NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
ZANZIBAR kama ilivyo eneo jingine
lolote ulimwenguni, nayo inavyo vyombo vya habari, ambavyo maudhui yake ni sawa
na vile vya mataifa mengine.
Nikukumbushe
tu kuwa, kazi za msingi za vyombo vya habari ni kuelemisha, kuburudisha na kuhabarisha
ingawa kwa pia ni kukosoa, kupongeza na kuhoji.
Kazi hii
hasa ni haki ya kikatiba, katika mataifa mbali mbali, kwa mfano Zanzibar katiba
yake ya mwaka 1984 kifungu cha 18 na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977, ibara 18 imeelezea haki hii.
Kama hivyo
ndivyo, unaweza kushangaa kuwa suala la kutoa, kupata na kusambaaza habari ni
haki ya kikatiba, sasa iweje kutungwe sheria yenye vifungu au maneno, yenye
ukakasi kwa waandishi wa habari.
SHERIA YA TUME YA UTANGAAZAJI
ZANZIBAR NO 7 YA MWAKA 1997
Sheria hii
ambayo sasa inatimiza umri wa miaka 26, tokea pele ilipotiwa saini na Rais wa
wakati huo wa Zanzibar Dk. Salmin Amour Juma, licha ya kufanyiwamarekebisho.
Kwa hakika,
lengo kuu la sheria hii, ni kuongoza vyombo vya habari Zanzibar ikiwemo redio,
televisheni na vile vyombo vya kisasa vyenye kurusha matangaazo yao, kupitia
njia ya mtandaoni.
Sheria hii,
kwenye sehemu yake ya kwanza, imeundwa na vifungu vitatu, kwani kile cha nne (4),
kimefutwa na kati ya hivyo kimoja kinatoa jina la sheria na maana ya maneno,
yaliomo kwenye sheria hiyo.
Sehemu ya
pili ya sheria hii, imeundwa na vifungu kuanzia cha tano (5) hadi cha 10, na
kubwa zaidi lililopo ni pamoja na uanzishwaji wa Tume ya Utangaazaji Zanzibar
‘TUZ’.
Kwenye sehemu
ya tatu ya sheria, imeundwa na vifungu vinne (4) kuanzia cha 11 hadi cha 14, ni
eneo lililotajwa zuio la utangaazaji, usiokuwa na leseni, masharti ya kuomba,
utoaji wake na kiwango cha matumizi na kuongeza muda.
Sehemu ya
nne (4), inaangalia uratibu na usimamizi wa utangaazaji, huku sehemu ya tano,
ikundwa na vifungu saba (7) na ikiangalia zaidi amsuala kifedha.
Sehemu ya 6 ya
sheria hii ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997, imeundwa na vifungu
vitano (5) kuanzia kile cha 26 hadi 30, ambacho, kinaelezea kufutwa kwa sheria
nambari 25 ya mwaka 1961.
MANENO YENYE UKAKASI NDANI YA SHERIA
HII
Wadau wa
habari kila siku, wamekuwa wakirejea maneno yao, wakisema kuwa, neno
hutafsiriwa kama lilivyo kwenye maandishi, na wengine wakaenda mbali zaidi
kuwa, mtumiaji sio mtunzi.
Kwenye
kifungu cha 7 (1) (d) lipo neno lililounda sentensi ‘kudhibiti shughuli za
watangaazaji na maadili yao ya utangaazaji pamoja na wafanyabiashara wa vifaa
vya utangaaji’.
Mdau wa
habari Ali Khamis Haji wa Madungu Chake chake, anasema neno ‘kudhibiti’
linatoa tafsiri ya ukakasi, kwamba suala la kudhiti sio neno rafiki.
‘’Neno
kudhibiti linaashiria namna ya kushika, kuweka chini ya ulinzi au wakati
mwengine mtu anayefanyakazi chini ya uangalizi fulani, wa tasisi
fulani,’’anasema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri
Issa Ali, anasema kwenye sheria za habari, neno ‘kudbiti’ linaleta ukakasi
hasa kuelekea uhuru kamili wa habari.
Mchambuzi wa
masuala ya sheria za habari Zanzibar Imane Duwe, anasema wakati wa Zanzibar
kuwa na sheria mpya ndio huu, na wala kusiwe na maneno kwenye sheria,
yanayoashiria uhalifu.
Hata kwenye
kifungu hicho (h) lipo neno ‘kutoa maelekezo yoyote kwa biashara ya
utangaazaji ambayo kwa maoni yake, itaona inafaa’ kwa mpewa leseni.
Neno kutoa ‘maelekez’o
na jengine lile kwa ‘maoni yake itaona inafaa’, haya yamewaibua
wadau wa habari na waandishi wa habari wakisema, yanaleta ukakasi.
Na ndio
maana mwanasheria wa Shirika la Magazeti ya serikali Juma Khamis Juma, anasema
neno moja tu lenye silabi mbili, likitafsiriwa linaweza kusababisha madhara.
‘’Neno ‘maelekezo’
au kwa ‘maoni’ ni hatari kuwemo kwenye maelezo ya sheria, au sentensi
inayotoa amri ya jambo, hivyo kuelekea uhuru kamili wa habari, haya
yanaukakasi,’’anasema.
Hata mdau wa
habari ambae ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani kwa sasa Khatib Juma Mjaja, anasema
sheria za habari, hazitakiwi kutumika na maneno yenya tafsiri zaidi ya moja.
‘’Ukisema ‘akiona
inafaa’, kwa ‘maoni yake’, akihisi, atatoa maelekezo
au akisema ‘akiamua’, haya yote yanapingana na katiba na hasa kifungu cha
18,’’anasema.
Kifungu
chengeni ni kile cha 15 (2) kuna msamiati kuwa ‘Tume inaweza kila baada ya muda
na kwa idhini ya Waziri kwa tangaazo lililochapishwa katika gazeti rasmi,
kutaja masharti hayo yatakayotekeleza na mpewa leseni’
Wadau
wanassema, neno ‘tume inaweza’ haliaendani na wakati uliopo wa zama za
ushirikishwaji na ushiriki na hasa Zanzibar, ikiwa ni nchi inayofuata mfumo wa
demokrasia.
Mwandishi
Salim Said Salim anasema, neno ‘tume inaweza’, sio sahihi kuwepo
kwenye vifungu hasa ambavyo vinasimamia sheria ya habari hapa Zanzibar.
Mratibu wa
Internews Zanzibar Zaina Mzee, anasema wakati umefika sasa Zanzibar kuwa na
sheria bora na rafiki na yenye maneno yanayoimarisha uhuru wa habari.
‘’Inawezekana
leo tunae Katib Mtendaji au waziri mzuri wa habari na pengine asikitumie
kifungu hicho vibaya, lakini je kesho na keshokutwa tutakaempata, hatoyatumia
atakavyo maneno hayo,’’anahoji.
Ndio maana
anasema, ili kuhakikisha Zanzibar kuna kuwa na sheria bora na rafiki, Internews
imekuwa ikiwakutanisha wadau, waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari, ili
kujadili kwa pamoja.
‘’Hamu ya
Internews siku moja ni kwa Zanzibar kuwa na sheria bora, rafiki n ainayokuza na
kuendeleza uhuru wa habari, ili wananchi wawe na maamuzi sahihi,’’anasema.
Anaamini kukiwepo
kwa vyombo vya habari makini, waandishi wakaandika habari makini, zikahaririwa
kwa umakini na wananchi watafanya maamuzi makini.
Mwandishi wa
ZBC Khadija Kombo anasema, maneno kama hayo yenye ukakasi, ndio yanayoashiria
shari baina ya sheria hizo na utendaji kazi wa vyombo vya habari.
Hata kifungu
cha 18 (1), kinachompa waziri uwezo wa ‘kukagua’
ingawa kwa kushirikiana na Tume, au mwengine wa wengine kwa ukaguzi au wakaguzi
kwa madhumini ya sheria hii.
Hapa neno ‘kukagua’,
halijakaa vyema kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari, wakisema kazi
ya habari haikaguliwi na hasa baada ya mpewa leseni kupewa leseni.
Kwa mfano
mwandishi wa mtandaoni Talib Ussi Hamad wa Unguja anasema, neno ‘kukagua’
lina ukakasi mkubwa kuelekea uhuru kamili wa habari.
‘’Kwani
isiwe pana neno kutembelea, kukukutana nao, kushauriana lakini suala la kuwepo
kwenye kifungu cha sheria neno kukagua, ni kama vile wakati wowote
akipenda,’’anaeleza.
Mwandishi
Berema Suleiman wa Zenj Fm redio, anasema maneno kama hayo na mengine
yanayofana nayo, yanaweza kutumika vibaya na waziri au mwengine atakaepewa
mamlaka.
‘’Kwa mfano
tunakumbuka wenzetu wa Cloud’s media walivamia usiku na aliyekuwa mkuu wa Mkoa,
kwa madai ya kukagua, na tuliona athari iliyojitokeza,’’anafafanua.
Kifungu
chengine chenye maneno yenye ukakasi na ukuaji wa wa uhuru wa habari ni cha 27
(1), ambapo waziri husika au mwengine aliyeidhinishwa, anaweza kutoa amri
kumtaka mpewa leseni, atangaaze jambo lolote ambalo kwa maoni ya Waziri, lina
maslahi kwa umma au uslama wa taifa.
Hapa wadau
wa habari wanasema, kifungu hicho kipo kishari shari zaidi, maana kimebainisha
uwezo wa Waziri, kumlazimisha mpewa leseni kutangaaza jambo ambalo anaona tu ni
kwa maslahi ya umma au usalama wa taifa.
WANANCHI
Omar Haji
Kassim na mwenzake Othman Omar Kombo wa Kambini kichokwe, wanasema waandishi
wasipokuwa huru, hata wananchi hawatokuwa huru, kufanya uamuzi sahihi.
Mratibu wa
Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Mashavu Juma Mabrouk anasema,
wanavitarajia mno vyombo vya habari, kuibua changamoto za jamii, na hilo
litawezekana ikiwa wako huru.
NINI ATHARI YAKE?
Moja wadau
wanasema, ni kuwafanya waandishi wa habari kufanyakazi kwa woga na nidhamu
iliyopindukia mipaka, huku ikieleweka kuwa, wao kazi yao ni kuitekeleza Katiba.
Mwandishi wa
Mwanahalisi mtandaoni Jabir Idrissa, anasema athari kubwa ni wawekezaji sekta
ya habari, kukosa hamu ya uwekezaji, na kundi kubwa kukosa ajira.
Miraji Manzi
Kae wa redio Jamii Makunduchi, anasema woga wa waandishi kukosa kufichua maovu,
wakati mwengine, hutokana na uwepo wa sheria kandamizi.
NINI KIFANYIKE?
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa Habari Zanzibar ‘ZPC’ Abdalla Mfaume, anasema moja ni
kuzisemea sheria na vifungu kandamizi, ili waandishi wa habari wafanyekazi zao
kama ilivyo, kwa makundi mengine.
Rahma
Suleiman wa Gazeti la Nipashe, anasema waandishi na wadau wa habari, waungane
kusindikiza mswada wa sheria habari Zanzibar ulipofikia, upelekwe hatua
nyingine.
Mchambuzi wa
sheria za habari Zanzibar Imane Duwe, anasema maneno kama ‘uwezo wa Mkurugenzi, Waziri,
akiona inafaa, akihisi, kwa maoni yake’ kwenye sheria mpya ya habari
yasitumike.
Mdhamini wa
Baraza la Habari Tanzania MCT-Zanzibar Shifaa Said Hassan, anasema chengine ni
kuharakishwa kwa mswaada wa sheria ya habari kufika barazani.
Mwisho
Comments
Post a Comment