NA HAJI NASSOR. UNGUJA
WAANDISHI wa habari Zanzibar, wamesisitizwa kuendelea kuzielimisha mamlaka za nchi, juu ya umuhimu wa kuwa na sheria rafiki za habari kwa maendeleo ya taifa.
Ushauri huo umetolewa na mataalum wa sheria Tanzania Chris Maina Peter, wakati akiwasilisha sheria zinazosimamia habari Zanzibar, kwenye mkutano wa siku moja, ulioandaliwa na Tasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA- Tanzania na kufanyika hotel ya Golden Tulip uwanja wa ndege Unguja juzi August, 22, mwaka 2022.
Alisema moja ya jukumu la vyombo vya habari, ni kutumia kalamu zao vyema kwa kuielimisha jamii na mamlaka husika kuelekea mabadiliko ya sheria.
Alieleza kuwa inawezekana mamlaka za nchi hazielewi ubaya na athari zilizopo katika tansia ya habari, hivyo wakiwaeleza wanaweza kuona.
"Jengine umoja na mshikamano wa hali ya juu ikiwa mbona mnasheria inakwaza kazi zenu ili mziambie mamlaka juu ya marekebisho hayo,"alieleza.
Katika hatua nyingine Professa Chris, alisema nchi inapokuwa na sheria kandamizi hasa inayolenga kuimarishia uhuru wa kujieleza na wa kupata habari maendeleo huwa ya kusua sua.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe Salim Said Salim, alisema sheria zilizopo sasa za habari Zanzibar, sio rafiki kwa ulimwengu huu wa ukweli na uwazi.
Akitokezea mfano alisema ,sheria ya Magazeti nambri 5 ya mwaka 1988 imempa madaraka makubwa waziri wa habari, ikiwemo kufungia gazeti kwa maoni yake.
Nae mwandishi Salma Said alieleza kuwa msawaada wa sheria mpya ya habari, ambayo imeshafika kwa makatibu wakuu kama itarudi kama walivyopendekeza, Zanzibar itakuwa na sheria bora.
Msaidizi Mhariri wa zbc redio Pemba Khadija Kombo Khamis, alisema lazima kwa kamati iliyopewa jukumu la kuwa na sheria mpya ya habari, waharakishe kufuatilia..
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar Ali Haji Mwadini, amesema hana shaka na msawada wa sheria uliopo ngazi ya majaribio wakuu kuwa itarudi kama ilivyo.
Hata hivyo Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi Jabir idrissa, alisema hofu yake ni kutorudi tena kwa msaada huo na kuendelea kutumika kwa sheria kongwe.
Mapema Afisa habari wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA Tanzania Jackline Daniel, amesema mkutano huo ni muendelezo wa kukutano na wadau kujadili changamoto za sheria kandamizi za habari.
Mwisho
ReplyForward |
Comments
Post a Comment