Skip to main content

''WATOTO WENYE MATATIZO YA MACHO WAWAHISHWE HOSPITALINI MAPEMA''

 



Na Joyce Joliga, Songea@@@@

Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wenye matatizo ya  mtoto wa jicho wanayozaliwa nayo au yaliyotokana na majeraha ili kupata matibabu sahihi na  kumuwezesha ubongo kukua vizuri na kuona vizuri.

Rai hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) Dkt. Barnabas Mshangila kwenye kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho inayoendelea katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali ambayo inaratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Hellen Killer International la hapa nchini.

Dkt. Mshangila amesema kawaida mtoto anapokua anatakiwa macho yake yaone vizuri ili ubongo na wenyewe uweze kukua hivyo mtoto anapoumia  akiwa chini ya miaka (7) na asipopelekwa hospitali kufanyiwa upasuaji husababisha kutokuona vizuri ukubwani.

“Mtoto asipofanyiwa matibabu kwa wakati na anapofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho akiwa mtu mzima, jicho huwa halioni vizuri kwani mwanga unakuwa haujaingia wa kutosha na kufanya ubongo nao usikue, ushauri wangu ni vyema wazazi kuwapeleka kwenye vituo vya afya watoto kwa ajili ya uchunguzi pale mtoto anapopata majeraha kwani anaweweza asisikie maumivu". Amesema Dkt. Mshangila.

Kwa upande wa waliofanyiwa upasuaji Dkt. Mshangila amesema ni vyema wakafuata masharti wanayopatiwa ikiwemo kutokufanya kazi ngumu na kutokukaa sehemu yenye moshi pamoja na vumbi pia kuhudhuria kliniki na kuonana na wataalamu kwa tarehe walizopangiwa.

Aidha, amesema mtu aliyefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho tatizo hilo haliwezi kujirudia mara baada ya upasuaji ila wapo baadhi ya watu huwa inaweka ukungu kwenye sehemu ambayo inaachwa wakati wanaweka lenzi ya mwanzo.

"Kuna wachache inaweka ukungu kwa kuona jicho linafifia tena lakini inakua sio kama mtoto wa jicho la mwanzo na huwa labda baada ya miaka mitatu, akija hospitali upasuaji wake huwa sio mkubwa na hurudi kuona tena". Amesema.



Hata hivyo amewatoa hofu baada ya watu ambao wana matatizo ya mtoto wa jicho ambao hudhani akifanyiwa upasuaji hawawezi kuona tena na kuwasihi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupatiwa huduma hizo ambazo zimesogezwa karibu na makazi yao.

Dkt. Mshangila ameongeza kuwa yapo matatizo mengine yanayosababisha upofu ambao hautibiki hivyo kama wataalamu kabla ya upasuaji wa mtoto wa jicho huwafanyia uchunguzi kama kuna shida nyingine kama presha ya macho, huwashauri wajue endapo watafanyiwa upasuaji hawatoona vizuri.

Mtoto wa jicho ni tatizo linalosababisha ukungu kwenye kioo (lenzi) ambapo mboni ya jicho hubadilika na kuwa jeupe na hivyo upasuaji hufanyika ili kutoa  lenzi yenye ukungu na kuweka lenzi isiyo na ukungu na visababishi vyake ni mabadiliko ya mwili yanayoambatana na umri.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch