Skip to main content

CHINA: WAANDISHI WA HABARI AFRIKA SAIDIENI KUKUZA UCHUMI

 



ZUHURA JUMA NA HAJI NASSOR, BEIJING@@@@

WAANDISHI wa habari wa nchi za Afrika, wametakiwa kuendelea kujifunza lugha mbali mbali, ili kusaidia kukuza uchumi katika mataifa yao.

Akifungua mafunzo ya siku 20 katika Ukumbi wa Hoteli ya RoyalLink ZiYu, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (CICG) Han Likiang alisema kuwa, kujua lugha mbali mbali ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo kuna haja kwa wanahabari kujifuza zaidi.

Alisema kuwa, ili uchumi ukue unahitaji mambo mbali mbali ikiwemo waandishi wa habari kujifunza lugha ambazo zitawasaidia kuandaa makala, vipindi na habari zenye tija hususan zinazogusa viashiria vya ukuaji wa uchumi wa ndani.

‘’Watakapotumia lugha mbali bali itawasaidia kuwahabarisha watu wengi duniani ambao wanaweza kuvutia hata wawekezaji na wageni, ambayo ni miongoni mwa kukuza uchumi wa ndani,’’ alisema.

Akizungumzia umuhimu wa CICG kuandaa mafunzo hayo ni kuendeleza uhusiano wa kimataifa wa china na mataifa mengine ya Afrika kwa lengo kubadilishana uzoefu wa kisera za kiuchumi miongozi mwa mataifa hayo.

‘’Mafunzo haya yatasaida sana kuendelea kukuza ushurikiano kwa mataifa ya Afrika, kwani watatembelea sehemu mbali mbali ambazo zitawasaidia kutangaza fursa zilizopo katika nchi hii,’’ alisema.

Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo ya kuwaleta pamoja washiriki wa mataifa mbali mbali, CICG lilikuwa na utamaduni wa kuwafuata waandishi katika mataifa yao.

‘’Lengo la kuwaweka pamoja ni kuona kwamba tunakutana na kujuana, jambo ambalo litasaidia kufanya kazi zetu kwa ushirikiano, huku tukiamini kwamba ni sehemu ya juhudi ya kukuza uchumi katika nchi zetu,’’ alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya kimataifa kutoka Shirika la CICG Feng Yin alieleza kuwa, mafunzo hayo ni fursa pekee kwa waandishi wa habari katika kukuza uchumi wa nchi yao, hivyo wanapaswa kuchukua juhudi za makusudi kuhakikisha nchi inapata maendeleo.

‘’Watakapoandika habari mbali mbali zitakazosaidia kukuza uchumi na nchi itapata maendeleo kwa sababu wananchi wanaamini sana vyombo vya habari,’’ alisema.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, mwandishi wa habari kutoka nchini Zambia, Emeldah Libaga alisema, mafunzo hayo ni muhimu kwao katika kuongeza uhusiano wa kutambua sera za kiuchumi za China ambazo zitasaidia kutanua wigo katika mataifa yao.

‘’Tunalishukuru sana Shirika hili kwa kutuweka pamoja na kutupa mafunzo, hii itatusaidia sana kuongeza uelewa wa masuala mbali mbali ya kiuchumi,’’ alifafanua.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na CICG kwa ufadhili wa Wizara ya Fedha ya China, ambalo limeanzishwa mwaka 1949 yamewashirikisha waandishi kutoka mataifa kadhaa ikiwemo Tanzania Zanzibar, Zambia, Gambia, Kenya, Gana na wenyeji wa China.

MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...