Skip to main content

UZINDUZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2026, NI ZAMU YA MKOA WA KUSINI PEMBA

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHIMBO la mwenge wa Uhuru, ni nia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuweka mwenge juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro. Lengo ni kuleta matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale penye chuki na heshima pale palipojaa dharau. Ambapo nia hiyo, aliitoa kwa mara ya kwanza mwaka 1959 huko New York, alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa. Kwa wakatu huo, alimteua Luteni Alexander Gwebe Nyirenda kutekeleza azma hiyo iliyoitwa “Operesheni Mwangaza”, ambapo yeye na wenzake, walianza maandalizi mwezi Novemba 1961. Kabla ya Tanganyika kupata uhuru, ambapo hatimaye usiku wa mkesha wa sherehe za uhuru tarehe 9 Desemba 1961, Luteni Nyirenda na wenzake, waliwasha na kusimika mwenge wa uhuru na Bendera ya Tanganyika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro. Hiyo ilikuwa kama ishara ya kuwa huru, kwa kupandisha mwenge kileleni ilikuwa kwanza, ni kuonesha kazi ngumu iliyoko mbele ya kulijenga taifa changa la Tanganyika. Pili, ilikuwa ni kuuwasha mwenge uangaze nje ya mipaka, kutoa matumaini pasipo na matumaini, upendo palipo na chuki na heshima palipo na uonevu na dharau. Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Philipi Mpango, kwenye hutuba yake aliyoitoa Aprili 2, mwaka 2025 mkoani Pwani, kwenye uzinduzi wa mwenge huo, alisema wazo la kukimbiza mwenge wa uhuru nchi nzima na kila mwaka. Akisema lilitolewa na vijana wa TANU katika kikao chao kilichofanyika Juni 26 mwaka, 1964, ambapo lengo kuu likiwa ni kutekeleza kwa vitendo, azma ya Baba wa taifa ya kuhamasisha umoja, upendo, amani na ujenzi wa taifa. Akaeleza kuwa, tangu wakati huo, mwenge huo umekuwa ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kupitia mbio hizo hamasa kubwa hutolewa. Akasisitiza kuwa, lengo ni kuendelea kudumisha amani, na kujenga uzalendo, umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania waote. Ndio maana anasema, katika kipindi chote hicho, mbio za mwenge wa uhuru, zimekuwa na mafanikio makubwa yanayosadifu maono ya waasisi wa taifa la Tanzania. ‘Mwenge wa uhuru 2025 unaowashwa leo (mwaka jana) utakimbizwa kwa muda wa siku 195, katika mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kufikishwa kwa ujumbe wake,’’alisisitiza. Makamu huyo wa Rais, mwaka jana aliiagiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano wa hali ya juu, kwa wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa, ili waweze kutekeleza jukumu la kizalendo, walilokabidhiwa la kuhakikisha kuwa wanawafikia wananchi. MGENI RASMI MWAKA 2026 NI Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ndie anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi, kwenye uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu 2026. Ambapo hafla ya uzinduzi huo, utafanyika Aprili 2 mwka huu, katika Uwanja wa michezo Gombani wilaya ya Chake Chake, mkoa wa kusini Pemba. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa mkoa huo, Rashid Hadid Rashid, wakati akizungumza na waandishi wa habari, juu ya uzinduzi huo, aliwakumbuhsa jambo wananchi.
Aakasema kuwa, katika uzinduzi huo Dk. Mwinyi atawahutubia wananchi, pamoja na kuzindua rasmi mbio za mwenge wa uhuru na kuendelezwa kwa ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo, katika wilaya nne kisiwani Pemba na Tanzania kwa ujumla. Maana alisema, mwenge wa uhuru hukimbizwa nchi nzima, ikiwa ni sehemu ya kuenzi uhuru wa taifa, kuenzi maendeleo ya nchi, sambamba na kudumisha amani, mshikamano na maelewano. "Mwenge wa uhuru mwaka huu 2026, unatarajiwa kuzinduliwa Pemba kitaifa Aprili 2, mwaka 2026 katika uwanja wa michezo Gombani, wilaya ya Chake chake, hivyo tunawaomba wananchi kuujza uwanja,’’anasisitiza. Anaeleza kuwa, matayarisho ya uzinduzi wa mbio za mwenge huo, yamekamilika na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imejipanga kikamilifu kuhakikisha tukio hilo la kihistoria, linakamilika kwa mafanikio. Mkuu wa mkoa huyo anafafanua kuwa, vikundi vya hamasa na halaiki, wasanii vimejipanga ipasavyo na kuhakikisha viongozi na wananchi kwa ujumla, wanapa burudani. Alieleza, tukio la uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru, linatarajiwa kudhuriwa na viongozi mbali mbali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania bara. ‘’Hapa nichukuwe nafasi hii, kuwataarifu wanachi wa mkoa wa kusini Pemba, kwamba wanaugeni mzito, hivyo aliwaomba kushiriki kikamilifu, katika tukio hilo la kihistoria,’’anasiistiza. Mkuu huyo aliwataka wananchi kuendeleza umoja na mshikamano ulipo Zanzibar, ili kudumisha taswira nzuri iliopo katika Mkoa wa Kusini Pemba. Aliwahakikishia wananchi usalama wa kutosha katika uzinduzi huo, huku akieleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga, katika kuhakikisha hali hiyo inadumu katika mkoa huo. "Niwahakikishie wananchi usalama upo katika mkoa wa kusini Pemba na vikosi vya ulinzi na usalama, vimejipanga ipasavyo, kuhakikisha hali hiyo inadumu muda wote", alisisitiza. Aidha, aliwataka wananchi kutoka maeneo yote ya Tanzania kufika katika mkoa wa kusini Pemba, kujumuika kwa pamoja ili kufanikisha kwa kiasi kikubwa, uzinduzi huo.
Alifahamisha kuwa, baada ya kukamilika uzinduzi huo, mwenge wa uhuru, utaanza mbio zake katika wilaya ya Chake chake na Mkoani, pamoja na kuendelea kukimbizwa katika wilaya nyingine. Hivyo aliwataka wananchi kuendelea kudumisha amani na mshikamano uliopo nchini hususan katika kipindi hicho cha uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru, ili kuhakikisha tukio hilo linamalizika kwa salama na amani. Hata hivyo aliwasihi wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia fursa hiyo kutangaza bidhaa zao, pamoja na kudumisha usafi, katika maeneo yao ili kudumisha haiba ya maeneo yao. ‘’Tuna vivutio vingi vya utalii kwenye mkoani mwetu na Pemba yote kwa ujumla, hivyo tunawaomba wageni watakaofika kisiwani hapa, pia wakajionee historia zetu ambazo ni za kusisimua,’’alifafanua. WANANCHI WANASEMAJE Idda Haji Mohamed wa Chake chake, anasema ni fahari kubwa, kwa serikali kuamua kfanya uzinduzi huo ndani ya mkoa wa kusini Pemba. Haji Mohamed Said, dereva wa tax, amesema ni faraja ya kuongeza pato lake, kupitia biashara hiyo, ambayo huneema wanapopata wageni. Fatma Omar Haji, mmiliki wa mgahawa Machomane Chake chake, anasema jambo hilo litasaidia kuendesha shughuli zake. Mkuu wa wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki, amesme mpango wa serikali wa kuweka mkoa wa kusini Pemba, eneo la uzinduzi ni kuongeza historia nyingine. ‘Amani, Umoja na Mshikamano wa Kitaifa,’’ndio kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2026. MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...