TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Washindi wa tunzo za umahiri wa uandishi wa habari wa
takwimu za wanawake na uongozi
kujulikana leo usiku wa 25 Febuari, 2023.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) leo Jumamosi tarehe 25 Febuari, 2023 zimeandaa hafla ya utoaji tunzo maalum za umahiri wa uandishi wa habari za takwimu zinazohusu masuala ya wanawake na uongozi Zanzibar ambayo itafanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil – Kikwajuni kuanzia saa 1: 00 usiku.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi katika
hafla hiyo ambayo inategemewa kuhusisha zaidi ya watu 150.
Kauli mbiu ya tunzo hizo ni “KALAMU
YANGU MCHANGO WANGU KWA WANAWAKE”
na ina lengo la kuimarisha kada ya habari katika eneo mahsusi la takwimu
za wanawake hivyo kuwashajiisha
waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuandika kwa weledi na umahiri masuala ya wanawake na uongozi.
Waandishi wa habari ni watu muhimu katika kuleta mabadiliko, hivyo wana nafasi kubwa ya kushajihisha kufikiwa kwa usawa wa
kijinsia katika vyombo vya maamuzi ikiwa wataandika habari za takwimu na uchambuzi mfululizo.
Kazi zilizopitiwa zilikuwa
ni 421 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio, televisheni
pamoja mitandao ya kijamii.
Kazi zilizowasilishwa zilitakiwa ziwe zimetolewa au kurushwa hewani
kuanzia Januari 2022 hadi Disemba 31, 2022 na ziwe zimezingatia
umahiri wa uandishi na uandaaji bora wa vipindi na makala ikiwemo ubunifu, vyanzo vingi na tofauti vya habari,
zenye kuweza kuleta mabadiliko, kutoa suluhisho pamoja na kupanga kwa umakini
takwimu za wanawake na
uongozi.
Jumla ya washindi 12 wanatarajiwa kutunukiwa zawadi katika
usiku huo maalum; mshindi wa kwanza,
wa pili na wa tatu baada ya kupitiwa na jopo la majaji watano wataalamu wa
masuala mbali mbali yakiwemo, habari
za magazeti, kielektroniki, mitandao ya kijamii, masuala ya wanawake na sheria.
Shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbali mbali
kutoka katika taasisi za Serikali, habari, vyuo vikuu, vyama vya
siasa, asasi za kiraia na wadau wa masuala
ya wanawake.
Kazi za washindi zitatangazwa na kuoneshwa kwa lengo la
kuwahamasisha waandishi na wadau wa
habari kujifunza na kutafuta njia za
kuimarisha kazi za wanwake na uongozi.
Hii ni mara ya pili kufanyika kwa tuzo hizo za takwimu za
wanawake na uongozi chini ya mradi wa
Kuinua Wanawawake katika Uongozi
(SWIL) Zanziba kwa mashirikiano na Ubalozi wa
Norway nchini Tanzania.
Imetolewa na
DK. Mzuri Issa Ali
Mkurugenzi TAMW/ZANZIBAR
Comments
Post a Comment