NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
TIMU ya
soka ya Nadhaf ya Wambaa, imetupwa nje kwa matuta na timu ya Mkaa, kwenye michauano
ya kuwania kombe la Mwakilishi wa Jimbo la Chambani, baada ya kutoshana nguvu
kwenye dakika 90.
Mchezo huo
uliovuta hisia za wingi, ulikuwa wa ufunguzi, ulipigwa uwanja wa Wambaa, ambapo
wanacheza kwa mtindo wa mtoano, na bingwa ataondoka na kitita cha shilingi
milioni 1, kutokwa kwa Mwakilishi huyo.
Wakati wanaume
hao wakishindwa kutambiana kwenye dakika za kawaida, hatua ya kupigiana mikaju
ya penalti, ilifanyika na timu ya Nadhaf, ikipoteza mkwaju mmoja, na wenzao kundoka
na yote mitano.
Kabla ya
ngarambe hizo, Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo, alisema huo
ni mwanzo, lakini kuna mashindani makubwa zaidi ya ngazi ya shehia yanakuja.
Alisema,
mashindani ya msimu huu yenye zaidi ya timu 12, ni madogo na mshindi amepanga kupata
shilingi milioni 1, ingawa hayanyokuja mshindi ataondoka na shilingi milioni 5.
Alieleza
kuwa, wameamua kuanzisha michuano hiyo, kusudi kuibua vipaji vya wanamichezo,
ambao vimekuwa vimelala kwa kukosa hamasa.
Mwakilishi
huyo alieleza kuwa, anaamini kupitia michuano hiyo, wapo wachezaji, baadae
wataunda timu za shehia ya kisha jimbo zima.
‘’Kama
utabahatika kuingia kwenye timu ya jimbo, itakuwa ni sehemyu madhubuti ya
mchezaji kujitangaaza, na hatimae ile dhana ya michezo ni ajira, itapatikana.
Katika hatua
nyingine, Mwakilishi huyo aliwataka wachezaji wote wa michuano hiyo, kuzingatia
sheria, kanuni, upendo na udugu kwenye michezo yao.
Wakati huo
huo, Mwakilishi huyo alikabidhi mipira, jezi, filimbi kwa ajili ya kusaidia
matayarisho ya michuano hiyo, ambayo inachezwa kwenye viwanja kadhaa jimboni humo.
Mapema Katibu
wa Shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar ‘ZFF’ wilaya ya Mkoani Juma Said
Mohamed, amemuomba Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Chambani, kuhakikisha baada
ya michuano hiyo, kunaundwa timu ya jimbo.
Aidha,
alipendekeza kuwa, kujengwa kwa uwanja japo mmoja wa kisasa ndani ya jimbo hilo,
ili kuwajenga vijana ari na hamasa kupenda michezo.
Mapema Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Mkoani Ali Nassor Juma, alisema kinachofanywa na Mwakilishi
huyo, ni kuona anawaonesha njia vijana, za kujiajiri kupiti michezo.
‘’Ajira
katika michezo, huanzia ngazi kama hii, ambapo mchezaji akifanya vizuri,
atanunuliwa na vilabu vikubwa, na kuanza kujipatia maslahi,’’alifafanua.
Hata hivyo,
alimtaka Mwakilishi huyo na Mbunge wa Jimbo la Chambani, kuendeleza michuano
hiyo, kama walivyowaahidi wanamichezo jimboni humo.
Mdau wa
michezo Jimbo la Chambani Said Mohamed Ali, alisema kitendo cha kuwepo kwa michuano
hiyo, ni sehemu kwa vina kutimiza ndoto zao.
Katika michuano
hiyo inayochezwa kwa mtindo wa mtoano, miongoni mwa vilabu vinavyoshiriki ni Mkaa,
Nadhafu, Jango Bus, Small tiger, Chensoo, Mansooun, Andikoni FC, Vijana star,
New Force, Mkondo, Ngwachani, Sahera Fc, Flamingo, Tumbi Fc, Tishio, Msumari, Black
Mamba na Baraza.
Mwisho
Comments
Post a Comment