Skip to main content

BARABARA MIZINGANI-WAMBAA YAANZA UJEZNI KIWANGO CHA LAMI




NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANANCHI wa shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema sasa wanaelekea kuondokana na changamoto ya muda mrefu ya usafiri, kufuatia kuanza kwa ujenzi wa barabara yao, kwa kiwango cha lami.

Walisema, walidumu zaidi ya miaka minane, wakiwa napita kwenye barabara iliyojaa changamoto, kwa kuwepo mashimo yenye kina kirefu, misingi isiyotarajiwa, jambo lililokuwa likiwapa usumbufu.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani humo, walisema kwa sasa, wanaelekea kusahau machofu na dhiki ya barabara chakavu, kufuatia kuanza kwa ujenzi wa kiwango cha lami.

Walieleza kuwa, walikuwa wakiahidiwa na wizara husika kwamba, iko siku ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha lami utafanyika, ingawa hawakuamini, kutokana na kukaa kwa siku nyingi.

Mmoja kati ya wananchi hao Asha Khamis Juma, alisema sasa wanaanza kuona nyota njema, kufuatia serikali kuanza kutimiza ahadi ya ujenzi wa barabara yao.

‘’Tumeshayashuhudia magari ya kampuni ya Iris Constriction, yakianza kusafisha barabara hiyo, na tulipoitwa tuliarifiwa na wajenzi kuwa, ni kwa kiwango cha lami,’’alieleza.

Nae Mayasa Haji Mohamed, alisema kwa sasa wanahamu kubwa, kuona siku moja barabara yao inamalizika kwa kiwango cha lamu, ili wasahau machungu.

‘’Kwa siku za karibuni, baada ya kumalizika nguvu ile lami baridi iliyotengenezwa kwa zaidi ya miaka 14 sasa kuharibika, ilitulazimu tunapokwenda Mkoani, kuzungurikia Mgelema, ili kuyakimbia mashimo,’’alisema.

Nae mfanyabishara Khamis Omar Khamis, alisema wamekuwa wakipata dhiki ya kusafirishia bidhaa zao, kutokana na barabara yao, kuzidiwa na uchakavu.



Dereva mwenye gari ya abiria ya Wambaa-Chake chake Khamis Haji Mohamed, alisema walilazimika kupitia barabara ya shehia ya Mgelema- Kipapo, ili kukimbia mashimo ya barabara yao ya Mizingani- Wambaa.

‘’Ukiitumia barabara hiyo kwenda mjini, ukifika uanzie gereji aidha kuna msumari umetoka au skuruu imekatika, kutokana na uwepo wa mashimo makubwa,’’alilalamika.

Mapema Ofisa Mdhamini, wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma, alikiri kuwa tayari ujenzi wa barabara ya Mizingani-Wambaa, umeshaanza kwa hatua za awali.

Alisema, waliokabidhiwa ujenzi huo ni kampuni ya Iris Construction, ambayo imeshaanza kwa hatua za usafishaji wa barabara hiyo.

Alieleza kuwa, ujenzi huo, pia utajumuisha barabara ya Sisimizini- Andikoni ambako kuna umabali wa kilomita 2, ambazo zitajumuisha kwa kiwango cha lami.

‘’Ni kweli baada ya majadiliano makubwa, wizara sasa imeamua kuhakikisha barabara zote, zilizojengwa kwa kiwango cha lami baridi na mfumo wa ‘labor base’ sasa kuzijenga kwa kiwango cha lami,’’alifafanua.

Aidha Ofisa Mdhamini huyo, alisema ujenzi huo utakwenda moja kwa moja hadi kwenye uwekezaji wa hoteli, ili kuhakikisha inarahisisha usafiri kwa watu mbali mbali.

Akizungumzia kuhusu utaratibu wa ulipwaji wa fidia, alisema baada ya kumalizika kwa sikukuu za krismas na mwaka mpya, wathamini watapita kila nyumba, iliyokando na bara bara, ili kuanza harakati za kulipwa.

‘’Kuanzia mwezi ujao, wenzetu wanaohusika watapita na kuchukua taarifa za kila mmiliki wa nyumba, ili kuhakikisha analipwa na kupisha ujenzi wa barabara hiyo,’’alifafanua.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Rashid Hadid Rashid, aliwaambia waandishi wa habari, kuwa ujenzi wa barabara hiyo na nyingine, utafanyika ndani ya mwaka huu wa fedha.  

Barabara nyingine ambazo zitaingia kwenye ujenzi wa kiwango cha lami ni Mtambile- Kangani, Kenya- Chambani na Mtambile- Mwambe, ambazo barabara hizo zilifunguliwa miaka 14 sasa.

Ambapo ujenzi wa barabara hizo, ulifanywa kwa mfumo wa lami baridi, na kuwashirikisha wananchi mwanzo hadi mwisho, ilijengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya mapinduzi na shirika la misaasa la Norway (NORAD).

                                 MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...