Wakizungumza kwenye kikao maalum cha
kamati kuu cha jumuiya hiyo, kilichofanyika Chumbageni, walisema wako tayari
kuona mashindani ya mwakani yanafanikiwa.
Walisema, suala la kuwakusanya watoto
katika jambo jema kama hilo, hawaa budi kuliunga mkono, kwani ndio eneo la
kutafuta kheir kutoka kwa Muumba,
Shehia wa Chumbageni Mgeni Othman Shaame,
alisema atazishauri taasis kadhaa na waumini wingine, ili kutoa michango yao ya
hali na mali.
Alisema, kutokana na mashindani ya tano
kufanikiwa, vyema binafsi ameingia tena hamu, kuona ashirikiane na Jumuiya hiyo,
kwa ajili ya mwakani.
‘’Kwa hakika, mashindani ya tano
yalifanikiwa vyema, na kwa kwa mara ya kwanza, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa
wilaya, sasa na haya ya sita yanayokuja tuko pamoja,’’alisema.
Sheha wa Wambaaa Mohamed Suleiman
alisema wazo la Jumuiya hiyo la kuwakusanya vijana, atahakikisha anatafuta
nguvu za zaida, ili kufanikisha.
Alieleza kuwa, njia moja wapo ya
kukitangaaza kitabu cha Muumba, ni kuwahifadhisha vijana, ili wajue wajibu na
haki zao.
‘’Vijana wakimjua Muumba na wao
kujibu wao, inaweza kuwa rahisi sasa kupata watu wenye maadili na kujali
wenzao,’’alisema.
Akifungua mkutano huo mkuu, Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo ustadhi, Hassan Othman Khamis aliwashukuru wote waliofanikisha
mashindani yaliyopita, na kuwaomba kuwaunga mkono kwa msimu ujao.
‘’Kwa hakika nguvu za wat una mashirika
mbali mbali, yalifanikisha mashindani yetu, kwa hili mlipaji ni Muumba
mwenyewe, ingawa tunajiandaa kwa kwa mwakani,’’alisema.
Katib wa Jumuiya hiyo ustadhi Abdalla
Haji Ali, alifaeleza kuwa, kwa mashindani ya mwakani kunauwezekano wa kuongezeka
madrassa, kutoka saba za mwaka jana.
Aidha wajumbe hao wa kamati kuu wa
jumuiya ya tahafidhil quran ya Wambaa, wameridhia uamuzi wa mashika fedha wa
zamani Ali Juma Khamis kujiuzulu na nafasi yake kukabidhiwa Salma Haji Makame
kwa mwaka mmoja ujao.
mwisho
Comments
Post a Comment