NA KHAULAT
SULEIMAN, PEMBA
ZOEZI la
uchukuwaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na viti maalum
linaendelea kupamba moto, kwa wanawake,wakiwemo wanahabari kupishana ofisi za CCM wilaya za kisiwani
Pemba.
Zanzibar leo kisiwani Pemba,
ambalo limepiga kambi katika ofisi hizo, limeshuhudia wandishi wabahari
wanawake, wajasirimali, watendaji wa serikali
na waachama wingine, wakitekeleza haki yao ya kidemokrasia.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja
kati ya watia nia hao kwa nafasi ya ubunge Jimbo la Chake chake, Ashura
Abdalla Simai 'mabodo', alisema moja ya sababu iliyomsukuma ni kutekeleza haki yake ya kikatiba
ya kisiasa.
Alieleza kuwa, pindi vikao
vya chama vikiridhia jina lake na kurudi, atakwenda bungeni kuwatetea wanawake wenzake
na wingine, kwani walio wingi hawajafanya hivyo.
“Wanawake wamekuwa wakikosa
matetezi kwa kina, wa mambo yanayotuhusu, hivyo nimechukuwa fomu hii kujaribu
bahati yangu kwa mara ya tano,”alisema.
Afisa habari wa ofisi ya Mkuu
wa wilaya ya Wete, Mwamize Mohamed Omar, aliyeweka nia ya kuomba nafasi ya
ubunge jimbo la Mtambwe, alisema nia yake ni kuimarisha huduma za kijamii.
‘’Wanawake wanaelekea kupata
mtetezi, pindi vikao vya juu vya chama vikiridhia kulirejesha jina langu, na kushinda
uchaguzi mkuu wa vyama vingi,’’alifafanua.
Mapema mtia nia kwa nafasi ya Uwakilishi jimbo
la Mtambile, mwanahabari nguli na mahiri Mchanga Haroub Shehe, alieleza kuwa amejipanga
kushirikiana na wananachi, katika kulifanikisha azma yake ya kuwatetea.
Alieleza kuwa, kwa uzoefu
wake wa uongozi kuanzia kwenye asasi za kiraia na hata kwenye utumishi wa umma, hana wasi
wasi pindi jina lake likirudi kutoka vikao vya juu vya chama.
‘’Mimi sihofii idadi kubwa
ya wanaume wanaomba kuteuliwa, ninachoangalia mimi ni mwanachama wa CCM na
kukamilisha sifa zote,’’alifafanua.
Awena Khamis Rashid ambaye
ni mtia nia, kwa nafasi viti maalum kwa wanawake wenye ulemavu, alisema kundi hilo
linamuhitaji, kwa ajili ya kulikomboa kimaendeleo.
“Wanawake wenye ulemavu, tuna
haki ya kugombea na kutetea haki zetu mbali mbali, ambazo kwa sasa,
hatujazifikia ipasavyo, ndio maana mtetezi nimefika,”alieleza.
Maryam Omar Said aliyekua Mbunge
wa jimbo la Pandani kwa tiketi ya CUF, na kuhamia CCM, amebainisha azma yake ya
kuchukua fomu kwa nafasi, kama aliyokuwa nayo awali.
‘’Mimi narudi nyumbani,
baada ya kuona Ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025, imevuuka lengo la
utekelezaji wake, ndio maana nimeshaweka nia ya kuomba fomu ya
ubunge Jimbo la Pandani,’’alifafanua.
Naye mgombea ubunge viti
maalum vijana Zadida Abdalla Rashid, alieleza kundi la vijana wanahitaji
mtetezi kama yeye, ndio maana ameamua kujitosa.
‘’Nguvu ninazo, uwezo upo,
haki ninayo lazima nijitokeze kuomba kuteuliwa kwenye nafasi hiyo, ili niingie
kwenye historia ya utekelezaji wa Ilani ya waka 2025 hadi 2030,’’alifafanua.
Zoezi la uchukuaji wa fomu
kwa nafasi za ubunge, uwakilishi, viti kwa maalum vya vijana uwakilishi na
ubunge, limeanza Junia 28 na likitarajiwa kumalizika Julai 2, mwaka huu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment