NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR @@@@
MKURUGENZI wa Chama cha
wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali,
amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi majimboni, ili kuongeza ushiriki wao bila ya kuogopa
vitisho.
Dk. Mzuri ameyasema hayo leo Oktoba 1, 2024
ukumbi wa mikutano wa chama hicho Tunguu Unguja, katika kikao cha kueleza namna
gani wanawake watapata ulinzi dhidi ya ukatili wa
kijinsia mitandaoni, kupitia mradi wa
wakuwawezesha waandishi wa habari vijana.
Amesema kuwa, hamu yao ni
kuona wanawake wengi wanaingia majimboni
kugombea nafasi mbali mbali, lakini suala la udhalilishaji mitandaoni,
linawarudisha nyuma.
“Jamii inaamii mtu akitaka
kugombea nafasi ya uongozi ni lazima awe msafi kwa asilimia 100, lakini
mwanamke ni binadamu na hakosi mapungufu,’’alisema.
Amesema kuwa, moja kati ya
kikwazo kikubwa kwa wanawake katika kugombea ni vitisho kutoka wagombea wanaume.
‘’Wanawake musiogope
kujitokeza kugombea, kwani wamekuwa kidogo katika kugombea nafasi za uongozi, wakisumbuliwa
na ukatili wa wa kijinsia mitandaoni
lakini musivunjike moyo,’’alifafanua.
Afisa kutoka Mamlaka ya
kuzuia rushwa na uhuhumu wa uchumi Zanzibar ‘ZAECA’ Yussuf Juma Suleiman, amesema
moja kati ya vikwanzo vinavyowarudisha
nyuma wanawake katika kugombea nafasi za
uongozi ni rushwa ya ngono.
Amesema kuwa, kabla wanawake
hawajaingia katika kugombea nafasi za uongozi, ni vizuri kupewa elimu ya uraia,
ili kujua miiko na misingi ya uongozi, ili wasiwe na mwanya wa kutoa rushwa.
Aidha amesema kuwa, serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imepitisha sheria mpya ya kuzuia rushwa na uhujumu wa
uchumi, sheria namba 5 ya mwaka 2023, kifungu cha 53.
Amesema, kifungu hicho
kimeharamisha rushwa ya ngono, kwa kukataza mtu yoyote kushawishi, kuahidi
kufanya ngono na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka saba na kisichozidi
miaka 10.
“Rushwa ya ngono ni uhalifu
kama ulivyo mwingine, na serikali imeazisha sheria ili kukabiliana nayo, lakini
wandishi wa habari toeni elimu ili wanawake wanaotia nia wasiwe ni mwanya wa
kutokea rushwa,’’ alisema.
Nae Afisa sheria Mwandamizi kutoka
ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Abdul-razak Said Ali amesema serikali imekuwa ikichukua jitihada mbali
mbali, katika kumuwezesha mwanamke kugombania nafasi za uongozi ili kuongeza
ushiriki wao.
Alisema kuwa, moja ya hatua
iliyochukuliwa na serikali ni kuongeza kifungu katika sheria ya vyama vya siasa
nambari 1 ya mwaka 2024, kifungu namba 10 (c) ndani ya marekebisho, kinatoa
masharti yanayohusiana na uanzishwaji wa dawati la kijinsia na ushirikishwaji
wa jinsia na jamii.
Na washiriki wa mkutano huo Mwalim
Mwatima Issa, Rashid alisema wandishi wa habari wanatakiwa kujipa kipaumbele
katika kufanya kazi zao.
Nae mshiriki Nusra Shabani
aliuliza kwanini vyama vidogo vya siasa, havipewi ruzuku ili kuviwezesha
vishiriki kikamilifu katika uchaguzi.
Mwisho
Comments
Post a Comment