NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
MATUKIO
610 ya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, yameripotiwa kutokea Zanzibar, kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu ya mwaka 2021 na 2022,
taarifa za ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa
serikali Zanzibar, zinaeleza.
Kwa miezi ya Januari hadi Machi mwaka 2021, Ofisi hiyo
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Zanzibar, ilikusanya matukio 363, ingawa
kwa mwaka jana, katika kipindi hicho matukio hayo yaliripotiwa 247, upunguzu wa
matukio 116.
Takwimu hizo zinafafanua kuwa, kwa mwaka 2021 kwa miezi
mitatu ya mwanzo, mwezi ulioongoza ni mwezi wa Machi ulioripoti matukio 141,
ukifuatiwa na mwezi wa Januari matukio 122 na Febuari matukio 100.
Kwa mwaka 2022, mwezi uliokihiri kwa matukio mengi ni
mwezi Febuari, ulioripoti matukio 100, huku mwezi Machi ukiripoti matukio 82,
wakati mwezi wa Januari yakishuka kwa 17, na kuripoti matukio 65 pekee.
Taarifa hiyo ikeleza kuwa, mwezi wa Febuari kwa miaka
yote miwili, iliripoti matukio sawa ya 100 kwa wanawake na watoto kudhalilishwa
kwa Unguja na Pemba.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba Juma Saad Khamis, alisema moja
ya vyanzo vya matukio hayo ni mporomoko wa maadili, uliozoeleka ndani ya jamii.
‘‘Lakini hata kwa jamii, kutokuwa tayari kutoa ushahidi makamani, na
kusababisha kesi kufutwa, huchangia matukio hayo kuendelea,’’alieleza.
Kwa upande wake, Hakimu wa mahakama amaalum ya kupambana na makosa ya
udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba Muumini Ali Juma, alisema chanzo ni wazazi
kuacha malezi ya pamoja.
Mwanasheria dhamana wa Mahakama kuu Zanzibar Ali Rajab, anasema
kuongezeka kwa matukio hayo, ni jamii kukosa elimu ya kisaikolojia, na kutoyapa
uzito matukio hayo yapotokezea.
Mzazi Saumu Haji Said wa Machomane anasema, kutotumika kwa sheria kama
zilivyoandikwa, baada ya mshitakiwa wa udhalilishaji kutiwa hatiani, ndio
sababu ya kuongezeka.
‘’Wahalifu hawana woga wanajua kuwa, atafungwa miaka saba, 10 au 20 na
atatumikia nusu yake, baada ya muda anatoka chuo cha mafunzo,’’anasema.
Wakili wa kujitegemea Pemba Zahran Mohamed Yussuf, anaona chanzo ni
harufu ya rushwa katika baadhi ya vyombo vya sheria, kunakopelekea watu
kuachiwa huru.
Mtoto Hidaya Haji Mkame wa Mizingani amesema chanzo cha matukio hayo, ni
wazazi kutowajibishwa kisheria, ikiwa tukio la udhalilishaji wa mtoto wake kuna
uzembe.
Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’-Zanzibar
Dk. Mzuri Issa Ali, anasema moja ya athari ya matendo hayo, ni kupata madhara
ya kiakili kwa muathiri.
‘’Mtu aliyedhalilishwa na hasa mtoto, hata hamu ya kuendelea na masomo
hana, kujichanganya na wenzake huondoka, maana kila wakati anajihisi
mpweke,’’anasema.
Aziza Iddi Ali anasema, ni kupungua ufahamu wake hasa kwa wale walioko
masomoni, na wakati mwengine hadi kupekekea utoro.
Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC' Harusi Miraji
Mpatani, anasema athari nyinge ni kupewa majina mabaya na wenzake.
Mtoto Khamisuu Is-haka Ngwali wa Msingi Mkoani, anasema hata kusemwa
ovyo na wenzake, moja ya athari, ambayo mtoto aliyebakwa anaipata.
Daktari Mohamed Ali Jape anasema, kupoteza haiba ya viungo vya mwili,
ndio athari kubwa inayowaumiza watoto hasa kutokana na umri wao, kutokuwa
tayari kupokea tendo hilo.
Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Mshibe Ali Bakari, amesema ni kwa
washtakiwa kupewa adhabu ndogo lakini yenye kufunza, inaweza kusaidia.
Mkurugenzi wa Mastaka Zanzibar Mgeni Jailan Jecha, alipendekeza kuwa,
elimu ya kiroho inahatajika kwa jamii, ili kumuogopa Muumba.
Mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto Tatu Abdallah Msellem,
anasema kama kutakuwa na adhabu kali kwa wakosaji, wengine wataogopa.
Mtoto mwenye ulemavu Maimuna Himid Mkombe wa Uwandani Chake chake,
anasema kama adhabu ya kifungo cha maisha itatolewa, itakuwa dawa.
Sheikh Said Ahmad kutoka Ofisi ya Mufti Pemba na Mchungaji Benjamin
Kissanga wanasema, elimu bado inahitaji kwa waumini, ili kujua athari ya
wanayofanya kidini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi, anasema kama sheria zikifanyiwa marekebisho, zile zinazokwaza, inaweza
kusaidia watu kujenga hofu.
Mwisho
Comments
Post a Comment