|
|
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MOJA ya madhara ya vifo vya ajali za Boda boda ni
kukatisha uhai wa abiria, madereva au waenda kwa miguu.
Wahanga wanasema,
licha ya magonjwa kama Corona, maleria, kipindu pindu kuwa yanapoteza wapendwa
wao, lakini ajali za Boda boda zinachangia.
Wanaainisha kuwa,
boda boda zimekuwa zikikatisha uhai wa wapenzi wao, wakuu wao wa familia au
wazazi wao, na kuwaacha wakiwa hawana uhakika wa maisha.
Hassan Haji Mohamed
wa Vitongoji wilaya ya Chake chake, anasema, kwa sasa anaishi na mguu mmoja kwa
miaka saba, baada ya kupata ajali ya boda boda.
‘’Nilikuwa nimepakiwa
nakwenda msibani kwa mdogo wangu, lakini kisha dereva alichanganya mwendo, na
kuingia pembezoni mwa gari ya mzigi iliyokuwa imeegeshwa na kupata kilema cha
kudumu,’’anakumbuka.
Mohamed Othman Juma
wa Mkoani mjini, anasema alipoteza vidole viwili vya mkono wa kulia, baada ya
boda boda aliyokuwa amepanda kugongana na gari ya abiria.
‘’Mwendo ulikuwa
mzuri kisa, lakini dereva alitaka kulipita gari la mazigo, lakini sukani
ilimshinda na kulivamia kwa mbavuni na mimi kuumia,’’anasimulia.
Khadija Ussi Haji wa
Wete ambae kwa sasa ni kuzuka na kuachiwa watoto watatu, anasema muume wake
alifariki kwa ajili ya boda boda.
Anasimulia kuwa, kwa
sasa anaishia maisha ya kubahatisha hasa kwa vile hakuna msaada wa familia hata
moja, jambo linalompa wasi wasi wa kila siku.
Khadija Chande Hamad
wa Kojani Wete, anasema kwa sasa anaishi na wajukuu zake watatu wote ni
mayatima wa ajali za boda boda, ambao baba yao alifariki eneo la Mchanga mdogo.
‘’Ilikuwa ni kama saa
7:00 imeelezwa wakifukuzana wao kwa wao kutoka Konde hadi Ole, ingawa kufika
Mchanga mdogo, walivamiana,’’anaeleza.
Kwa sasa bibi huyo na
wajukuu zake, anasema anaishi kwa maisha ya kuomba omba, kutoka kwa ndugu na
jamaa zake, kwani familia ya upande mmoja imesusia kutoa huduma.
POLISI LINATAJA
MADHARA YA AJALI HIZO
Kamishna wa Polisi
Zanzibar ‘CP’ Hamad Khamis Hamad, anasema moja ni kupunguza nguvu kazi ya
taifa, kwani wengi wa madereva wa boda boda ni vijana.
‘’Kuzipa gharama za
mazishi au matibabu familia ambazo, pengine hawakujipangia kwa wakati huo, ni
miongoni mwa madgara ya ajali za boda boda,’’anasema.
Mkuu wa kikosi cha
usalama barabarani ‘TRO’ mkoa wa Mjini magharibi Unguja Khamis Mwakanolo,
anaona madhara ni abiria, dereva au mpatwa na ajali kupata madhara ya mwilini
mwake.
Nae Mkuu wa usalama
barabarani Mkoa wa kusini Pemba ‘RTO’ Shawal Abdalla Ali, anaona madhara ni
kujidhoofisha kiuchumi kwa mmiliki wa boda boda,
‘’Lakini pia
kusababisha vifo, vilema, vizuka na kuongeza kwa mayatima, huwa ni madhara
makubwa yatokanayo na ajali za boda boda,’’anaaninisha Shawal.
MADEREVA WA BODA BODA
Omar Khamis Haji
‘Kiomi’ anasema madhara ni kupoteza uhai wao, jambo ambalo linaweza kuwaweka
wengine kwenye umaskini.
‘’Maana inawezekana
familia tayari inakutegemea, lakini kama ukipata ajali na kisha kuwa kilema ama
kupoteza uhai, tayari umeshawasababishia wengine kuishi kwenye
umaskini,’’anasema.
chanzoa cha ajali hizo ni usimamizi hatarishi
wa askari wa usalama barabarani.
Maulid Himid Haji wa
Ole, anasema madhara anayoyaona ni kuwapotezea imani jamii, juu waenesha boda
boda kuwa wamekuwa chanzo cha ajali za barabarani.
Ussi Haji Said na
mwenzake Bakar Juma Ibrahimu, wanasema pamoja na kupata vilema vya kudumu,
lakini wamekuwa wakiitia hasara serikali kwa matitabu.
‘’Mwaka 2020 mwenztu
eneo la Chake chake alijigonga na ukuta na kuvurugika vibaya, ilibidi
asafirishwe na kutumika gharama zaidi ya shilingi 800,000 na hadi leo ni
mlemavu,’’anasema Ussi.
Mwenyekiti wa Jumuia
ya waendesha boda boda mkoa wa kusini Pemba Kassim Khamis Juma, anaona amdhara
ni vijana kuondoka duniani kila siku.
‘’Ni kweli ajali za
boda boda zimekuwa nyingi mno, jambo linapunguza idadi ya vijana na kuongezeka
wazee, ambao wanaelekea kukosa wasaidizi,’’anasema.
Mmiliki wa Boda Boda
Fatma Haji Said wa Msingi Chake chake, anasema kwake ni kupotezea kwa mali yake
(boda boda), ambayo aliamini ndio kitega uchumi chake.
‘’Tumetakiwa
tujiajiri, sasa kama umenunua chombo baada ya siku nne, kijana anakwambia
ameiongesha na mti, ni kukurejesha nyuma kimaisha,’’anasema.
TAKWIMU ZA AJALI
Uchunguuzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini kuwa, kwa mfano kwa
mwaka 2019 hadi mwaka 2020 kwa Tanzania, kulikuwa na ajali za piki piki 1,133 zilizosababisha vifo 674, sawa na majeruhi 948.
Imebainika kuwa, kati
ya ajali hizo, Tanzania bara kuliripotiwa ajali 964, zilizosababisha vifo 573 na majeruhi 767 kwa miaka hiyo miwili.
Wakati kwa Zanzibar,
kuliripotiwa ajali 169 sawa na vifo 101 huku idadi ya majeruhi wakiwa ni 181.
Katika kipindi cha
Januari hadi Disemba pekee kwa mwaka 2020 kwa Tanzania, kulikuwa na matukio 505 ya ajali za pikipiki,
ikilinganishwa na matukio 628 katika
kipindi kama hicho mwaka 2019.
Kwa upande wa
Zanzibar, mikoa iliyoongoza kwa ajali za piki piki katika mwaka 2020, ni mkoa
wa Mjini magharibi ulioripoti ajali 1,774, ukihusisha vifo 25.
Ingawa kati ya hao,
wanaume waliongoza kwa kuwa 24, huku wanawake akiripotiwa mmoja aliyefariki,
kutokana na ajali za piki piki.
Mkoa mwengine ni wa
Kusini Unguja kwa ajali 469, sawa na vifo watu 10, huku wanaume wakiwa wanane
(8), na wanawake wawili.
Mkoa wa kusini Pemba,
uliripoti matukio 604, yakihusisha vifo 10, wakiwemo wanawake wawili (2) na
wanaume wanane (8).
Uchunguzi ukabaini
kuwa, kwa mwaka huo wa 2020, mkoa wa Kaskazini Unguja ulikuwa na ajali 311,
ambazo zilihusisha vifo vya wanaume wanane (8) na mwanamke mmoja, ambapo mkoa
wa Kaskazini Pemba, ulikuwa na ajali 858, sawa na vifo vya watu watano (5) wote
wakiwa wanaume.
ATHARI ZA AJALI ZA PIKI PIKI
Kassim Haji Ali
abiria ambae kwa sasa ana mkono mmoja, anasema kwanza ni kupata ulemavu wa
kudumu ambao haukutarajiwa.
Mayasa Hassan Hemed
ambae mume wake alipoteza maisha mwaka 2022 kwa ajili ya pili pili, anasema ni
vifo na kuwaacha watoto wakiwa na mlezi mmoja.
Baba ambae mtoto wake
alifariki kwa ajili, anasema ni kukosa nguvu kazi ya familia, kwani kila
familia inawategemea wengine kwenya kazi.
Mkuu wa kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Mjini magharibi Unguja ‘RTO’ Khamis Mwakanolo,
athari ni kuongeza umaskini ndani ya familia, kwa matibabu makubwa.
Mmiliki wa piki piki
(boda boda) Michakaini Chake chake Pemba Kombo Haji Kombo, anasema kwanza ni
kuwarejesha nyuma wao walioekeza kwenye vyombo hivyo.
Doktari Khamis Haji
Khamis anasema, ni matumizi ya dawa yasiyotarajiwa, kwa waendesha piki piki,
ambao kwa mwezi hujitokeza katia ya watatu hadi watano.
NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA AJALI?
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati akikabidhi
piki piki za mkopo mkoa wa kusini Pemba, aliwataka madereva kukomaa katika utii
wa sheria za barabarani.
‘’Sitofurahishwa
kusikia siku moja muendesha boda boda amekuwa chanzo cha ajali barabarani,
kwani tunawakabidhi vyombo hivi vikakuze uchumi na sio kuongeza ajali,
majeruhi, vilema na vifo,’’aliwakumbusha.
Kamisha wa Polisi
Zanzibar ‘CP’ Hamad Khamis Hamad, anasema kwanza ni elimu kwa waendesha piki
piki, juu ya matumizi sahihi ya barabara.
Mwenyekiti wa Jumuiya
ya boda boda mkoa wa kusini Pemba, Kassim Khamis Juma, anasema kuimarishwa kwa
miundo mbinu ya barabara, hasa kutokana na ongezeko la vyombo vya moto.
Dereva wa piki piki
Othman Issa Yakoub anasema utaratibu wa kukagua piki piki kila wakati uondoke,
na badala yake kuwe na mifupo ya kisasa.
Mwananchi Zuhra Juma
Mmanga wa Ngwachani Mkoani anasema, ni uwepo wa adhabu kali kwa dereva wa piki
piki, atakaetiwa hatiani kwa kosa hilo.
Afisa Sheria kutoka
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Bakar Omar Ali, anasema kamera
zilizopo mjini zitumike kuwatia hatiani wanaokiuka sheria.
MITANDAO YA KIJAMII IMERIPOTI NINI?
Ajali za barabarani zinatajwa
kuwa ndio zinasababisha vifo vingi vya watu duniani kulimo magonjwa yoyote,
Shirika la Afya Duniani WHO linasema.
WHO kwenye ripoti yake ya mwaka 2018, limeanisha licha ya
bara la Afrika kuwa na idadi ndogo ya vyombo vya usafiri, lakini ndilo lenye
ajali nyingi za barabarani duniani, kuliko mataifa ya Ulaya.
Katika ripoti hiyo ‘WHO’ linasema kuwa kuna vifo 27 kwa
kila watu 1000, huku likifafanua kuwa, kuna vifo vya barabarani katika nchi za
Afrika ni mara tatu zaidi ya ajali zinazotokea Ulaya.
Ripoti ikafafanua kuwa, karibu nusu ya mataifa 54 ya
Afrika hayana sheria za mwendo kasi katika nchi zao, huku nchi kama Botswana,
Ivory Coast na Cameroon, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeona kiwango cha vifo
vikiongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni , zinasema kuwa
watu milioni 1.35 waliuwawa katika ajali za barabarani duniani kwa mwaka 2016,
kiwango ambacho kiko tofauti kidogo na mwaka uliopita.
Upande mwengine katika ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia, imeelezwa kuwa hadi
kufikia mwaka 2020, idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani
katika nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, itaongezeka kwa asilimia 80.
Mwisho
Comments
Post a Comment