Skip to main content

MWENGE WAUKUBALI USHIRIKA WA UPANDAJI MIGOMBA KUKUU KANGANI

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ali Ussi amesema, ameridhishwa kwa asilimia 100, na utekelezwaji wa mradi wa upandaji wa migomba uliotekelezwa na kikundi cha ‘tusitupane Cooparative’ kilichopo shehia ya Kukuu wilaya ya Mkoani Pemba.

Alisema, mradi huo ni miongoni mwa jitihada za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, za kuunga mkono wananchi wake, katika kuhakikisha wanatumia fursa za kiuchumi zinazowazunguka katika maeneo yao.

Aliyasema hayo jana, wakati alipotembelea shamba la migomba la kikundi hicho, shehiani humo, ikiwa ni shamra shamra za mwenge huo, kwa mwaka huu.

Alieleza kua, mradi huo ni utekelezaji wa ahadi alizoziweka Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi baada ya kuingia madarakani, za kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo nchini.



Alifafanua kua, kilimo hicho kinaonyesha dhahiri kwamba, vijana wa kikundi hicho wamefanya jitihada nzuri, katika kutimiza azma na maono ya Dk. Mwinyi.

"Vijana wa kikundi hichi, wamefanya jitihada kubwa katika kutimiza azma ya serikali, kwani wameonesha wazi mafanikio ya jihudi zinazofanywa na serikali, za kuwawezesha wananchi wake katika kutumia fursa za kiuchumi," alisema.

Alieleza kwamba, kikundi hicho kimefanya kazi kubwa ambayo, ni hatua muhimu katika kujikwamua kimaisha na kujiimarisha kiuchumi, kutokana na mchango wa kilimo kuwa mkubwa.

Aidha kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ali Ussi, alitoa wito kwa wananchi kushiriki uchaguzi mkuu, kwa amani na utulivu, huku akiwataka  kuwaunga mkono viongozi waliopo madarakani.

"Kama ilivyo kaulimbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ya "jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu" naombeni Oktoba tuwaunge mkono viongozi wetu waliopo,"alisisitiza.



Awali akisoma risala ya kikundi, Katibu wa kikundi hicho Habibu Ali alisema, kikundi hicho kilianzishwa 2019 na kupata usajili mwaka 2023, kina wanachama 24, wanaume 16 na wanawake wanane, hadi sasa kimepokea mkopo wa shilingi milioni 5, kutoka serikalini na shilingi milioni 10 kutoka kwa taasisi ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (ZEEA).

Alieleza kua, hadi sasa kikundi kimeshapanda migomba 380 ya aina tofauti, ambapo kati ya hiyo 145, imeshaanza kuzaa na kuvuna ndizi 46, ambapo zimeuzwa na kujipatia shilingi 490,000.

Aliongeza kua, shamba lao lenye ekari 1.25, limefanikiwa kutoa ajira kwa vijana, limesaidia kuongeza lishe na uhakika, uhifadhi wa mazingira na matumizi bora ya ardhi kwa kutumia mbolea za samadi.

Katika ukaguzi wa mradi huo, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, alishiriki katika zoezi la upandaji wa migomba shambani hapo.

Wakati huo huo, kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, alitembelea mradi wa lishe bora, ambapo  alifungua klabu ya uhamasishaji wa lishe bora kwa afya imara, iliopo skuli ya msingi Kukuu.

Katika ufunguzi huo alisema, klabu hiyo itasaidia kutoa elimu ya matumizi ya lishe bora kwa jamii, ambapo kauli mbiu yake ni "mtaji ni afya yako zingatia unachokula".

Wilaya ya Mkoani mwenge huo na ujumbe wake, ulitembelea jengo la kuhifadhia mwani Mtuhaliwa, diko na soko la samaki Mbuyuni, uwekaji wa sanduku la maoni bandarini na ujenzi wa dakhalia Kiwani na kufanyika mkesha eneo la Tasini jimbo la Kiwani.

                                                     MWISHO

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...