Skip to main content

Posts

AWENA SALIM KOMBO: MWANAMKE ANAEPAMBANIA UONGOZI KWENYE JIMBO LAKE

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA   "SIKATI tamaa ipo siku nitafanikiwa lengo langu nililolikusudia kwa sababu kila kitu kimepangwa kwa muda maalumu, hivyo naamini bado wangu haujafika"   Sio maneno ya mtu mwengine bali ni Awena Salim Kombo mwenye umri wa miaka 50 mkaazi wa shehia ya Kangagani Wadi ya Kiuyu, Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Pemba.   Awena ni mwanamke shupavu mwenye ndoto ya kuwa kiongozi tangu akiwa kijana mdogo, na ndipo mwaka 1990 alipoamua kujiunga kwenye chama cha Mapinduzi CCM, ili kusudi apate nafasi ya kuwa kiongozi.   Lengo lake la kusaka uongozi ni kutaka kusaidia jamii kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili.   "Hivi sasa baadhi ya wanajamii wenye matatizo hunifuata kutaka msaada, hivyo wakati mwengine nashindwa kutokana na hali yangu kutomudu" anaeleza.   Mwaka 2017 Awena alianza kupata nafasi za uongozi katika chama chake, ambapo alijiona tayari anaenda kutimiza ndoto zake ...

BIZUME: MWANAMKE ANAEPAMBANA KUFIKIA TAIFA KIUONGOZI

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA    BIZUME Haji Zume, mkaazi wa shehia ya Kinyasini Jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, ni miongoni mwa wanawake mashuhuri wenye nia ya kufika mbali kiuongozi.   Ingawa matarajio yake yeye mpaka sasa, ni kugombea nafasi za ndani ya chama tu kuanzia tawi hadi Taifa, na sio Jimboni kwa kile anachodai kwamba ni lazima kwanza ushikilie nafasi hizo ili uwe imara zaidi.   Atapojijenga zaidi kwa nafasi za ndani ya chama, hapo ndipo ataanza kutafuta njia ya kusonga mbele kwani, huwezi tu kufika huko ikiwa hukuanza nafasi za chini.   "Nataka na mimi nifikie kugombea Uwakilishi na Ubunge katika Jimbo lakini, huwezi kufika huko ikiwa bado kwenye chama hujashika nafasi yeyote," anasema Bizume.   Lengo la mama huyo kugombea nafasi hizo, ni kuhakikisha anajijengea uwezo zaidi wa kiuongozi, kujenga mahusiano mazuri na wanachama, pamoja na kukubalika kwenye chama chake.   Anasema, hiyo itampa fursa ya kus...

NJUMA ALI JUMA: MJASIRIAMALI ANAEJIAMINISHA KIMAISHA SASA, AWAPA WOSIA WENZAKE

NA TATU MAKAME. ZANZIBAR@@@ UNAPOZUNGUMZIA ujasiri na ucheshi alionao mwanamke utagundua kuwa ni kiungo muhimu katika jamii hasa kwenye nafasi za uongozi. Aidha wanawake wenye uthubutu wa kufanya harakati za jamii wamekuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi jamii kufanya harakati za maisha ili kuendeleza maisha yao katika jamii. Hata hivyo serikali na taasisi binafsi nazo zimekuwa mfano mkubwa kuwahamasisha wananwake kuingia kwenye nafasi za uongozi baada ya kuwapatia mafunzo ya kuwania nafasi za uongozi ili kuachana na mfumo dume wa kuwa mwanamke uwezo wake mdogo kuwa kiongozi. Hata hivyo Mradi wa SWIL unaoimarisha uongozi wa wanawake unaoendeshwa na Chama cha waandishi wa habari Tanzania Tamwa ZNZ nao umekuwa mfano bora wa kuwahamasisha wanawake kuingia kwenye nafasi za uongozi na kuwa kioo kwa jamii. Kwa mujibu wa Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA) Imane Duwe alisema kiongozi sio lazima awe mwanasiasa au mtu maarufu kama wengine. Hata hivyo alisema wanawake wanaoing...