karibu na kamati hiyo, ili kufikia malengo husika.

Wananchi wa kijiji cha Kidutani, walifikia uamuzi wa kuwa na kamati hiyo ya maadili, baada ya kuoenekana kujitokeza kwa vitendo viuvu ikiwemo wizi hasa nyakati za usiku pamoja na kundi la watoto kukatisha masomo.

Wakati hayo yakifanyika, wizara ya Maendelezo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa mwaka wa fedha 2025/2026, imepanga kutumia shilingi milioni 5,737,003,000, ili kuendesha programu mbali mbali, ikiwemo ya kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Kitaifa wa Kumaliza Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Jingine lililokusudiwa kufanywa na wizara hiyo ni Mradi wa Mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Wasichana.

                 Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...