NA MWANDISHI MAALUM, PEMBA
JAMII imetakiwa kuendelea kushirikishiana katika kupinga ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa wanawake na watoto nchini, ili kuondosha vitendo hivyo.
Wito huo umetolewa na mweyekiti wa Madiwani Baraza mji Mkoani Mohamed Said Ali akifunguwa kongamano la kujadili ukatili kijinsia kwa wanafunzi na wanajamii wa mkoani liloandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za wanawake Tanzania kisiwani Pemba ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani.
Amesema serekali inaendelea kuchukuwa jitihada mbali mbali za upinga vitendo hivyo ikiwemo kuwachukulia hatuwa za kisheria watendaji wa makosa hao.
Aidha amesema licha jitihada hizo lakin bado kuna baadhi ya Jamii wanakwamisha jitihada hizo kwa kutotowa tarifa za ukatili kwa vyombo vya sheria kuchukuliwa hatuwa na badala yake kuzimaliza wenywe majumbani au kutotowa ushahidi wa katika vyombo vya sheria.
"Serekali inajitahidi kupambana kuona vitendo hivi vinaondoka lakin Hadi sasa Kuna baadhi ya familia vikitokea munamalizana wenywe majumbani Tena muna kaa maeneo ya Mbali na tokea munajadili mwatowa mamuzi "alisema
Mratibu wa mtandao wa utetezi wa haki za wanawake Tanzania Riziki moh'd amesema katika kuadhimisha siku kumi na sita za ukatili wa kijinsia wameamuwa kuanda kongamano hilo Wilaya ya mkoani ili kuwajengea uwelewa wanajamii juu kupinga vitendo hivyo ndani ya Jamii zao.
Akiwasilisha mada ya ukatili wa kijinsia Saada Abdallah Suleiman kutoka mtadao wa utetezi wa haki za wanawake Pemba amesema ukaji wa muda mrefu wa ufuatiliaji wa mashahid kwa baadhi ya vyombo vya Sheria hupelekea baadhi ya mashahid kukata tamaa kutowa ushahid mahakaman na kupeleka kesi hiyo kutopata hukum.
Aidha ameitaka Jamii kuwa na malizi ya pamoja katika kuwalea watoto wao ili kuwa watoto wema wenye madili.
Pia ametowa wito kwa vijana kutumia mitandao ya simu katika natumizi mazuri na kujiepush na utandawazi wa mitandao ya kijamii.
Ameongezea kuwa endapo vitatokea vitendo hivyo ndani ya Jamii ni vyema kutowa ripoti kwa sheha,Polis ustawi wa Jamii pamoja na jumuiya na tasisi zinazotetea vitendo hivyo ikiwemo Tamwa Zafela mtandao wa utetezi wa haki za wanawake Tanzania.
Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamesema bado kuna hitajika nguvu za pamoja katika kupinga vitendo hivyo sambamba na kufika katika Jamii Zaid kutowa Elimu hiyo.
Hussan khamis mkazi wa Jondeni Mkoani amesema kwa sasa tayari jamii imeshapata uwelewa katika kutowa tarifa ukatili katika vyombo vya sheria lakini bado kuna hitajika kutolewa elimu zadi.
Amesema Hali ya vitendo hivyo kwa muonekano wa kawaida tayri vimepunguwa vitendo hivyo nivyema kama wanajamii kuendelea kushirikiana na vyombo vya Sheria ili wakosaji wachukuliwe hatuwa pale vitakapo tokea.
Nae Khamis Ali Hassan makazi wa mapinduz ameshukuru kwa Elimu hiyo waliyoipata ya ukatili wa kijinsia na kuomba vyombo vya Sheria kuangalia pande zote mbili za utowaji wa adhabu kwa kesi za udhaliilishaji wa kijinsia (uja uzito).
Jumla ya wanajamii wanafunzi mia mmoja na hamsini (150) wameshiriki katika kongamano hilo liloandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za wanawake Tanzania kisiwani Pemba .
MWISHO
Comments
Post a Comment