NA HAJI NASSOR@@@@
WIZARA ya Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo Zanzibar, imesema katika Baraza la Wawakilishi linalotarajiwa
kuanza wakati wowote, sheria mpya ya habari, itasomwa kwa mara ya kwanza.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo Riziki
Pembe Juma, jana Mei 2, 2026 hoteli ya Madinatul-Bahar iliyopo nje kidogo ya mji wa Unguja, kwenye
hafla ya utoaji tuzo, kwa waandishi wa habari za takwimu, kuhusu wanawake na uongozi.
Alisema, tayari kila kitu kimeshakaa sawa na kinachosubiriwa,
ni kufika kwa siku ya kuanza kwa kikao cha Baraza hilo, na mswada huo kusomwa.
Alisema, wizara imeshakamilisha taratibu zote, na
sasa wadau wa sheria hiyo wakiwemo waandishi wa habari, wafuatilie Baraza la Wawakilishi
lijalo.
‘’Najua mliowengi mnahamu ya kutaka kusikia, kuhusu
nini wizara imefikia, juu ya sheria mpya ya habari, lakini niwaarifu kuwa,
itapelekwa Barazani mwaka huu wa 2026/2027,’’alifafanua.
Katika eneo jingine Waziri Pembe, alikipongeza Chama
cha waandishi wa habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’-Zanzibar, kwa kuendelea
kuikumbushia sheria hiyo.
Kuhusu washindi wa tuzo hizo, aliwataka kuongeza bidii
ya kuandika habari za wanawake na uongozi, kwa kutumia takwimu.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA-Zanzibar Nairat
Ali Abdull, aliikumbusha wizara ya habari, kuhusu upatikanaji wa sheria, mpya ya
habari Zanzibar.
Alisema, moja ya changamoto ambayo waandishi wa
habari wanakumbana nayo, ni kuwepo kwa sheria kongwe, ambazo sio rafiki kwa uandishi
wa habari wa sasa.
Kuhusu tuzo za takwimu kwa wanawake na uongozi,
alisema TAMWA imefanikiwa kuendesha tuzo hizo kwa msimu wa awamu tano mfululizo.
Hata hivyo, aliwapongeza timu ya majaji waliopitia
kazi hizo, na kuahidi mapendekezo walioyatoa kuyafayiakazi, ikiwemo kuzidi
kuwaelimisha waandishi wa habari.
Mwandishi wa jumla ni Yussra Mohamed wa ZBC radio,
mshindi wa tunzo ya elimu ni Zuhura Juma Said wa Gazeti la Zanzibar leo Pemba.
Mshindi kwa upande wa mitandao wa kijamii ni Fatma
Hamad Faki wa Pemba ya leo blog, Khadija Rashid Nassor aliibuka na ushindi kwa
Redio jamii, akitokea Mkoani Pemba.
Wingine ni Yussra Mohamed ni mshindi wa kwanza kwa
redio kubwa, wilaya ya Kaskazini ‘B’ kwa Unguja na Wete kwa Pemba, waahamasishaji
jamii wao, waliibuka na ushindi wa kwanza.
Wadau wa habari Zanzibar, wameshatoa mapendekezo
yao, kwamba sheria ya
magazeti namba 5 ya mwaka 1988, na ile ya Tume ya ya Utangaazaji namba 7 ya mwaka
1997, waliomba zifutwe, ili ziendane na wakati.
Mwisho
Comments
Post a Comment