Skip to main content

KUCHELEWA KUHAMIA KWA WAJASIRIAMALI KITUO CHA MICHAKAINI, MANISPAA CHAKE CHAKE ILIKOSA 'BUNDA' LA MAPATO

 


 NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@

MWENYEWE Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwenye hutuba yake ya ufunguzi wa Kituo cha wajasiriamali Chake chake, alielezea kufarajika.

Mbele ya umati wa wajasiriamali na wananchi wa mkoa wa kusini Pemba, ameelezea kuwa, sasa atapa usingizi baada ya kumalizika kwa kituo hicho.



‘’Leo nimefarajika kuona sasa kituo hichi kipya na cha kisasa, nakifungua rasmi, sasa wajasiriamali wa mji wa Chake chake, waliokuwa wakihangaika huku na kule wamepata utulivu,’’akasisitiza.

Eneo jingine Dk.  Mwinyi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho, mwezi Oktoba 2023, akatoa rai kama sio maagizo kwa Baraza la Manispaa Chake chake.

Moja, akaanza kusisitiza kwa watendaji, kuhakikisha usafi unafanyika kwa udhati, ili wananchi watakaofika hapo, wasishuhudie uchafu kuzagaa.

Jingine akaelekeza, watendaji wa Manispaa na Halmashauri, kuhakikishe, hakuna hata mjasiriamali mmoja, anaepanga bidhaa zake nje ya soko hilo.

‘’Haiwezekani hata kidogo, kuwa wapo wingine wameweka bidhaa zo nje, hapo ni dhahiri wale waliomo ndani watakosa wateja,’’alifafanua.

Kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho, Dk. Mwinyi ambae sio muumini wa kodi kubwa, akasema ni lazima miezi mitatu ya mwanzo, wajasiriamali wasilipe kodi.

‘’Ingawa niwaombe wenzetu wa Baraza la Manispaa Chake chake, kuwatoza fedha ndogo kwa ajili ya usafi, kwani ndio kwanza wanaanza sasa biashara,’’anasema.

Kwa kule kuona kwake mbali, alisema kwa wakati huo, ilikuwa ni kuwavutia wajasiriamali hao, kuhama katikati ya mji na kuingia ndani ya kituo hicho.

Akitaja kuwa, hapo baadae Baraza la Manispaa litakwenda kutunisha mfuko wake wa mapato, kupitia vikuta na fremu za milango zilizomo.



Maana alisisitiza kuwa, ujenzi wa vituo hivyo vya wajasiriamali vya Unguja na Pemba, vipo kwa ajili ya kuwawekea mazingira mazuri, wajasiriamali.

‘’Kama mlivyosikia kuwa, ujenzi wa Kituo cha wajasiriamali hichi cha Michakaini, fedha nyingi zimetumika, sasa lazima wajasiriamali wahamie, ili wafanye kazi zao kwa ufanisi,’’alisisitiza.

Kwa wakati huo, alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia, wajasiriamali wote wa Unguja na Pemba, kila anayeomba mkopo, atapatiwa na serikali.

‘’Huku tunaendelea kutoa mikopo, na wakati huo huo tunawaondoa wajasiriamali kufanyabiashara zao, pembezoni mwa barabara,’’anasisitiza.

Na ndio maana, baadhi ya wajasriamali wakasema kituo hicho cha kisasa, ni msaada mkubwa kwao, kwa ajili ya kupata utulivu wa biashara zao.

HALI HALISI BAADA YA MIAKA MIWILI YA UFUNGUZI

Ilitarajiwa mno, kuwa shilingi milioni 107,190,000 zikusanywe na Baraza la Manispaa Chake chake Pemba, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, baada ya ufunguzi wa kituo hicho.

Ingawa, imebainika kuwa hazikupatikana, baada ya wajasiriamali kugoma kukitumia kituo chao cha Michakaini Chake chake Pemba kwa wakati, uliokusudiwa.  

Maana kituo hicho kipya kilichojengwa kwa ajili yao, kina milango 63 ya maduka, ambapo kila mmoja Baraza lilikusudia kuukodisha kwa shilingi 50,000.

Hapo, Baraza hilo lilikusudia, kujipa wastani wa shilingi milioni 3,150,000 kwa kila mwezi mmoja, na hasa kuanzia mwezi Novemba mwaka 2023.



Ingawa imebainika, baada ya wajasiriamali hao kukataa kuingia kituoni humo, Baraza hilo, kuanzia mwezi Novemba, 2023 hadi Januari mwaka huu, limeshapoteza shilingi milioni 85,050,000.

Aidha mapato ya shilingi ya milioni 22,140,000 nayo hayakukusanywa na Baraza hilo kwa kipindi hicho, yaliokuwa yatokane na vizimba ‘vikuta’ 82.

Ambapo kwa mujibu taarifa za uongozi wa Baraza hilo, kila kimoja, kilitarajiwa kukukodishwa kwa shilingi 10,000 kwa wajasiriamali.

Ikafahamika kuwa, vikuta hivyo kama vyengepata wajasiriamali, kwa mwezi mmoja Baraza lingekusanya shilingi 820,000, sawa na jumla shilingi milioni 3,970,000 ijumuisha na kodi ya milango 63.

Ndani ya kituo hicho kilichofunguliwa mwezi Novemba mwaka 2023, Baraza la Manispaa lilitarajia wajasiriamali wa nguo za mtumba na wauza viatu, wakitumie na kuanza kulipia vikuta 82 na milango 63.

Na ndio maana baada ya wajasiriamali hao wa mji wa Chake chake kugoma kikutimia kituo hicho, walilisababishia Baraza la Manispaa hilo, kupoteza mapato ya zaidi ya shilingi milioni 107.190 kwa fremu 63 za milango na vizimba 82 kukosa wateja.

Uchunguzi ulibaibi kuwa, baada ya kufunguliwa kwa kituo hicho mwezi Oktoba mwaka 2023, mwezi uliofuata Baraza hilo la Manispaa, lilianza kuwahamisha wajasirimali, hasa wauza mitumba na viatu, kuhamia kituoni hapo.

Kwa wakati huo Askari na uongozi mzima wa Baraza la Manispaa, ulihamia ndani ya mji wa Chake chake, ili kuwasaka wajasiriamali, wanaopanga bidhaa zao chini na kuwaomba kuingia kituoni hapo, bila ya mafanikio.

Msaidizi Ofisa Mapato wa Baraza hilo, Said Mabrouk Juma, alikiri kuwa, kulikuwa na ugumu kwa wajasiriamali wa nguo za mtumba, viatu na urembo kukitumi kituo hicho.

’Pamoja na kuwatumia hata askari wa jiji na wakati mwingine na Mkurugenzi kuwapitia, lakini walikataa na sisi kuendelea kupoteza mapato,’’anafafanua.



Ikafahamika kuwa, baada ya kugoma kuingia kituoni hapo, waliwaomba kwa mara nyingine, kwa sharti la kuwaondolea kodi, na kuwaomba kuchangia fedha ya umeme tu shilingi 20,000 na kukubali.

‘’Wapo waliokubali kuingia kituoni hapo, ingawa walituomba na kukubaliana nao, kwamba wasitozwe kodi na badala yake, wachangie huduma ya umeme, na hadi sasa hilo linaendelea,’’anaeleza.

Mkurugenzi wa Baraza hilo Shida Kombo Mohamed, akabainisha kuwa, kuanzia mwezi Januari mwaka 2025, rasmi walipokubaliana na wajasiriamali hao, kuchangia gharama za umeme, kituoni hapo.

‘’Ni kweli wakati wanahamia kituoni hapo, hata biashara ilikuwa ngumu kwa kukosa wateja, na ndio maana tuliwaomba kuchangia huduma umeme, kwa shilingi 20,000 kwa mwezi,’’anasema.

Wenyewe sasa, wanampango kuanzia mwezi Machi mwaka huu, kila mlango mmoja, kuuwekea mita yake ya umeme, ili kuondoa changamoto ya matumizi, kama yaliyopo sasa.

‘’Kwa sasa mchango wa umeme uko sawa kwa kila mjasiriamali, ingawa baada ya kushauriwa kuhusu kila mmoja awe na yake mita, tumelikubali na harakati zimeshaanza,’’anabainisha.

Baadhi ya wajasiriamali waliopo kituoni hapo, walikiri kuwa walikosa uwelewa na kuchelewa kuhamia ndani ya kituo hicho, jambo lililochelewa kupanua biashara zao.

Hija Omar Khamis, anasema kwa sasa biashara eneo hilo imetononoka, baada ya wateja kuzoea, tokea walipohamia mwezi Januari, mwaka jana.

Khadija Sultan, anasema umaarufu wa bidhaa za nguo za mtumba kituoni hapo, kinaendelea kukua, kadiri siku zinavyosonga.

‘’Ni kweli pale mwanzo, tulipokuwa tukiondolewa ndani ya mji wa Chake chake, tuliona kama tunaonewa, ingawa sasa biashara imechangamka kiasi,’’anasema.

Mtama Mwalimu Haji, anasema eneo hilo sasa limekuwa lulu kwa wenzao, kuja kuwaomba wachanganye biashara, baada ya kuona soko limekuwa.

MAKUSANYO YA WIZARA NA BARAZA LA MANISPAA CHAKE CHAKE

Aliyekuwa Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohamed, wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, alisema wizara hiyo iliidhinishiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 5.109.

Ambapo ni kupitia mafungu yake ya bajeti, kwa ajili ya kuchangia Mfuko Mkuu wa Serikali, ingawa hadi mwezi Machi 2025, ilifanikiwa kukusanya zaidi zaidi ya shilingi bilioni 3.126 sawa na asilimia 61.

Kwa Baraza la Manispaa Chake chake, kwa mwaka huo wa fedha, lilikadiria kukusanya shilingi milioni 880, 788, ingawa nalo lilikusanya wastani wa shilingi milioni 459. 385.

Aidha mwaka huo pia, lilifanikiwa kutoa mchango wa fedha kwenye mfuko wa pamoja wa kuwawezesha wananchi wa shilingi milioni 43.814.

Mapungufu hayo ya makusanyo ya wizara, yanaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa, kwa Baraza la Manispaa Chake chake kutokusanya zaidi ya shilingi shilingi milioni 107 kwenye kianzio kipya cha mapato.  

             mwisho   

Comments

  1. Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.

    Niliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com

    WhatsApp: +2349046229159

    Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
    Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.

    Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.

    Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.

    Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.

    Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.

    Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi

    ReplyDelete

Post a Comment