Skip to main content

ZHC YAJA NA MPANGO WA NYUMBA KWA WENYE KIPATO CHA CHNI ZANZIBAR

 





NA SALMA LUSANGI, ZANZIBAR@@@@

Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) limesema linampango wa kujenga nyumba za kuwapangisha watu wenye kipato cha chini katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.                                                                                                                                                  

Kauli hiyo imetolewa mwisho wa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Mwanaisha Ali Said wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Shirika hilo Darajani, Unguja.

          Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga ardhi ya akiba kwaajili ya Maendeleo hivyo Shirika litatumia fursa hiyo kujenga nyumba za kupangisha na  kuuza kwa wananchi mbali mbali  kwaajili ya kuleta makaazi bora.    

   Mkurugenzi Mwanaisha  amesema  ZHC kwasasa imeanza  kujenga nyumba za kuuza katika eneo la Mombasa kwa Mchina lakini hata mwananchi mwenyewe kipato cha chini anaweza kununua kutokana na utaratibu mzuri ambao ZHC  imepanga kuziuza nyumba hizo.

       Alieleza kwamba nyumba hizo zitauzwa kwa Wazanzibari waliyopo ndani na nje ya nchi,  muhimu mtu  afuate taratibu za manunuzi zilizoekwa na Shirika hilo.                                                                                                                        
Alifahamisha ZHC itauza nyumba hizo kwa njia tatu, aidha njia kulipa pesa zote kwa pamoja,  au njia ya kulipa pesa kwa awamu nne au kwa njia ya benki (mogeji hauzi)  

    
 Morgage house)  ni njia ambayo mtu anazungumza na benki hivyo sisi Shirika tunapokea pesa kutoka benki na lakini mteja yeye atafunga mkataba na benki kwaajili ya kukatwa pesa za nyumba hiyo" Alisema Mwanaisha.

Aliezea kwamba ZHC iko tayari kupokea pesa za nyumba zinazojengwa  Mombasa kwa Mchina kwani ujenzi umeshaanza tangu Machi 2023 na utamalizika baada ya miezi 15 kuanzia mwezi huyo.                                                                                                                                                         
Amesema nyumba hizo zitauzwa bei tofauti kutokana na idadi ya vyumba kwani kuna nyumba za vyumba viwili zitauzwa tsh. Milioni 136 na nyumba ya vyumba vitatu zitauzwa milioni 153, bei hizo bila vati (VAT).                                                                                                                      
 Aidha mkurugenzi Mwanaisha alizungumzia suali la mazingira ya usafi katika eneo la nyumba hizo, alisema dhamana ya usafi, ZHC itamkabidhi Bodi ya Kondominia ambayo ni taasisi moja wapo ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi  ndio itakayobeba dhamana  ya kuweka Mazingira safi katika maeneo ya nyumba hizo.                                                                                   
Mwisho Mkurugenzi Mwanaisha amemshukuru Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaunga mkono katika gharama za Ujenzi wa nyumba hizo  kwani bila ya kupata msaada kutoka Serikali kuu Shirika lisingeweza.                                                                                                 
 Ujenzi wa Nyumba za Mombasa kwa Mchina utagharimu Tsh. Bilioni 9.8 ambapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa Tsh bilioni 6.8 na Shirika la Nyumba Zanzibar ( ZHC) limetoa Tsh Bilioni 3.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo ni vy

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan