NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@
SKULI ya sekondari ya Connecting Continent iliyopo
nje kidogo ya mji wa Chake chake, ni miongoni mwa skuli 10 binfsi zilizopo kisiwani
Pemba.
Skuli hiyo ipo nje kidogo ya mji wa
Chake Chake, imekuwa ikiwavutia zaidi na wanafunzi wasichana kutokana na
upasishaji wake mzuri wa kila mwaka.
Conecting ni miongoni mwa skuli 10
binafsi kisiwani Pemba, zilizobahatika kuruhusiwa kuwekeza katika elimu kwa
ngazi ya sekondari.
Skuli hiyo ilianzishwa mwaka 2006
ikimilikiwa na wawekezaji wajerumani, ikiendeshwa na michango midogo midogo ya
wafadhili wenyewe na ada nyepesi zinatolewa na wazazi na walezi.
Skuli hiyo ilianza kufanya
mitihani ya taifa mwaka 2008, na kufika mwaka 2022, wanafunzi 671 walihitimu.
Kati ya wanafunzi hao wanawake
walikuwa 332 na wanaume walikuwa 339 kwa wakati huo, wakitokea skuli mbali
mbali za msingi kisiwani Pemba.
Mwandishi wa makala hii hakutaka
hadithi za mdomo alitaka kujua kinaga ubaga historia japo fupi ya skuli hio hadi
ilipofika.
Mwalimu mkuu skulini hapo mwana
mama Mwache Juma Abdalla, anasema kuwa mwaka 2020 wanafunzi 58 walifanya
mtihani wa taifa kidato cha nne, 24 wanawake na 34 wanaume,mwaka 2021, 43 wanaume
17 wanawake 26, mwaka 2022, 83 wanaume 28 na wanawake 55.
Mwaache anaeleza kutokana na
ufaulu kupanda mwaka hadi mwaka ni uthibitisho tosha kuwa, skuli hiyo, jambo
ambalo litaweza kufikia malengo waliyojipangia.
Anaeleza kuwa, idadi kubwa ya wanafunzi
wanaofaulu ni wanawake, na ndio maana kila mwaka wanapokea zaidi wanafunzi wa
jinsi hiyo.
Anaona Serikali ya Mapinduzi inafanya
jitihada mbali mbali kuhakikisha kila mtoto, anapata haki ya msingi ikiwemo
elimu.
Kutokana na umuhimu huo, ndipo Serikali
ikaruhusu mashirika na taasisi mbali mbali hata kutoka nje kuwekeza tasnia hiyo
nchini, kwa maendeleo zaidi.
Hatuwa hiyo ni pamoja na kuanzisha
skuli za maadalizi, msingi na Sekondari kwa kufuata misingi na kanuni
zilizowekwa.
LENGO LA WAMILIKI KUANZISHA SKULI HIYO
Moja ni kuwasaidia wananachi wa Zanzibar,
kupata skuli bora itakayoinua maisha yao kwa
maendeleo, na kupata elimu yenye kiwango.
Anafahamisha kuwa, skuli hiyo inachukuwa
wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji maalum, ili makusudi lengo liweze
kufikiwa.
Lengo ni kuona kila mmoja, anapata
haki hiyo ya elimu sawa kama wanavyopata wengine katika jamii mbali mbali.
Akielezea suala la kupokea
wananfunzi kwanza zipo taratibu mbali mbali hufanyika ikiwemo usaili utakaoleta
majibu mazuri.
‘’Tunafanya mitihani mara mbili
kwa kipimo zaidi na ili mwanafunzi turidhike nae na kuendelea na darasa la tisa
nilazima afikie daraja C, bila hapo skuli haichukui kwani itakua ni mzigo bila
matunda,’’anasema Mwalimu huyo Mkuu.
Akigusia mafanikio, anasema ni
mengi na makubwa, ikiwemo kupasisha wanafunzi katika kiwango cha juu kila
mwaka, kuengezeka kwa madarasa kutoa vyumba vinne (4) na kufikia 10, maabara
tatu (3) na maktaba.
WANAFUNZI WA SASA
Fatma Mohamed Bakar anaesoma kidato
cha tatu mwenye ulemavu wa viungo, anaeleza sababu zilizomfanya kujiunga
skulini hapo, ni pamoja na kiwango kizuri cha ufaulu hasa wanawake.
‘’Waalimu wa skuli hii wanakua na
juhudi binafsi katika ufundishi, ambao unatufanya kila mmoja kufahamu na kisha
kufaulu,’’anasema.
Husna Mohamed Haji anaeleza amejiunga
katika kituo hicho mwaka 2021, akiwa darasa la tisa baada ya kupasi michepuo
katika skuli ya Pindua.
Anaeleza kuwa licha ya kuwa na upungufu
wa usikivu haikuwa changamoto kwake, kutoendelea na masomo katika skuli hiyo
kubwa.
“Nashukuru kwa kuwapa moyo wa
imani wazazi, walimu wangu pamoja na wanafunzi wenzangu na jamii iliyonizunguka
hadi nilipofika,’’anasema.
‘’Walimu wanaposomesha hutoa sauti ili niweze kusikia
na kufahamu vizuri kinachosomeshwa na kisha hufanya vizuri kuanzia mitihani ya
ndani hadi taifa,” anaeleza.
Kwa upande wa malengo yake ya
baadae Husna anasema ni mengi moja ni kuhakikisha anasoma kwa bidi hasa masomo
ya sayansi ili kufikia ndoto zake yakuwa ijinia.
‘’Lengo langu nikuhakikisha
najikita zaidi kusoma masomo ya sayansi
ikiwemo physics,Chemistry na hesabati,(PCM)ili niwe injinia,” alieleza.
KWA UPANDE WA MATOKEO KWA MWAKA
Mwaka
2022 katika ufaulu wa wananfuzni walipata daraja la tatu, nne, lakini miaka ya karibuni
kiwango cha ufaulu kilipanda.
Mwalimu huyo anaeleza kuwa, hiyo
ni kutokana na ushirikiano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe, kuhakikisha
wanatoka walipokuwa na kufika pale wanapotaka kimaendeleo.
Anaeleza kuwa mashirikiano hayo ndio
njia pekee iliyopelekea kuondosha daraja la nne na zero, na kupata daraja la
kwanza, la pili na tatu tu.
Ambapo kwa mwaka 2022 skuli
ilifanikiwa kupasisha kwa kiwango cha daraja kwanza wanafunzi 4, daraja la pili
wanafunzi 43, la tatu wanafunzi 30, na daraja la nne walikuwa
wanafunzi wawili (2).
Hivyo matokeo hayo ni ushahidi
tosha kwamba skuli hiyo inatoa matokeo mazuri zaidi kuliko skuli nyengine za
binfsi zilizopo Kisiwani humu, ni takribani miaka 8 sasa hakuna zero.
MASHIRIKIANO NA SERIKALI.
Mwalimu huyo anasema mashirikiano
baina yao na Wizara ya elimu ni mazuri, na ndio maana wakaweza kufikia hapo
walipo sasa.
‘’Bila mashirikiano na Wizara tusingalifika
hapa tulipofika kimaendeleo, kwani kila jambo linahitaji mashirikiano.
CHANGAMOTO
Alisema kuwa nikukosa dahalia la
uhakika kwa watoto wanafunzi, kwani sehemu wanalala ni nyumba za watu binafsi.
‘’Zipo yumba za watu binafsi
wazazi ndio wanatoa fedha zao kwa ajili yakulipia kodi na chakula, jambo ambalo
linawapa mashaka, kwa kuwepo uangalizi mdogo hasa kwa wanaume.
Akizungumzia suala la kodi kwa
Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA, ameomba wafanyiwe msamaha kwani kituo hicho
hakipo kibiashara kipo kusaidia jamii zaidi kupata elimu.
‘’Kwa mfano hapa wapo wanafunzi
300, lakini wapo waliofiliwa na mzazi, wenye mazingira magumu na wenye kipato
duni hawalipi ada,’’anasema.
Hivyo mamlaka hiyo ni vyema kumuunga
mkono mfadhili huyo, kwani lengo ni kusaidia
watoto hasa mayatima na wenye hali ngumu na sio kibiashara.
WALIOWAHI
KUSOMA
Juma Kitwana Bilali anaeleza kuwa,
Connecting ni miongoni mwa skuli binafsi yenye kiwango kizuri cha kupasisha
hasa watoto wa kike.
‘’Mimi nimesoma connecting na kwa
sasa nasomesha wenzagu katika kituo hichi,” anaeleza.
Hivyo kuwataka wazazi na walezi
kuendeleza mashirikiano kwa walimu, ili wapate kuboresha taaluma hiyo kimaendeleo.
Mwanafunzi Omar Ali Juma, anasema
ameshawahi kuwa baharia katika meli za nje, baada ya kumaliza elimu yake ya
sekondari skuli hapo.
MALENGO YA SKULI BAADAE
Mwalimu huyo anasema ni kufika mbali
zaidi kielimu, kutoka walipo kimatokeo, na pia kuwa na wanafunzi hadi wa kidato
cha sita.
Akizungumzia suala la upasishaji
anasema kuwa wanaka kuwa na kiwango cha daraja daraja la kwanza, na pili tu sio
tatu, nne wala zero.
Skuli ya Conecting Continent Organization
iliyopo Mgogoni Wilaya ya Chake Chake imeanzishwa mwaka 2006, ikiwa na wanafunzi
18 tu wa darasa wa tisa.
Ambapo kwa sasa wapo na wanafunzi wakidato
cha nne 58, wakiwemo wakike 29 na wakiume 29, wanaotarajiwa kufanya mitihani
yao ya taifa kwa mwaka 2023.
Mwenyekiti wa bodi ya wazazi skulini
hapo Said Mohamed Ali anasema kuwa skuli ipo vizuri kiutendaji kwani kimatokeo
takribani miaka 8 sasa hawajawahi kufelisha.
Anachojivunia Mwenyekiti huyo ni
umoja, mshikamano uliopo baina ya waalimu, wazazi na Bodi ya wazazi skuli hapo.
Afisa Mkurugenzi wa mamlaka ya mapato ZRA Pemba Jamal Hassan Jamal, amewataka watendaji wa skuli hiyo kujisajili na kulipa kodi ili kuondosha changamoto zisizokuwa za lazima.
Anaeleza kuwa Serikali haina nia
ya kumkwaza mtu bali ipo kusaidia wananchi wake, hivyo kuwataka kujisajili
mamlaka kwa mujibu wa kipato chao.
“Ipo sheria namba 7 ya mwaka 2009
inasema yoyote anayeanzisha biashara kwa ajili yakujipatia kipato, lazima
kuomba usajili mamlaka ya mapato Zanzibar.
Aidha kuwataka kufuata sheria
kuomba usajili ZRA, ili kuepusha kwa ujenzi wa taifa.
MWISHO.
Comments
Post a Comment