Skip to main content

MJANE WA WATOTO SABA AOMBA MSAADA PEMBA

 


NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@

MJANE mwenye watoto saba amewaomba wahisani na watu wenye uwezo, kumpa msaada wa bati na miti, kwa ajili ya kuezekea nyumba yake, ili apate kustirika na watoto wake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake kijiji cha Madenjani Wilaya ya Wete Pemba, leo Juni 12, 2025 mama huyo Rehema Salum,  alisema nyumba anayokaa imeshakua mbovu, mvua yote inamnyeshea ndani mwake.

Alisema anapatashida kwani mvua inaponyesha husimama barazani hata kama ni usiku mkubwa,kwa vile ndani hujaa maji na kukosa sehemu salama.

‘’Ndani hujaa maji, vitanda vyangu vyote vimeshaharibika sina hata pakulala na watoto wangu saba, naomba binadamu wezangu munisaidie nateseka,’’alilalamika.

Alieleza tayari alishajenga vyumba viwili vya matufali, ingawa ameshindwa kuezeka, hivyo ameomba asaidiwe bati pamoja na miti kwa ajili ya kuezekea, ili apate kuishi sehemu anapostahiki  binadamu.

Alifahamisha kuwa mume wake amemuacha na watoto saba, na kumuachia mzigo wa malezi, na kwa sasa hamuulizi huduma ya aina yoyote kwa watoto wao.

Alisema amesharipoti maeneo mbalimbali ikiwemo ustawi wa jamii wilaya ya Wete pamoja wizara ya Maendeleo ya Jamii, ingawa hakuna hatua aliyochukuliwa.

Katika hatua nyingine, alimuomba sheha wa shehia  kumuingiza katika miradi ya maendelo ambayo inakuja, ili iweze kuwasaidia kumoa uhakika wa chakula.

Mtoto wa mjane huyo, Bilali Mohamed Rashid (16)  anaesoma darasa la kumi, anasema ndoto zake za baadae ni kuwa waziri wa Fedha.

Alifahamisha kuwa, kitendo cha kukosa huduma kutoka kwa baba yao kinamuathiri, kwani wanashindwa kupata huduma wanazotakiwa, kutoka kwa wazazi wao, ndio maana anasoma kwa bidii.

‘’Tunakwenda skuli hatuna viatu mvua kama hizi, hatuli chochote, na tukirudi tunakuta hamna kitu, kwakweli hilo linaniathiri na linaweza kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zangu,’’alifafanua.

Nae Nasra Mohamed Rashid ambae anasoma darasa la pili  amesema ipo haja serikali, kuweka adhabu kali kwa wazazi pindi wakizitekeleza familia zao.



Baba mzazi huyo ambae ni mstaafu wa JWTZ, Mohamed Rashid alipopigiwa simu na mwandishi wa habari alisema, sio kwasababu hataki kuwahudumia watoto wake, bali ni kutokana na halingumu ya maisha yake.

‘’Ni kweli mstaafu, ingawa ninachokipata, hakitoshelizi kukigawa nyumba mbili, inafaa kama hawa watoto atanirejeshea nipate kuwahudumia kwa chungu kimoja,’’alisema.

Mwana harakati wa kulinda na kutetea haki za watoto Pemba Tatu Abdalla Msellem alisema kuvunjika kwa ndoa isiwe sababu ya kila mzazi kufumbia macho wajibu wake wa malezi na huduma kwa watoto.

Sheikh Said Ahmed Mohamed  kutoka Ofisi ya Mufti Pemba, anasema kisheria mwanamme ndie mwenye jukumu la kutoa matunzo kwa familia yake, hata baada ya kuvunjika kwa ndoa.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki lililopo Mkungu Malofa Chakechake Robert Miguwa Ndalami, anasema dini imeelekeza wanaume watoe huduma stahiki kwa familia zao akiwemo mama na watoto.

Ripoti ya Wizara ya Kazi, Uezeshaji, Wazee na Watoto, kwa sasa wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ya mwaka 2017/2018, imeeleza kua, kesi 534 za utelekezaji watoto zimeripotiwa Zanzibar.

Ambapo kesi 412 ni kwa upande wa Unguja na 122 kwa Upande wa Pemba, hata hivyo ripoti hiyo haijaweka wazi sababu rasmi za utelekezaji huo.

MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...