Skip to main content

TAMWA ZANZIBAR YATAKA UWEPO MAZINGIRA YA USAWA WA KUJINSIA ZEC

 



MUHAMMED KHAMIS, TAMWA- ZNZ::

CHAMA cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar kimesema  wakati umefika kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar 'ZEC' kuhakikisha kinaweka mazingira ya usawa wa kijinsia, katika utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali, zikiwemo za usimamizi wa chaguzi na nyenginezo.

 

Kauli hiyo  imekuja  kufuatia mkutano malumu wa majadiliano, baada ya  kumalizika kwa mkutano  awali uliofanyika Septemba mwaka jana na kupeana na majukumu kwa pande zote mbili kupitia, sera jinsia ya mjumuisho kwa ajili ya kutazama uwepo wa mazingira ya  usawa wa kijinsia katika muundo wa tume hiyo na utendaji wa kazi zake.

 

Akizunguma katika mkutano huo Mkurugenzi wa Chama hicho Dk.Mzuri alisema ushiriki wa wanawake katika shuhuli za tume hiyo utaleta mwanga zaidi na hatikame kuwafanya wanawake wengi waweze kufikia malengo yao yakiwemo ya kuwa viongozi.

 

Alisema kwa miaka mingi katika kazi za tume hiyo kumeonekana  wanaume wengi ndio wanaoshiriki shughuli za tume zikiwemo za usimamizi wa chaguzi zinazofanyika huku idadi kubwa ya ushiriki ikionekana kuwa ya wanaume na wanawake kuwa nyuma licha ya kuwa ndio wenye idadi kubwa katika kila chaguzi zinazofanyika.

 

Alisema iwapo wanawake wengi watashiriki katika utendaji wa tume hiyo utapelekea wanawake wengi zaidi kushiriki katika harakati za kuchagua na kuchaguliwa na hatimae idadi kubwa ya wanawake kutumiza ndoto zao za kuw aviongozi itafakiwa.




‘’Hata kama ikitokea idadi kubwa ya wanawake hawakuomba nafasi kwenye tume lakini muna wajibu wa kukweka kanuni ambazo zitalazimisha asasi za kiraia kupeleka idadi kubwa ya wanawake katika shughuli za tume zikiwemo zile za usimamizi wa chaguzi zinazofanyika kila baada ya miaka mitano’’aliongezea Dkt,Mzuri.

 

Kwa upande wake  mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema wakati mabadiliko hayo ya kuleta usawa wa kijinsia  yanaendelea kufanyika kunahitajika kujengwa mazingira lazimisha katika sheria ya msajili wa vyama vya siasa ambayo itaonesha uwepo wa idadi sawa ya ushiriki wa wanawake katika kugombe anafasi za uongozi.

 

 

Alisema kuwepo kwa sheria hiyo kutapalekea mazingira rafiki kwa wanawake wengi na kuondoa ukandamizwaji ambao kwa miaka mingi wanawake wamekua wakilalamika, na wanadai kuwa hufanywa na watu wenye nafasi za maamuzi kwenye vyama vyao kupitia idadi kubwa ya wagiombea kuwa wanaume na wananwake huwa wachache.

 

 

Awali Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar Khamis Kona Khamis alisema mkutano huo wa majadiliano umekuja wakati muafaka ambapo tume hiyo ipo kwenye mchakato wa kulifganyika kazi suala hilo.

 

Smbamba na hayo alisema licha ya uwepo wa changamoto za hapa na pale lakini kwa kiasi kikubwa tume hiyo inaendelea kufanyika kazi maswala ya kijinsia na ndio maana baadhi ya wilaya zikiwemo kaskazini Unguja maafisa wote wa tume hiyo ni wanawake.

 


Pamoja na hayo alisema bado TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na asasi nyengine za kiraia wana wajibu wa kupeleka mapendekezo yao pale wanapoona kuna changangamoto za mifumo na iwapo watafanya hivyo watasaidia sana utendaji kazi wa tume hiyo na kupeleka mbele maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

                           MWISHO 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch