NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KATIBU Mkuu wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amewakumbusha wakuu wa vitengo
vya wizara hiyo Pemba, kuendelea kufanyakazi kwa pamoja, kwani huo ndio msingi
wa mafanikio.
Alisema, changamoto
ya udogo wa bajeti ya kutosha, uhaba wa watendaji katika vitengo vyao, pamoja
na kikwazo cha usafiri, vinaweza kupata ufumbuzi, ikiwa wataendelea kufanyakazi
kwa ushirikiano.
Katibu Mkuu
huyo, aliyasema hayo Gombani Chake chake, wakati akisalimiana na wakuu wa
vitendo vya wziara hiyo, alipokuwa kisiwani Pemba, kwa mapunziko ya sikukuu.
Alieleza
kuwa, umoja na mshikamano ndio suluhisho la changamoto kadhaa zinazowakabili,
na kinyume chake, wanaweza kuyumba kiutendaji.
Alifahamisha
kuwa, kama viongozi wakuu wa wizara hiyo wanashirikiana kwa karibu, ni vyema mwenendo
huo wakauiga, kwani unaweza kuwapandisha juu kiutendaji.
‘’Niwalazimishe
watendaji wenzangu, kuwa mkitaka kufanikiwa pamoja na changamoto kadhaa, jambo
la msingi na la lazima ni kuwa wamoja,’’alishauri.
Akizungumzia
ufanisi wa wizara hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi, alisema karibuni
wanaopata maudhui kupitia ving’amuzi vya Z-MUX, watapata hata tv za nchi
jirani.
‘’Wizara
umeshajipanga kuimarisha upatikanaji wa maudhui kupitia ving’amuzi vyetu, na
naamini kama mpango wetu utafanikiwa, tutaongeza idadi ya wateja,’’alifafanua.
Katika hatua
nyingine, Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Zanzibar Fatma Hamad Rajab, aliwasisitiza watendaji hao, kuzingatia stahiki za
wafanyakazi wao.
Alieleza
kuwa, suala la maslahi ya wafanyakazi liwekipaumbele cha kwanza katika utendaji
wao, kwani ndio wanaoweza kuinyanyua wizara kiutendaji.
‘’Sitoridhishwa
hata kidogo, kuona watendaji wa chini wanapelekewa mbele malipo ya stahiki zao,
lakini waratibu wanajilipa mwanzo, lazima tuwe waungwana,’’alifafanua.
Hata hivyo,
amepongeza wakuu hao wa maidara kwa kuonesha mshikamano wao katika utendaji wa
kazi za kila siku, jambo ambalo linampa moyo kwenye nafasi zao.
Mapema Kaimu
Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Khamis Massoud Khamis alisema, wamekuwa wakishirikiana vyema na
watendaji hao katika utendaji wao wa kila siku.
Kwa upande
wake Mkuu wa Idara ya Habari Melezo Pemba Jamila Abdalla Salim, alisema udogo wa
bajeti walionao, ni miongoni mwa changamoto zao.
‘’Gari yetu
kwa sasa inahitaji matengenezo ya haraka, na hasa kwa vile mwezi ujao kuna
shughuli ya kitaifa ya mbio za mwenge wa uhuru, lakini hata vifaa vyetu vya
sauti vimechoka,’’alilalamika.
Nae Mkuu wa
Idara ya Uchapaji Pemba, Kassim Hamad Nassor, alisema utamaduni huo wa Katibu Mkuu
wa kukutana na wakuu wa Idara, unazidisha uhai wao katika kufanikisha majukumu
yao ya kila siku.
Katibu mkuu
huyo wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab,
amekusudia kuendeleza utamaduni wa kuwa na vikao kila baada ya muda na wakuu wa
Idara, ili kusikiliza mafanikio na changamaoto zao.
Mwisho
Comments
Post a Comment