Na Muandishi wetu Zanzibar@@@@
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) Mhandisi Dkt
Mngereza Mzee Miraji amesema Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Zanzibar
2022-2027 wenye lengo la kuimarisha sekta ya maji na kumaliza tatizo la maji safi na
salama Zanzibar alianzisha kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo mbali mbali.
Mhandisi Dkt Mngereza aliyasema hayo jana katika hafla iliyoandaliwa ya
kumkabidhiwa Tuzo ya Kifahari ya VIP Global Water Change Maker, Mhe Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husseini Mwinyi iliyofanyika jana
Ikulu Zanzibar.
Alisema katika kipindi ulichoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na
Madini alichukuwa juhudi mbali mbali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya
maji safi na salama, kwa kukutana na Mashirika ya Kimataifa ya Misaada ikiwemo
JICA, USAID, BPI, Banks ikiwemo AFDB, wawakilishi wa balozi mbalimbali ikiwemo
UK, EU, JAPAN n.k.
Alielezea kwamba hivyo Wizara ya Maji, Nishati na Madini (WMNM) na Taasisi ya
Ushirika wa Wadau wa Maji (GWP ) walishirikiana kuandaa mpango huo uliojumuisha
wataalam wa fani mbalimbali kutoka Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Tanzania (SMT),
South Afrika na Ethiopia chini ya ufadhili wa GWP ambapo mshauri elekezi wa kikosi
alikuwa Dkt Victor Kongo.
Aliesema kuzinduliwa kwa Mpango huo pamoja na kuutangaza kwa kufanya
Makongamano na Warsha mbali mbali kulipelekea Washirika wa Maendeleo kujitokeza
na kuonesha nia ya kuunga mkono Serikali Zanzibar katika kutatua changamoto ya
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Mhandishi Dkt Mngereza alisema Miongoni mwa Washirika wa Maendeleo walijitokeza
ni pamoja na KFW na GIZ za Ujerumani, Ruden Institute ya Norway, UNESCO-IHI Delft
ya Uholanzi, JICA ya Japani na Benki ya EXIM India.
Aidha alimshukuru Rais Mstaafu Jakaya Mrisho, kupitia GWP kwa juhudi zake za
kubeba jambo hili kwa hatua zote,alipokuwa Dakar,nchini Senegal aliagiza utekelezaji
wa hilo na baada ya muda mfupi alipatikana na kuanza kazi, May-Nov 2022.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ushirika wa Wadau wa Maji (GWP ) Dkt Victor
Kongo alisema zoezi la Mpango Mkuu wa maji lilikua gumu kidogo kwani ilibidi watafute
nyaraka na ripoti mbali mbali kuanzia miaka ya 60 iliyopita hadi sasa ili kutambua
miundo, mifumo na mipangilio iliyopo ya usimamizi wa sekta ya maji Zanzibar na
changamoto zake. Pia, walifanya tathmini kutambua wingi na ubora wa rasilimali maji
Zanzibar na changamoto za usimamizi wake.
Alisema kupitia mashirikiano mazuri na taasisi ya Global Water Partnership, Dkt.
Mngereza aliweza kuhudhuria kikao cha dunia cha World Water Forum kule Dakar
Senegal ambapo alikutana na wadau wa kimataifa katika sekta ya maji.
Alifahamisha kwamba wadau hao ni pamoja na mkuu wa chuo cha kimataifa cha IHE-
Delft kilichoko Uholanzi ambacho ni hodari katika utafiti na taaluma katika sekta ya maji.
Alisema Pia kupitia chuo hicho pamoja na taasisi ya SADC Groundwater Monitoring
Institute, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wizara ya Maji nishati na Madini
walianzisha kongamano la kila mwaka la kisayansi kuhusu maji Zanzibar ambalo
lilifanyika kwa mara ya kwanza tarehe 14-15 Septemba mwaka 2022 na litakuwa
likifanyika kila mwaka.
Alifahamisha tathmini waliyoifanya ilibainisha mambo makuu saba kati ya mambo hayo
ikiwemo athari za mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya maji Zanzibar, Kwa muda
mrefu, hakujakuwa na mpangilio maalum au Programme ambayo ina ratibu mwenendo
wa utekelezaji wa miradi katika sekta ya maji. Hali ambayo ilisababisha kutokuwa na
muelekeo maalum wenye malengo katika sekta ya maji.
Vile vile alisema Sera ya maji ya 2004 ina mapungufu kadhaa ambayo inatakiwa
kushughulikiwa kwa kufanya mapitio ya hiyo sera. Pia Kunahitajika hatua madhubuti za
kuboresha miundo mbinu iliyopo na pia kuongeza miundo mbinu mipya ya kusambaza
maji.
Sambamba na hayo hatua madhubuti zinahitajika kujenga mashirikiano na taasisi za
kikanda na kimataifa katika sekta ya maji ili kupanua wigo wa mashirikiano ya kitaluma
na utafiti.
Aidha Dkt Mngereza na Dr Victor wamempongeza Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali
Mwinyi kuwa Mpokeaji wa Kwanza wa Tuzo ya Kifahari ya VIP Global Water Change
Maker, pamoja kuwa pongeza viongozi wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini kwa
Kuendeleza utekelezaji wa Mpangu Mkuu wa Maji Zanzibar.
Mwisho.
Comments
Post a Comment