NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KILA ifikapo Juni 5 ya kila mwaka, Zanzibar huungana na nchi nyingine,
kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Siku hii kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, ilianzishwa mwaka wa1972,
ambapo ni miaka 54, sasa imeshapita.
Iliasisiwa wakati wa mkutano wa Stockholm wa Umoja wa
Mataifa, tena kuhusu mazingira ya binadamu nchini Sweden.
Inafafanuliwa kuwa, pia mkutano huo, ulipitisha azimio la
kuunda United Nations Environment Programme (UNEP), ili
kuongeza juhudi za kimataifa za kupamba na uhifadhi wa mazingira.
Aidha mtandao wa dcc.go.tz unaripoti kuwa, sherehe
rasmi ya kwanza, ilifanyika mwaka wa 1973 chini ya kaulimbiu “Dunia Moja
Pekee”.
Tena tarehe hii, imekuwa jukwaa la kimataifa la kuhamasisha jamii,
kuchukua hatua za kulinda , kuhifadhi mazingira na kuendeleza uendelevu wa rasilimali
za asili.
UNEP, inahimiza jamii kuchukua hatua kali dhidi ya wale wachafuzi,
waharibifu wa mazingira wakifafanua kuwa, anariharibu dunia na sio eneo moja
pekee, bali ni yote.
Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nalo pia limekuwa likitekeleza
kampeni za kupunguza matumizi ya plastiki, ikiwemo kuhamasisha matumizi ya
mifuko mbadala rafiki kwa mazingira.
Kupitia tovuti ya vpo.go.tz, inafafanua kuwa, siku
hii ya leo ya mazingira duniani, huwa na umuhimu mkubwa kwa jamii, ikiwemo kuongeza uelewa
wa kimazingira.
Umuhimu mwingine ni kuhamasisha watu kuchukua hatua za kulinda
mazingira, na kupunguza uchafuzi, ambao athari yake ni kubwa.
Siku hii, huwasaidia wanajamii kupata fursa ya kuelewa wajibu wao,
katika uhifadhi wa rasilimali za asili, na kuondoa dhana kuwa, miti hujioatea
wenyewe.
IPI MIKAKATI YA SMZ KULINDA, KUHIFADHI MAZINGIRA
Kwa Zanzibar, ipo Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais, ndani yake ikiwemo Idara na Mamlaka za kusimamia uhifadhi wa
mazingira.
Maana hivi karibuni, akisoma bajeti ya
wizara hiyo, Kaimu wa Waziri Hamza Hassan Juma, alisema wazi kuwa, uhifadhi wa
mazingira ni jukumu la kila mtu.
Akafafanua kuwa, hilo litahakikisha kuwa,
nchi inadumu, kwa kuzuia uchafuzi wa hewa, maji, na ardhi kupitia upandaji
miti, utupaji taka sahihi, na kuepuka uharibifu wa misitu.
Akasema serikali yenyewe, haijalala
katika kuhakikisha mazingira Zanzibar yanakuwa kama yale ya asili, kwani ipo
mikakati kadhaa.
‘’Rasimu ya awali ya ripoti ya hali halisi
ya mazingira ya miaka mitano ya 2021/2026, imeonesha ongezeko la joto katika
bahari, na asidi ambayo imepelekea kufubaa kwa matumbawe,’’anafafanua.
Jingine anasema, ni kuongezeka kwa kina
cha bahari, uingiaji wa maji ya baharà katika maeneo ya kilimo na makaazi,
kupungua uzalishaji wa mwani na kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji taka.
Mkakati mwingine uliotajwa na Kaimu waziri
huyo ni kuchukua juhudi za kutekeleza, matakwa ya Mkataba wa kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC),
Tena ni kwa kukamilisha mikakati ya kitaifa,
kikanda na kimataifa ikiwemo NDC, NAP pamoja kufanya tathmini ya maeneo 60,
yanayoingia maji ya bahari.
Jingine ili kukabiliana na uharibifu na
uchafuzi wa mazingira, matayarisho ya michoro na gharama za ujenzi wa matuta,
kuta za kuzuia maji ya bahari katika maeneo ya Mtangani.
‘’Maeneo mingine ni Mtambwe, Ndagoni,
Maisara na Bumbwini Mafufuni, pamoja na kudhibiti matumizi ya mifuko ya
plastiki,’’anaeleza.
Ambapo kwa mwaka 2025/2026 kilogramu
2,263, Unguja kilogramu 1,736.5 na Pemba kilogramu 526.5 zimekamatwa, kufuatia
doria zinazofanywa.
Hamza anaeleza kuwa, baada ya kukamatwa
kwa mifuko hiyo, wafanyabiashara walitozwa faini ya shilingi bilioni 9.100, ikilinganishwa
na kilogramu 400 zilizokamatwa kwa mwaka 2024/2025.
Kaimu huyo Waziri, akasema wakati leo Zanzibar
ikiadhimisha siku ya mazingira duniani, kumbe hayo ni mafanikio makubwa,
yaliyopatikana katika kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki, kupitia
operesheni 54 zilizofanywa.
Juhudi
nyingine za serikali, ni uimarishaji wa uhifadhi wa mazingira, ambapo kwa mwaka
2025/2026, maeneo139, yamekaguliwa kiwilaya ikilinganishwa na maeneo 185, kwa
mwaka 2024/2025.
Tena ukaguzi ukaonesha kuwa, wilaya ya
Kati Unguja, iliongoza ikifuatiwa na Chake chake Pemba, kisha Magharibi ‘B’ na
Micheweni, kwa kuwa ni maeneo yanayochimbwa rasilimali, zisizorejesheka.
Serikali,
imekuwa ikitoa miongozo ya kimazingira iliyosaidia, kupunguza kero, uchafuzi na
uharibifu wa mazigira, imetolewa na tathmini 101 za kimazingira, ambapo Unguja ni
68, Pemba 33 zilifanyika,
Kwa mwaka wa fedha huu, Afisi hiyo inayo
programu kuu ‘P00201’, ya uratibu wa mabadiliko ya tabianchi.
Ambapo matokeo ya muda mrefu ni kuwa na
mazingira endelevu, pamoja na kupungua kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Zuri zaidi, kwa juhudi za serikali katika
mapambano dhidi ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira, kwenye programu hiyo,
kwa mwaka uliopita, ilitekeleza shughuli kadhaa, ikiwemo kukuza uwelewa wa
biashara ya kaboni.
Kaimu Waziri huyo, akagusia kuwa, kwa
mwaka 2026/2027, malengo yao ni kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa mazingira,
pamoja jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Na ndio maana, programu kuu ya uratibu wa
mabadiliko ya tabianchi, imeombewa shilingi bilioni 7.909, zikiwemo fedha za
mishara na miradi kadhaa ya maendeleo.
Kisha Afisi imepanga shabaha kadhaa,
ikiwemo kutayarisha kanuni na miongozo ya kimazingira, na kufanya tathmini ya
hali halisi ya mmong’onyoko wa fukwe.
Jingine
ni kuandaa mandiko ya miradi ya kimazingira na mabadiliko ya tabiachi, pamoja
na kukuza uelewa kwa jamii, juu ya mazingira na mabadiliko tabianchi.
JAMII
INAONAJE MIKAKATI HII
Ali Khamis Makame wa Makoongwe Mkoani,
anasema kama sio kelele za serikali, sasa kusingekuwa na mkoko hata mmoja, baharini.
Omar Haji Kassim wa Wambaa, ansema juhudi
za serikali ikiwemo kutoa elimu kwao, ni jambo linalosaidia kuhifadhi na kutunza
mazingira.
Mahamoud Mjabu Hamad wa Kojani Wete,
anasema hata uwepo wa sheria, zinazopiga marufuku nyavu za kukokota na mitego
haramu, imesaidia.
‘’Leo tukiadhimisha siku ya mazingira
duniani, walau tunasema, Zanzibar bado kijani kibichi cha asili kipo, tofauti na
baadhi ya nchi,’’anasema.
Sauda Khamis wa Tundaua Chake chake,
anasema hata wao wamefikiwa na juhudi za serikali, maana wamepanda mikokoto
zaidi ya 1,500.
John Chicomo mwandishi wa habari mbobevu
wa mazingira, aliwahi kusema, kalamu ya mwandishi wa habari ikitumika vizuri,
inakuwa msaada wa kuhifadhi na kulinda mazingira.
Wapo wanawake 2,086 ambao ni wakulima wa kilimo msitu wa shehia
nane za Unguja na Pemba, wakiwemo wa shehia ya Mchangamdogo, Wete watanufaika
na huduma ya maji ya umwagiliaji wa kilimo chao, kufutia ‘CFP’ kuanza uchimbaji
wa visima 24.
Taarifa zinaeleza kuwa, wanawake hao walimo kwenye mradi wa miaka
mitano wa kukabiliana na mabadiliko tabianchi, kwa hatua za awali CFP, itaanza
na uchimbaji wa kisima kimoja kimoja, kati ya shehia hizo nane.
CFP kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Mbarouk Mussa Omar, anasema
tayari zoezi hilo, limeshaanza kwa uchimbaji wa kisima kimoja, shehia ya Kiuyu
Minungwini.
‘’Mradi huu wa kukabiliana na mabadiliko tabianchi, asilimia 80
unawalenga wanawake, na asilimia 20 ndio unawangalia wanaume, na ndio maana kati
ya wanufaika wote 2749, wanawake ni 2086 na wanaume ni 663,’’anafafanua.
Mkulima Mtumwa Makame Shaame wa kijiji hicho, alisema kuwa, kwa
sasa kilimo chao kimenusuriwa na uwepo wa mvua, ingawa baadae watahitaji
kutekelezewa ahadi hiyo.
MWISHO



Comments
Post a Comment