Skip to main content

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR WATIMIZA MIAKA 62, WAWAPA FAIDA YA UONGOZI WANAWAKE ZANZIBAR

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

TAIFA la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa limo kwenye shamra shamra ya kusherehekea siku yake za kuzaliwa ‘birthday ’.

Taifa hili ambalo liliasisiwa mapema Aprili 26, mwaka 1964, kwa wasisi, kuchanganya udogo kama ishara ya kuunganisha nchi mbili na kuwa na taifa moja.

Maana kabla ya Muungano huo, tusema chini ya mwaka 1963, Zanzibar ikijulikana kama Jamhuri ya watu wa Zanzibar, ambapo baada ya Muungano huo, taifa jipya sasa limezaliwa, nalo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yapo malengo mablimbali yaliosababisha hata waasisi wetu, Julias Kambarage Nyerere kwa Tanzania bara na Sheikh Abeid Amani Karume kwa Zanzibar, yaliowasukuma kuungana.

Moja wapo ni kuimarisha uhusiano wa umoja wa kitaifa, sambamba na kutanua fursa za uongozi, kwa nchi mbili hizi, ikiwa ni pamoja na kitaaluma, uongozi na biashara.

Na ndio maana katika safu ya uongozi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitanua wigo wa uongozi kwa wazanzibari, ambao nao ni wahusika wa Muungano huo.

Kundi la wanawake ambalo kwa muda mrefu lilikuwa limesahualiwa hasa kwenye safu ya uongozi, kwa kuwepo dhana kadhaa, ikiwa ni pamoja na kwamba hawawezi kuongoza.

Kwani si unakumbuka, ilipita karne kwa karne kundi hili, tokea tumetawaliwa na wageni na hata baada ya kujitawala wenyewe bado, hawakuwa wakipewa kipuambele.

Uwepo kwa Muungano wa Jamhuri ya watu wa Tanzania, na sasa ukitimiza miaka 62, wanawake wa Zanzibar kama vile wameongeza wigo wa uongozi kwao.





Maana, fursa iliyopo kwa wanawake hawa wa Zanzibar, kwamba wanaweza kuwa viongozi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lakini hata serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na ndio maana, mzanzibari wa kwanaza mwanamke kushika nafasi nyeti ya uwaziri wa fedha alikuwa na Zakia Hamdani Meghji, ambae anasili ya visiwani.

Yeye Meghji kupitia uwepo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliukwaa uwaziri huo kwenye awamu ya nne ya rais Dk. Jakaya Kikwete na kuhudumu kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2007.

Hapa ndio alipofungua dimba kwa wanawake wa Zanzibar kuingia ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nafasi mbalimbali.

Kumbe faida moja kubwa ya Muungano huu unaotimiza miaka 62 sasa, kwa wanawake wa Zanzibar ni kupata uweledi na nafasi ya kushiriki uongozi, kwa serikali zote.

Wakati alipoteuliwa na Dk. Kikwete Novemba 2005 waziri huyo wa kwanza wa Fedha mwanamke tena kutoka Zanzibar, na wapili baada ya uhuru, Meghji alisema anachangamoto kubwa.

“Tanzania inakusanya mapato kidogo, lakini inahitaji matumizi makubwa, sasa lazima nijipange sana ili kuhakikisha, watanzania wanapata maendeleo makubwa,’’ aliwahi kusema wakati huo.



Waziri Meghji ingawa hakutokea Zanzibar moja kwa moja kupitia nafasi hiyo, lakini ni mwenye asili ya Zanzibar, tena kupitia Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.

Ingawa mwafrika wa kwanza kushika nafasi hiyo ya uwaziri wa fedha, alikuwa ndani ya utawala wa kigeni na nje ni Paul Bomani, aliteuliwa na wageni kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1965 mwaka mmoja baada ya huru, ambae sasa ni marehemu.

Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar ambo ni miongoni mwa tunu za taifa, ulimpa fursa ya utumishi mwanamke mwengine wa Zanzibar Saada Mkuya Salum nafasi ya unaibu waziri wa fedha.

Yeye alianzia kushika nafasi hiyo tokea Machi 7, 2012 hadi Januari 20, mwaka 2014, ambapo awali rais wa wakati huo, alimteua kuwa mjumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Fursa na haki ya kuingia bungeni kwa wanawake wa Zanzibar, ni ishara na nafasi ya wao, kujitoa kuikumbia kuelekea kwenye 50 kwa 50 ndani ya vyombo vya maamuzi.

Maana Mkuya, ijapokuwa kwa kipindi kifupi alihudumu kwenye nafasi ya uwaziri wa Fedha, jambo ambalo baadae lilimpa hamasa na ujemadari, kisha kuingia ndani ya Jimbo la Welezo na kuukwaa ubunge kamili.

Ingawa Muungano huu uliwaamsha pia akina Mauwa Abied Daftari hadi kuhuduma kwenye wizara inayosimamia Mawasiliano, lakini baada ya kustaafu kwake na kujijenga vyema hata Rais wa Zanzibar ameshamteua kuwa mshauri wake mkuu wa masuala ya Pemba.

 Gwiji na mahiri wa kuongoza hadi kimataifa, Amina Salum Ali nae alishabisha hodi kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nafasi pia uwaziri wa fedha.



Amina ambae alishahudumu kimataifa kwa miaka zaidi ya saba, sasa amerejea tena Zanzibar, na aliwahi kuingia kwenye safu ya wanaoutamani urais wa visiwani.

Lakini mwanamke wa kwanza wa Zanzibar alieingia ndani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na leo kuifungulisha dunia ukurasa mpya ni Dk. Samia Suluhu Hassan, alienzia uwaziri Zanzibar na sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Ikulu mwaka huo 2010 mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Dk: Kikwete, alisema anachotaka kuona, ni kutatua kero za Muungano.

Kuhudumu kwake ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanamke huyu mzanzibari, alinogewa na kuaminiwa na watanzania kadhaa walioshiriki Bunge maalum la Katiba.

Maana, Samia mwezi Machi, 2014 aliwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, na kuwastaajabisha walimwengu pale alipomiminiwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumuangasha mpinzani wake Amina Abdalla Amour, aliepata kura 126.

Umahiri na uzoefu wake wa uongozi, aliouanza kwenye serikali ya Zanzibar, kwa kuwa waziri kwenye wizara mbili na vipindi viwili tofauti, kisha kuhuduma ndani ya Muungano, Samia hakuishia hapo.

Maana Julai, 2015 rais wa wakati huo, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alimteua kuwa mgombea mwenza, ambapo kwa sasa, ndie mwanamke wa kwanza kwa Tanzania, kabla na baada ya uhuru kushika nafasi ya Makamu wa Rais.

Hapa ndio wanawake wa Zanzibar hasa kwenye safu ya uongozi wanapoona kuwa, Muungano huu umewatoa kiukumbi, maana wameshatanua mbawa na kuwajengea umaarufu.

“Kazi yangu ni kuona wanawake wanasonga mbele kimaendeleao na watanzania wote, bila ya kijali dini, rangi wala chama mtu anachoshabikia,’’ alisema.

Kumbe wanawake wa Zanzibar kuwepo kwa Muungano huu, kama ndio waliofanikisha aidha kutatuliwa kwa kero za Muungano au wao kuwapa nafasi kuionyesha jamii na duania kuwa wanaweza.

Wengi husema kama ukiwa kiongozi kwenye visiwa, dunia na walimwengu huchelewa kukuona, lakini baada ya kujitupa ndani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo  mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa rais tena ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa hili heko Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, heko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na heko waasisi wa Muungano huu na viongozi na wananchi tunaoendelea kuutunza na kuenzi.

Ilishasemwa zamani na viogozi wa taifa hili kuwa, lazima Muungano huu uendane na matakwa na haja ya wazalendo waliyopo, na ndio maana baada ya miaka kupita, kuliibuka kero na kutafutiwa.

Leo tukiwa kwenye moyo na macho ya furaha, kila mmoja ni shahidi jinsi Muungano huu, ulivyowatoa kiukumbi wanawake wa Zanzibar, kwenye eneo la uongozi.

Wanasema bado tupooo….bado tunaendeleaaa….kuuenzi na kuudumisha Muungano huu ambao, waasisi wake wameshatangulia mbele ya haki, lakini fikra, mawazo na busara zao bado zipo na zinatumika.

Nakumbuka sana wakati Waziri aliyewahi kuhudumu uongozi kwa nafasi ya uwaziri wa fedha ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amina Salum Ali, akiwania kiti cha urais, aliahidi kuulinda Muungano huo.

Mkuu wa mkoa wa kusini Rashid Hadid Rashid,  ameeleza kuwa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar, sio tu kwamba umewaunganisha wananchi, bali umetoa fursa za uongozi kwa wanawake.

“Wapo wanawake leo hii, wamefukwa viongozi wetu wakuu, akiwemo Dk. Samia Saluhu Hassan, ambae alilelewa na Muungano na sasa anaiongozi serikali kuu,’’aliwahi kusema.

Khamis Haji Mbaraka Chakechake anaona, Muungano kama umeletwa kwa ajili ya kuwapa nafasi wanawake wa Zanzibar, kuonyesha umahiri na uwajibikaji kwenye uongozi.

Lakini Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, yeye daima amekuwa mkali kwa wale wanaoubeza, kuudharua na kupuuza Muungano huu.

Hakuwa tofauti sana na rais wa awamu ya nane, ya Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, akisema wazi wazi kuwa, hatomvumilia yeyote, atakaeonyesha dalili za kutaka kuuvunja Muungano huu.

                         Mwisho .

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...