NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MKURUGENZI wa Baraza la Mjia Mkoani
Muumini Abeid Salum, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika mashindani ya sita ya
tahafidhil-quran, ya kanda ya Wambaa wilayani humo asubuhi ya kesho Machi 14, 2026.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi, Katibu wa Jumuiya ya tahafidhil qur-an kanda ya Wambaa, Mwalimu Abdalla
Haji Ali, alisema tayari maandalizi ya shughuli hiyo, yameshakamilika.
Alisema, Mkurugenzi huyo,
atawashuhudia wanafunzi wakishindana kwa juzuu ya kwanza, pili, tatu, tano,
saba, 10 na 20, wakiwemo wanafunzi wa kike na kiume.
Alieleza kuwa, mashindani hayo ya
aina yake kwa mwaka huu, yanatarajiwa kufanyika msikiti wa Ijumaa Wambaa wilayani
humo.
Alisema, baada ya majaji kukamilisha
kazi yao hiyo na kutoa matokeo, mgeni rasmi huyo atatoa zawadi ikiwemo fedha
taslimu, kwa washindi na washiriki wote 45.
‘’Ni kweli asubuhi hii, Mkurugenzi wetu
wa Baraza la mji la Mkoani, atayashuhudia mashindani ya sita ya tahafidhi
qur-an, yanayoandaliwa na jumuiya yetu,’’alifafanua.
Akizitaja madrassa zitakazoshiriki
kwa mwaka huu, alisema ni pamoja na almadrassatul- raufu rrahim ya kijiji cha
Andikoni, Allah kadiri ya kijiji cha Wambaa.
Madrassa nyingine zilizothibitisha kushiriki ni minaatu
rrahman ya Kwazani, nur-ddin ya Ndongoni, hidayatul-
islamiya, shamsu ddini ya Kutukuu, kaafur ya Tumbi na imaniya ya
Chumbageni.
Katika hatua nyingine, Katib huyo aliwaomba waumini wa dini ya
kiislamu wa shehia za Wambaa na Chumbageni na shehia jirani, kuhudhuria katika
mashindani hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ustadhi Hassan Othman
Khamis, aliwashukuru waumini wa dini ya kiislamu na mashinrika mingine, kwa
kutoa michango yao, itayofanikisha kufanyika kwa mashindani hayo.
Alisema, michango ya wazazi, walezi, ofisi ya Mkuu wa wilaya ya
Mkoani, waalimu wa skuli za Tumbi, Kunguni, Wambaa, Mwakilishi wa Jimbo la
Chambani na baadhi ya wawekezaji, imesaidia kwa kiwango kikubwa.
Mwalimu mkuu wa almadrassatui Allah kadiri ya Wambaa Awesi
Abdalla Ali, alisema maandalizi kwa upande wake, yameshakamilika, ikiwemo wale
wanafunzi wa juzuu ya kwanza hadi ya 10.
Mshika fedha wa Jumuiya hiyo, Salma Haji Makame, alisema
walipanga kukusanya shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya zawadi za washindi na
sadaka kwa washiriki.
‘’Kwa fedha tulizokusanya mwaka huu, zimesaidia kwa kiwango kikubwa,
kufanikisha shughuli yetu, ikilinganishwa na mwaka jana, jambo ambalo tunaona
tumepiga hatua,’’alifafanua.
Baadhi ya wananchi wa shehia za Chumbageni na Wambaa walisema,
wamefurahishwa kwa kukamilika kwa maandalizi hayo, na kuwaomba wenzao kuhudhuria.
Fatma Ali Hassan, alisema ni vyema kwa wazazi na walezi wenzake,
kushiriki ili kuwaunga mkono watoto wao, kuzidi kukihifadhi kitabu cha Allah.
Raya Juma Khamis na Asha Haji Ali, walisema ni wakati wao
wazazi, kuwashajiisha watoto namna bora ya kukihifadhi kitabu cha Allah, ili
kikawe muombezi kwao.
Hii ni awamu ya sita, kwa Jumuiya hiyo tahafidhi qur-an kanda ya
Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani, kuendesha mashindani hayo, ambapo kwa
mwaka jana, ilihusisha madrassa saba pekee.
Mwisho

Comments
Post a Comment