Skip to main content

WALIOKEZA SHILINGI MILION 1.6 KWA UFUGAJI MATANGO BAHARI KUVUNA 20 MILIONI

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANAKIKUNDI cha ufugaji wa majongoo bahari, ‘tumuombe mola’ cha Makangaale wilaya ya Micheweni Pemba, wanatarajia kujipatia shilingi milioni 20 mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa watafanikiwa kuuza bidhaa hiyo, baada ya kuekeza vifaranga vyenye thamani ya shilingi million 1.6 mwaka jana.

Fedha hizo, ni uwekezaji wa vifaranga 3,300 vya majongoo habari, walivyovinunua kwa shilingi 1,650,000 wastani wa shilingi 500 kila kifaranga kimoja, chenye urefu kati ya nchi nne hadi tano.

Wanakikundi hao cha tumuombe mola wamesema kati ya vifaranga hivyo, wanatarajia kuvuna majongoo yaliokwisha pevuka 2,500 na kisha kila moja kuliuza kwa bei ya shilingi 8,000 na kujipatia shilingi milioni 20.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Hator Hassan, alisema haiwezekani kuotesha vifaranga vya idadi 3,300 kisha kuvuna kama ilivyo.

‘’Zipo changamoto kama za kufa na hasa wakati wa usafirishaji wa vifaranga kutoka eneo moja kwenda kwenye bwawa lao, wizi na wingine kufa kabla ya kufikia kupevuka,’’alifafanua.

Alifafanua kuwa mara ya kwanza, wakati wanaanza kazi hiyo, walitumia shilingi milioni 1,000,000 kwa ununuzi wa vifaranga 1,000 ingawa hatimae, walivuna majongoo 340 na kujipatia shilingi milioni 1.7.

Aliongeza kuwa, ingawa hawakula hasara, kama inavyoonekana, lakini hawakuvuuka lengo lao la kujipatia fedha zaidi shilingi milioni 5.

‘’Kama sio changamoto ya vifaranga kufa au kuibiwa wakiwa ndani ya bwawa letu, hata ule mwaka 2021 wakati tunaanza, tungejipatia faida ya shilingi milioni 4,’’alifafanua.

Aidha Mwenyekti huyo, aliongeza kuwa, hata mwaka 2023, walitarajia kujipatia faida ya shilingi milioni 9, ingawa hatimae, walipata shilingi milioni 1.5.





Aliongeza kuwa, tayari wameshafuga mara mbili, tokea waanze kazi hiyo mwaka 2021, na kutumia gharama ya shilingi milioni 3.1 kwa ununuzi wa vifaranga 4,000.

Hata hivyo, alisema kwa sasa wanasubiria hadi mwishoni mwa mwaka huu, na ikiwa vifaranga walivyovitia ndani ya bwawa hilo, havitapitia changamoto ya wizi na kufa, hawana wasiwasi wa kuvuna shilingi milioni 20.

Mmoja wa wanachama hao Hamad Omar Hamad, alisema wamekua wakibadilisha maisha yao, kupitia kazi hiyo, ikiwemo kujihakikisha fedha za matumizi.

‘’Ni kweli kabla ya kuanza kazi hii ya ufugaji wa majongoo bahari, sikuwa na uhakika wa wapi naweza kujipatia fedha za haraka, ingawa kwa sasa nnapo,’’alisema.

Hata hivyo, waliwaomba wafadhili kadhaa, kuzitatua changamoto zao, ikiwemo kuwapatia boti dogo kwa ajili ya doria, viatu vya kuvulia, ili kuepusha hasara za miguuni.


Afisa Ustawi wa mkoa wa kaskazini Pemba Nassra Massoud Sanani, alikiri kukifahamu kikundi hicho, na kusema amekuwa akiwaunganisha na wadau mbali mbali wakiwemo FAWE-Zanzibar.

Alisema, FAWE wamekuwa wakifanyakazi na taasisi kadhaa za kimataifa kama vile UN-Women na wameshaanza kuwapatia mafunzo kadhaa.

Afisa miradi FAWE -ofisi ya Pemba Hija Hamad Issa, alisema hivi karibuni, walikuwa na mafunzo ya siku nne ya mnyororo wa biashara, ambapo mwakilishi wa kikundi hicho, alikuwa miongoni mwao.

‘’FAWE unao mradi wa pamoja, ambao unawaangalia wajasiriamali wanaojishughulisha na kilimo cha mwani, majongoo bahari, migomba, ndizi na mihogo ili kuwa wabunifu,’’alifafafanua.

Alisema, wamekuwa wakifanyakazi kwa karibu na UN-Women katika mradi huo, ambao wapo wajasiriamali 20 wa wilaya za Wete na Micheweni wameshanufaika.





Mapema Mwakilishi wa shirika la kimataifa la UN-Women Tanzania Emile Kivugo Mwakafundu, alifafanua mradi huo, unawalenga wajasiriamali wa mazao ya baharini na nchi kavu.

Alisema, mradi huo wa miaka mitatu, utamalizika mwakani, ambao lengo ni kuona wajasiriamali hao, wanaziongezea thamani bidhaa zao.



Alieleza kuwa, kupitia wadau wao wa FAWE- Zanzibar wanawafundisha namna ya kutoziuza bidhaa zao, kama walivyozivuna na badala yake, waweza kuzisarifu ili wauze kwa mfumo wa bidhaa.

Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, katika kuimarisha ufugaji wa majongoo bahari na upatikanaji wa vifaranga, Idara kwa kushirikiana na Kampuni ya Zanzibar Marine Hatchery imezalisha vifaranga milioni 1.5.

Ambapo kati ya hivyo vifaranga 80,000 vimegawiwa kwa wafugaji wa Unguja na Pemba na vyingine 70,000 kwa ajili ya biashara na uzalishaji.

                       Mwisho

 

Comments

  1. Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.

    Niliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com

    WhatsApp: +2349046229159

    Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
    Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.

    Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.

    Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.

    Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.

    Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.

    Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi

    ReplyDelete

Post a Comment