Skip to main content

KITUO CHA ELIMU MBADALA WINGWI CHEMCHEM YA AJIRA KWA VIJANA

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@

WIZARA ya Elim una Mafunzo ya Amali Zanzibar, ni moja ya wizara tegemezi hapa Zanzibar, katika kufanikisha maendeleo ya kila siku.

Wizara hii, awali ilikuwa na mfumo wa elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu pekee, kwa miaka kadhaa.

Kisha, wizara hiyo ikaanzisha mfumo wa Mafunzo ya Amali, ambao mfumo huu uliwahusu zaidi wale, walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Na kwa wakati huo, elimu ya lazima kwa Zanzibar, iliishia darasa la kumi (F11), ingawa miaka 1980, elimi ya lazima iliishia darasa la kumi na moja (F111).

Haja ya kuongeza kiwango cha elimu Zanzibar, haikuja bure bali, ilitokana na maendeleo ya kielimu ya kidunia, nah apo sasa elimu ya lazima hadi sasa kwa Zanzibar inaishia kidato cga nne.

JE WALIOSHINDWA KUMALIZA ELIMU YA LAZIMA WAFANYE NINI



Wizara kwa muda mrefu sasa na kama alivyowahi kusema Katibu mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said, kuwa hakuna mtoto wa kizanzibari ambae hatopata elimu.

Hapa, akaenda mbali zaidi, kuwa hilo linawezekana, maana zipo program za elimu mbadala na watu wazima, ambapo kwa Pemba, kituo chake cha kisasa kipo Wingwi tokea mwaka 2017.

Akasema Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima na ina lengo la kupunguza kiwango cha wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanajamii.

Ndio maana anasema kwa mwaka wa fedha 2024/2025, programu hii ilitengewa shilingi bilioni 3.404, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 1.391 ni kwa ajili ya mishahara na shilingi bilioni 2.013 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Ingawa kwa mwaka jana wa fedha, hadi kufikia Aprili 2025, jumla ya shilingi bilioni 1.315 sawa na asilimia 39 zilipatikana.

 Tena kati ya fedha hizo, shilingi milioni 233.438 sawa na asilimia 12 ni fedha za matumizi mengineyo na shilingi milioni  mia 1.081 sawa na asilimia 78 ni kwa ajili ya mishahara.

 Imefahamika kuwa, wanafunzi 1,902 wakiwemo wanaume 1,171 na wanawake 731 wamesajiliwa kujiunga na madarasa 97 ya Elimu Mbadala Unguja na Pemba.

 Kwa sasa wizara inaendelea na kazi ya tathmini ya progamu zinazoendeshwa na Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima kwa lengo la kuimarisha programu zilizopo na kuanzisha programu mpya.

Eneo jingine wizara inaendelea kuwajengea uwezo vijana, katika fani mbalimbali ambapo wapo 150, Unguja 75 na 75 Pemba, wamepatiwa mafunzo ya ushoni, vijana 42 wakiwemo wanaume 35 na wanawake saba wamepatiwa mafunzo ya uchongaji wa samani pamoja na ukarabati wa madawati yaliyoharibika.



Ikafahamika kuwa, matokeo ya muda mfupi ya program hiyo ni wanafunzi 1,902 wakiwemo wanaume 1,171 na wanawake 731 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 14, waliokuwa nje ya skuli wamerejeshwa masomoni Unguja na Pemba.

YEPI MATUNDA YA KIUTUO CHA ELIMU MBADALA WINGWI?

Vijana wa kike, wametajwa sasa kujisomea ufundi wa uunganishaji umeme majumbani, kupitia Kituo cha Elimu Mbadala cha Wingwi Pemba, ambapo hapo awali fani hiyo, ikisomwa na wanaume pekee.

Maana Kaimu mkuu wa Kituo hicho Mussa Faki Iddi, anasema wastani wa vijana wa kike 25 kila mwaka, huwapokea kituoni hapo, wakiomba fani ya ufundi wa umeme wa majumbani.

Kwa sasa fani hiyo, sio ya wanawaume pekee, kama ilivyokuwa wakati kituo kinafunguliwa mwaka 2017.

Anaongeza kuwa, fani hiyo pamoja na ushoni wa nguo ndio pekee, ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.



Kumbe kuanzia mwaka 2019 hadi sasa, wanawake wanaojiunga na kituo hicho, wapo wastani wa 25, ambao wanaomba ufundi wa umeme wa majumbani.

‘’Fani hapa zipo kadhaa ikiwemo ya ushoni wa nguo, upambaji maharusi na uchoraji piko, fundi bomba ingawa kwenye fani ya umeme, sasa na wanawake wamekuwa wingi,’’anafafanua.

Fani nyingine zinazobeba wanawake wingi ni ushoni wa nguo za aina mbali mbali kwa kutumia cherhan.

‘’Fani ya pili ambayo ninaiyona inawanafunzi wingi ni ushoni wa nguo, ambapo kila mwaka nayo hubeba kundi kubwa la wanafunzi,’’anafafanua.

Akizungumzia sifa za kujiunga na Kituo hicho, ni pamoja na wale walioshindwa kupata elimu kabisa katika maisha yao, kwa changamoto moja ama nyingine.

Sifa nyingine ni kwa wale walioshindwa kumaliza elimu ya msingi, wakiwa walikatisha njiani, kupata ujauzito au waliacha kwa mifumo ya matokeo mabaya ya maisha.

‘’Tunazingatia umri, ambapo ni kuanzia miaka 17 na mwanafunzi asizidi miaka 23, akija hapa atasomea ufundi na masomo mingine kwa miaka mitatu bure,’’anafafanua.

Kihusu vifaa vya kujifunzia, anasema vipo kwa wingi, ingawa hutokezea changamoto ua uhaba pindi idadi ya wanafunzi, ikiongezeka, katika mwaka.

‘’Hapa wanafunzi wanapata kufanyakazi wa vitendo, iwe ni wale wa upishi, uchoraji piko, fundi bomba, uchongaji na wakimaliza wanakuwa vibarua wazuri,’’anafafanua.

Sasa akawataka wazazi na walezi, kuendelea kuwaandikisha vijana wao katika kituo hicho, ili kila mmoja aweze kujiajiri katika maisha yake.

Wahitimu waliopita kituoni hapo, akiwemo Mohamed Issa Jafari, ambae kwa sasa amekuwa fundi wa uunganishaji wa umeme majumbani, anasema anaendelea kujiajiri mwenyewe.

‘’Kwa hakika kituo kile cha Elimu Mbadala kwangu ni mkombozi, maana nilishakata tamaa ya maisha, ingawa baada ya kujiunga na kumaliza, sasa nimejiajiri,’’anasema.

Mhitimu Maryam Haji Kombo wa Micheweni, anasema kwa sasa ni fundi mzuri wa nguo wa kike, na anaowateja hadi mikao ya Tanzania bara.

‘’Wapo wateja wangu hadi mikoa ya Arusha, Tanga, Dar-es Salaam, Morogoro ambao nawashonea nguo za watoto wao,’’anaeleza.

Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Hidaya, anasema kituo hicho ni kizuri mno, ikiwa serikali itaendelea kukiwezesha vifaa vya mazoezi.

Mohamed Haji Hamza na Mayasa Issa Hija ni wazazi ambao watoto wao, wameshamaliza ufundi wa aina mbali mbali, wanasema kituo hicho, kinafaa kuongezea chingine.

‘’Kwa mfano, sio kituo kuwepo Wingwi pekee, bali kila wilaya kinatakiwa kiwepo, ili kuwarahisishia wingine kunufaika na huduma hizo,’’anafafanua.

Hili la uwepo wa vituo hivi linachangiwa, na nia ya thati ya serikali ya awamu ya nane, chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Maana, wizara hiyo kwa sasa imeshaongezewa bajeti yake kuu kutoka shilingi bilioni 265.5 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni 830 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 212.6.

                                    Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...