NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANAWAKE wa shehia wa Makombeni
wilaya ya Mkoani Pemba, wameomba kuongezewa ufahamu juu ya dhana ya uchumi wa
buluu, ili waifahamu kwa kina malengo ya serikali kuu.
Walisema,
wamekuwa wakisikia juu juu ya dhana hiyo, ingawa bado wamekuwa hawana uwelewa
wa ndani, na kusababisha kubakia na uwelewa wa wao zamani.
Wakizungumza
na waandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar ofisi ya
Pemba waliofika kusikiliza changamoto zao, walisema bado dhana hiyo haiku vyema
kwenye akili yao.
Walisema
kua, wanahitaji mamla husika kufika Makombeni kuwaeleza kwa kina juu ya dhana
ya uchumi wa buluu, ili waende samba mba na kaluli ya rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Mmoja kati
ya wanawake hao Mayasa Makame Chumu, alisema bado baadhi yao wamekuwa
wakisikiliza vyombo vya habari, ingawa dhana hiyo bado hawajaipata vyema.
‘’Dhana ya
uchumi wa buluu tunaiskia kwenye vyombo ya habari, lakini hasa kuipata kwa
upana bado, baada hatujawahi kuwapa wataalamu kutueleza,’’alieleza.
Nae Mwajuma
Khamis Juma, alieleza kuwa ni wakati sasa kwa wataalamu kutoa Idara ya Uchumi
wa buluu kufika Makombeni ili kukutana nao ana kwa ana.
Naeo Faida
Faki Kombo, Zuhura Haji Kheir na Semeni Juma Kheir, wamesema vipindi vya kwenye
redio na tv wanavisikia, ingawa hawapati kuuliza maswali.
Walieleza
kuwa, wamekuwa wakisikiliza vipindi vya kwenye redio, lakini changamoto
wanayokumbana nayo ni kukosa kuuliza juu dhana ya uchumi wa buluu.
‘’Vipindi
vya redio ni kweli vinatoka kwenye redio, lakini hatupati kuuliza sasa tunaomba
wataalamu husika wafikie shehiani kwetu,’’wamependekeza.
Sheha wa
shehia wa Makombeni Mwashum Haji Makame, alikiri kuwa ipo haja kwa wataalamu
kutoka Idara ya Uchumi wa buluu kufika shehiani mwake.
Alieleza kuwa
wananchi wamekuwa na hamu kubwa ya kukutana na wataalamu ili kuelezea namna
ambavyo dhana hiyo inaweza kuwakomboa.
‘’Wananchi
wa shehia yangu wengi wanaitegemea bahari kwa shughuli zao mbali mbali za
maendeleo, ikiwemo suala la uchumi wa buluu, lakini bado hawana uwelewa
mpana,’’alieleza.
Hata hivyo
sheha huyo amewataka wananchi wake, kuendelea kufuatilia kwa karibu vyombo vya
habari, ambapo wanaweza kupata uwelewa japo mdogo, ili kujua vipi habari
inaweza kuwasaidia.
Kaimu Afisa
Mdhamini wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Pemba, Abdull-malik Mohamed Bakar,
alisema tayari shehi zote za Pemba, wameshazifikia kutoa ufafanuzi wa dhana ya
uchumui wa buluu.
Alieleza
kuwa, inawezekana wapo wananchi ambao hawakubahatika kuhudhuria kwenye mikutano
wakati maafisa wa Idara ya Uchumi wa buluu walipopita kwenye shehia zao.
‘’Kama
wananchi hao wa shehia ya Makombeni wanahitaji tena elimu, tutawasiliana na
uongozi wa shehia, ili kutupangia mkutano mwengine,’’alieleza.
Hata hivyo
aliwasisitiza wananchi hao, kuendelea kufuatilia vyombo vya habari, kwani
kumekuwa na vipindi kadhaa vinavyoendeshwa juu ya dhana ya uchumi wa buluu.
Rais wa
Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi tayari ameshakabidhi vifaa vya uvuvi, ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa dhana hiyo kwa vitendo.
Mwisho
Comments
Post a Comment