Skip to main content

UDHALILISHAJI VYUO VIKUU NI CHANGAMOTO NYINGINE KWA WANAFUNZI, MADAWATI YA JINSIA YAWEZA KUWA MURUBAINI

 



IMEANDIKWA NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ 


VYUO vikuu na taasisi za elimu ya juu, ni sehemu  zinazotegemewa  katika uzalishaji wa wataalamu  na watumishi mbali mbali nchini.

Wataalamu hao ndio nyenzo ya maendeleo katika kila nchi duniani kote na hili hakuna anayelipinga.

Katika miaka ya hivi karibuni, vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu  vimekua vikikabiliwa na tuhuma za uwepo wa kesi za ukatili wa kijinsia, ikiwemo rushwa ya  ngono, udhalilishaji, pamoja na ukandamizaji wa kijinsia hususani kwa watoto wa kike.

 Ripoti  ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), imeeleza kwamba imeshughulikia  malalamiko ya rushwa ya ngono.

Na ndio maana majalada ‘file’ 23 yamefunguliwa katika mikoa tofauti Tanzania, jambo linalodhihirisha uwepo wa jambo hilo ovu.

Ikafahamika kuwa, kesi 10 zilifunguliwa mahakamani ambapo kesi tano ‘5 zilishinda na kati ya hizo, nne zilihusu taasisi za elimu ya juu, hii ilikua ni 2013 hadi Machi 2020 inaeleza.

Katika kulitibu hilo serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2022, chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, ilitoa agizo rasmi.



Kwamba, vyuo vikuu vyote nchini vya serikali na binafsi vianzishe madawati ya kijinsia, ili kuhakikisha wanafunzi wanakua salama wanapokuwa vyuoni.

Na hapo ndipo nyoyo za wanafunzi, wazazi na wadau wote wa elimu, zilipobeba tumaini jipya, hasa kwakuzingatia hali ya unyanyasaji wa kijinsia, ilivyo kwa miaka ya karibuni.

Ambapo kwa mujibu wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kutoka mwenzi Januari 2024 hadi Novemba 2024, matukio 1718 ya udhalilishaji yameripotiwa.

Sasa basi agizo la uanzishwaji madawati ni hatua muhimu katika kukabiliana na hali hiyo, kwani kwa sasa masuala ya udhalilishaji yameonekana kushamiri  hata sehemu zinazotegemewa zingekemea vikali matukio hayo.

NINI DAWATI LA JINSIA?

Dawati la Jinsia ni kitengo maalum  kinachoshughulikia kesi na matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia, ikiwemo ubakaji, shambulio la mwili na mengineyo.

Na lengo la kuanzishwa madawati haya vyuoni ni kutokomeza vitendo vya ukatili wanavyokumbana navyo wanafunzi, wanapokua vyuoni.



JE MADAWATI HAYO YANA UMUHIMU VYUONI?

Abbas Makame mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar anasema, madawati ya jinsia vyuoni yamekuja kutoa msaada kwa wanafunzi wanaokumbana na changamoto za udhalilishaji na ukatili wa kijinsia,

Anasema, kwani mara nyingi changamoto hizo hua ni kikwazo kwa wanafunzi kufikia malengo yao, hasa ikizingatiwa wazazi wameshapoteza rasilima fedha nyingi.

Abuu-Bakkar Amour Massoud mwanafunzi wa Chuo Cha Kiislamu Morogoro ‘MUM’anaeleza kua Madawati ya jinsia vyuoni ni chachu ya kuimarisha usawa wa kijinsia.

Anasema kuanzishwa kwa madawati hayo vyuoni, kutahakikisha usawa wa upatikanaji wa elimu, kati ya wanafunzi wanaume na wanawake, bila kujali utofauti wao wa jinsi.

"Madawati haya yatasaidia kuhakikisha mwanamke anasoma akiwa salama kama mwanamme, jambo ambalo litastawisha maendeleo ya kila mwanafunzi hapa Chuoni bila kujali jinsi yake, " anaeleza.

 Husna Ali Hamad mwanafuzi kutoka Chuo Cha Kumbukumbu  ya Mwalimu Nyerere tawi la Zanzibar anasema, madawati ya jinsia vyuoni yatakuza uelewa kuhusu masuala ya jinsia kwa kufanya kampeni mbalimbali.

Khulayta Hamad Shapandu kutoka Chuo Cha Abdulrahman Alsumait, anafafanua madawati ya jinsia, ni taasisi muhimu vyuoni kwani wanafunzi watapata sehemu ya utatuzi wa changamoto za  kijinsia zinazowakabili, wakiwa vyuoni.

“Sasa tumepata sehemu za kukimbilia pale tunapopata changamoto za kijinsia tukiwa vyuoni, kwani madawati haya yanamuhakikishia mwanafunzi usalama wake, pamoja na haki zake zote za msingi,”anaeleza.



JE WAZAZI WA WANAFUNZI WANAYEPI? 

Asha Zuber Khalfan mkaazi wa Mbuguani Mkoani Pemba anasema, madawati  ya jinsia vyuoni, yamekuza imani kwa wazazi juu ya usalama na ustawi wa watoto wao, kwa kipindi chote wakiwa masomoni.

 ‘’Kwa sasa tunaamini kwamba watoto wetu wapo salama ikilinganishwa na miaka iliopita, kwani wamepata sehemu sahihi ya kupigania haki zao pindi, zikivunjwa kwa namna yeyote ile," anafafanua.

Ali Mohamed Makame mkaazi wa Mtambile Mkoani Pemba anasema, ni jambo muhimu, kuwepo kwa madawati ya jinsia vyuoni, kwani kutasaidia kuongeza ufanisi kwa wanafunzi.

"Ustawi wa wanafunzi unategemea usalama na utulivu uliopo katika mazingira yake anayojifunzia, na haya madawati yanamuhakikishia hilo, muda wote jambo linalochochea ustawi wake kwa ujumla,"anafafanua.

 

 KUNAMAFANIKIO YEPI KUTOKA KWA MADAWATI HAYO?

Aisha Sunnah Haji Mjumbe wa dawati la jinsia Chuo kikuu Cha Zanzibar anasema, dawati limefanikiwa kutoa  uelewa kwa wanafunzi, juu ya masuala ya udhalilishaji pamoja na athari zake kwa mtu mwanafunzi mmoja mmoja na taifa kwa jumla.

Anaeleza kuwa, kwamba watendaji wa dawati la jinsia Chuoni hapo wamekua wakichukua jitihada mbali mbali, katika kuhakikisha kila mtu anauelewa tosha, juu ya udhalilishaji na ukatili wa jinsia.

"Sisi kama watendaji wa dawati, tumefanikiwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo hiki, juu ya athari za udhalilishaji, na lengo mahususi la kuwepo kwa haya madawati na kwasasa wengi wanauelewa," anaeleza.

 

KUNA CHANGAMOTO ZIPI KATIKA UENDESHAJI WA MADAWATI HAYA?

Ramadhan Mohamed Hassan ambae ni Mwanasaikolojia kutoka dawati la jinsia la Chuo kikuu Cha Zanzibar anasema, pamoja na kufanikiwa kufikisha elimu, bado  wanafunzi wengi hasa wakiume hawayatumii ipasavyo.

Anasema mara nyingi wanafunzi wa kiume, huamini kwamba madawati ya jinsia yapo kwa ajili ya wanawake pekee, na ni vigumu kwao kuyatumia, jambo linalorejesha nyumba mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji.

Said Suleiman Ali Mratibu wa dawati la jinsia la Chuo kikuu Cha Zanzibar anasema, hakuna ushirikiano wa kutosha baina ya watendaji wa dawati na mashahidi wa kesi mbali mbali zinazoripotiwa.

Anaona baadhi ya watu wenye ushahidi mzuri wa  malalamiko yalioripotiwa, wanakua wazito katika kutoa ushirikiano, jambo linaloathiri utendaji wa madawati hayo.

" Mara nyingi baadhi ya watu wenye ushahidi wa kutosha juu ya malalamiko yalioripotiwa, katika dawati wanakataa kushirikiana nasi, hili linaathiri sana utendaji wa dawati," anasema. 



WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM INASEMAJE?


Amoun Mpanju Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake  na Makundi Maalum anafafanua kwamba ni wajibu wa Vyuo Vikuu vyote na vya Kati, ni kuhakikisha wameunda madawati ya jinsia, ili kutoa wahitimu waliofuzu bila kuathiriwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Ni wajibu wa vyuo vikuu vyote nchini kuhakikisha wameunda madawati ya jinsia yatakayotumiwa na wanafunzi, ili kutoa wahitimu waliofuzu bila kuathiriwa na vitendo hivyo,’’anafafanua.

MITANDAO YA KIJAMII IMERIPOTI NINI?

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limeeleza kuwa idada kubwa ya wanafunzi ulimwenguni hukumbana na vitendo vya udhalilishaji na ukatili wanapokua vyuoni.

UNESCO katika utafiti wake iligundua kwamba, nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto sawa kuhusu udhalilishaji katika vyuo vikuu, na kueleza kwamba asiilimia 30 ya wanafunzi huripoti matukio ya udhalilishaji wakiwa vyuoni.

Hata hivyo, Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Michigan mwaka 2020 nchini Marekani ulibaini kuwa, karibu asilimia 25 ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliripoti kuwa, wamewahi kukumbana na udhalilishaji wa kijinsia, wakiwa vyuoni.

Aidha UNESCO imetahadharisha kwamba, iwapo hatua za haraka hazijachukuliwa kudhibiti hili, kunahatari ya ongezeko ya matendo ya udhalilishaji vyuo vikuu duniani kote.

JE WADAU MBALI MBALI  WANAMAONI GANI?

Nunu Issa Juma Makamu wa Rais Chuo Kikuu Cha Zanzibar anasema, ni vyema kwa wanafunzi kuyatumia madawati ya jinsia yaliomo vyuoni mwao,  ili kupunguza matendo ya udhalilishaji yanayowakabili wakiwa vyuoni.

Said Suleiman Ali Mkufunzi Chuo kikuu cha Zanzibar anasema kwamba, ni vizuri kwa wanafunzi kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kutoa fursa, kwa waalimu kutoa haki sawa kwa kila mwanafunzi bila kikwazo chochote.

Dkt. Lilian Macha Mratibu dawati la jinsia Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) anasema, ni vyema kwa madawati yote kufuata majukumu yao kwa usahihi ili kuepusha migogoro katika jamii

Nae  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe anasema Wizara ilishatoa muongozo wa kuanzisha wadawati ya jinsia, katika kila chuo na itahakikisha miongozo hiyo inafanyiwa kazi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima anasema, wizara iliandaa muongozo na kuratibu uanzishwaji wa madawati hayo, kwa lengo la kuweka mfumo imara wa kushughulikia masuala la unyanyasaji wa kingono vyuoni.

 

                                MWISHO

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...