NA HAJI NASSOR, BEIJING@@@@
NI wastani wa saa 1:45 kwa mwendo wa gari isiyo kuwa ya umma, kutoka katikati ya jiji la Beijing, hadi iliko milima hiyo.
Milima hiyo, kwa hakika ni sawa na ile inayooko baadhi ya mikoa ya Tanzania bara, mfano mzuri ni Mwanza.
Maana imejengwa kwa mawe (majabali makubwa), ikiwa imezungurikia nje kidogo ya Beijing, na hata ardhi yake ikiwa ni mfumo wa mawe.
Wataalamu wa kichina, waliona milima hiyo isibakie bure, maana kwa zaidi ya miaka 100, sasa tokea kuasisiwa imekuwa ni sehemu ya kutunisha mfuko wao wa pato la ndani.
Ni eneo lenye utulivu kiasi, likiwa limezungurukwa na milima ya asili, na kwa hakika ingekuwa vigumu kupitisha barabara, pingine kupata upande wa pili.
NAMNA MILIMA HIYO ILIVYOGEUZWA ENEO LA KITALII
Zipo zaidi ya mita 5,500 (sawa na umbali wa viwanjwa 55 vya mpira wa miguu), ambavyo zilianza kujengwa vidaraja kuanzia chini.
Tunaelezwa kuwa, ujenzi huo ulijengwa kwa matofali maalum ya mawe, kwa mtindo wa kama vidaraja na kushukia ama kupandia mlima.
Pembezoni mwake, mumewekwa ukuta ulioshikamana na vyuma vizito, ili kumuhakikishai usalama mpanda mlima huo, baada ya kulipa wastani wa shilingi 5,000 kwa fedha ya Tanzania.
Unakisiwa kuwa, upana wake ni kati ya mita 4 hadi 5, baadhi ya maeneo yamenyanyuka kati ya mita 7.8 hadi mita 14 kwa nje, kulikoshikamana na ardhi ya mawe.
Namna ya upandaji wa vidaraja hivyo, unaweza kupumzika pasipokuwa na kibanda, kadiri utakavyopenda, ingwa kila wastani wa urefu wa viwanja viwili vya mpira wa miguu (mita 200), vipo vibanda vya kumpunzikia.
Ijapokuwa huzuiliki ikiwa afya ya kuanza mwanzo na kumalizia mwisho huna, lakini iwapo utafikia mwisho unakabidhiwa nishani maalum, yenye mfano wa dhahabu na wahusika.
Kumbuka, ushahidi wa kuanza mwanzo na kumaliza, kwa sasa unachungwa na ulinzi wa kamera maalum, ambazo zimeunganishwa, na kurahisisha kumuona kila mmoja.
Hapo wageni kutoka mataifa mbali mbali na hata wenyeji hufurika kwa wingi, kupanda ukuta huo, ambao maarufu huitwa ‘great wall’.
Kwa kawaida, wenyeji wetu wanasema idadi ya watu huongezeka mara dufu kwa siku za baridi, ili watu kuzalisha joto la mwili, hasa waakati wa kupanda, kwa kule kutumia nguvu za kunyanyua miguu.
‘’Na hata wanafunzi, wazee wenye magonjwa ya miguu, maradhi ya kupumua na wageni hata utawaona wanatembelea ukuta huu, ambao kwetu sisi wachina unahistoria yake,’’anasema muuza kofia Yeu Is Kwu.
Anasema, msimu wa baradi hujipatia fedha nyingi hadi Yuwan 2,000 kwa siku, baada ya kuuza kofia zenye jina na nembo ya China, kwa wageni na wenyeji.
‘’Ukipanda mlima huu, inapendeza uwe na kofia na ujiti maalum ‘mop’ ili kupata kasi ya kupanda na kupata kisaidizi wakati wa kushuka,’’anaeleza.
Muuza chai na mahindi eneo hilo la chini ya ukuta huo, Yu Usy Sun, anasema hakuna siku wanaofika eneo hilo watu wasizidi 80,000 wakipanda ukuta huo.
Anasema wageni, wazee na wanafunzi ndio wamekuwa hawaadimiki eneo hilo, wakija kijifunza mambo kadhaa, ingawa kwa wazee ni uchangamshaji wa mwili.
Mwananchi aliyetembelea eneo jilo Li Tes Yu (55), akizungumza kwa msaada wa mtoto wake kwa lugha ya kiingereza, anasema amekuwa na shida ya kupumua kwa mwezi mmoja sasa.
‘’Hapa sikuja kama mtalii wa ndani, nimekuja kutoka Shanghai kutimiza ushauri wa kitabibu wa kufanya mazoezi na kutembelea milimani,’’anaeleza.
‘’Wewe ni nani, ni mwandishi wa habari, umetoka wapi, Tanzania, mbona upo hapa, ni kutembelea kama mtaalii, aliniuliza, ingawa yeye akasema ni kufuata tiba.
Kumbe maeneo kadhaa ya China yako tambarare, na ndio maana, wanaotaka kufanya mazoezi kwa nguvu na kasi wapo wanofuata milima hiyo.
Mwenyeji wetu tuliyetoka nae katikakati ya jiji la Beijing Magic, anasema kila mmoja, hufika kwenye milima hiyo kwa azma yake mwenyewe.
Anasema, wageni ni kwa ajili ya kutembelea kwa mara ya kwanza au ya pili, ingawa wanafunzi kusoma kwa vitendo na wapo baadhi ya wazee na wagonjwa kutekeleza ushauri wa daktari.
Mc. John Gabreil kutoka Natharland, anasema hii ni mara yake ya kwanza, kufika katika eneo hilo, ambalo awali alikuwa analisoma kupitia mtandaoni pekee.
‘Ni eneo zuri ambalo wenzetu wa serikali ya China, wamelitumia na sasa limekuwa likiingia kwenye rikodi ya dunia kiutalii, ingawa ni jambo la kutengeneza,’’anasema.
KUNDI LA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA AFRIKA
Momodou Jow kutoka Gambia anasema, ni eneo la kujifunza kwa mataifa mingine ya Afrika, namna ya kutumia malighafi kuchochea uchumi.
Mwandishi Aggrey Mutambo wa Kenya, anasema ni eneo zuri lililotumia utaalamu wa hali ya juu, namna milima ilivyosarifiwa na kuwa sehemu ya utalii.
‘’Milima ipo kila mahali na hasa ndani ya mataifa ya Afrika, lakini uwezo mdogo wa fedha za uwekezaji na utaalamu hafifu, imebakia kama ilivyo,’’anafafanua.
‘’Kwenye mataifa ya Afrika milima ipo, lakini ni yenye kuporomoka, maana maumbile ya ardhi zenyewe ni mchanga laini, ingawa kwa hapa jiwe limetawala,’’anasema.
Mtaalamu wa sayansi ya jamii kutoka taasisi ya Magharibi mwa bara la Asia na Afrika, anayefaniya kazi zake nchini China Professa: He Wenping, anasema ukuta huo juu ya milima, ni sehemu ya kuimarisha historia ya ukombozi wa China.
Inawezakana misaada ambayo mataifa ya Afrika wameshayapokea kutoka China, yenye thamani ya dola bilion 615.8 kuazia mwaka 1950 hadi mwaka 2018, ilichangiwa na pato katika milima hiyo pia.
Maana ukombozi wa China chini ya chama tawala cha CPC, kwa wakti huo wa kuanzia mwaka 1949 chini ya Chamen Mao, ilikuwa inabuni kila mbinu kuhakikisha, inajiendesha.
Kwani China ilikuwepo tokea mwaka 2070BC, (kabla ya ukiristo), huku chama cha kikomonisti ‘CPC’ kikiwa ndio mkombozi wa wananchi tokea kilipoasisiwa zaidi ya miaka 100 sasa.
Katika ziara ya eneo hilo, waandishi wa habari wa redio, tv, mitandao ya kijamii na magazeti waliopo nchini China, walitembelea milima hiyo, kama sehemu ya mafunzo ya siku 21.
Ni waandishi wa kutoka Gambia, Zambia, Kenya, Ethiopia, Tanzania Zanzibar na wenyeji China, ambao pia walishatembelea, makumbusho ya chama cha CPC, dawa asili, ofisi za star times, ofisi za uchapishaji wa gazeti la China-Aftika na dawa asili.
Mwisho
Comments
Post a Comment