Skip to main content

SHEHA WAWI: 'TUTASHIRIKIANA NA MSAIDIZI WA SHERIA WETU'

 


NA AMINA AMHED, PEMBA

UONGOZI wa  Shehia ya Wawi Jimbo la Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba,  umesema utatoa kila aina ya ushirikiano  na msaidizi wao mpya wa sheria, katika kutatua changamoto mbali mbali za jamii zikiwemo matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikikosa ufumbuzi, kwa kutokuwepo msaidizi wa sheria makini.

 Hayo yalielezwa Januari 22, 2023 na Sheha wa Shehia ya Wawi Sharifa Ramadhan Abdalla, alipokuwa akifungua mkutano maalum wa kutoa Elimu  kwa wajumbe wa sheha wa shehia hiyo, kutoka kwa Msaidizi moya wa sheria Kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake Chake Pemba 'CHAPO'. 


 Alisema anaamini kuwa Idara ya Katiba na Masaada wa Kisheria kumuwezesha Msaidizi huyo wa sheria, haikukosea, kwani amemuwa mtendaji mzuri na mfuatuliaji hata kabal ya kupata mafuanzo ya awali ya sheria na sasa kuijiunga na CHAPO  na kuwa katika shehi hayo.

Alisema kwa anavyomfahamu Msaidizi huyo wa sheria, naamini zile chhamgamoto mbali mbali ikiwemo kero la udhalilishaji, ambazo zinaendelea  zinajitokeza katika  vijiji vilivyomo ndani ya shehia hiyo, vinakwenda kupungua kwa kasi shehiani humo.

Sheha huyo alieleza kuwa, kilichobakia kwa jamii na wajumbe wa sheha ni kumpa ushirikiano wa dhati Msaidizi huyo wa sheria ili aendelee kuisaidia jamii katia majanga mbali mbali na hasa wizi, udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya.

 ''Kwanza sisi uongozi wa shehia ya Wawi tumefarajika kwa elimu uliyotupa na tunajivunia kuwa na Msaidizi wa sheria wewe, maana kila mmoja anajua utendaji wako wa kazi na ufuatialiaji wako na sisi tutakupa ushirikiano wa hali na mali,''alieleza.


Katika hatua nyingine sheha huyo wa shehia ya Wawi, alisema kama jamii ikishirikiana kwa moyo wa kweli, hakuna ovo wala uhalifu wa wowote utakaoshinda ndani ya shehia ya Wawi.

 "Uwepo huu wa Msaidizi wa sheria  ndani ya shehia hii ya Wawi, itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,  katika kutatua baadhi ya kesi hasa za madai, kwani zipo ambazo huishia kienyeji ni kutokana na kukosa msaada wa kisheria katika jamii,''alisema sheha huyo.  


Akizungumza katika mkutano huo Msaidizi huyo wa sheria jimbo la Wawi kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake Chake CHAPO. Haji Nassor Mohamed, alisema kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa shehia,  Msaada wa kisheria utawafikia  wananchi katika maeo mbali mbali tena bila ya malipo.



Alisema kuwa, sasa yuko tayari kutumwa na wananchi wenzake, ili kutoa elimu ya kisheria, ushauri na msaada bila ya malipo, kwani ndio msingi mkuu wa upatikanaji haki kwa jamii ya jimbo la Wawi.

Msaidizi huyo wa sheria alieleza kuwa, Idara ya Katiba na Msaada wa sheria ilitumia gharama kubwa kumuwezesha, sasa hana budi kutimiza malengo ikiwa ni pamoja na kuitumikia jamii wakati woowte.

Hata hivyo ameuomba uongizi wa shehia ya Wawi na jimbo kwa ujumla kumpa ushirikiano wa hali na mali, ili kufanikiisha kuifikia jamii, katika kupata na kutetena haki zao.

''Inawezekana jamii yetu imeshakata tamaa kufuatilia haki zao katika vyombo vya sheria, sasa uwepo wangu mimi na tukishirikiana hatua kwa hatua tunaweza kufikia malengo na kuirejeshea serikali imani kwa wananchi wake,''alieleza.

Mapema mjumbe wa Bodi ya CHAPO Zuwena Hamad Ali, alisema CHAPO imepama mtu madbuti na makini kwenye utendaji wa kazi hasa wa kujitolea.

Alisema, msaidizi huyo wa sheria anamfahamu vyema utendaji wake wa kazi tokea akiwa mwandishi wa habari, sasa kilichobakia kwa wananchi wa Jimbo la Wawi ni kumtumia ili kushirikiana katika utatuzi wa changamoto mbali mbali.


''Kwanza niseme kuwa, kwa changamoto tulizonazo shehia ya Wawi na aina ya Msaidizi wa sheria tulienae kama tutashirikiana zitapungua kwa kiwango kikubwa mno,''alifafanua Mjumbe huyo wa Bodi ya CHAPO. 
   
 Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo  akiwemo Mjumbe wa sheha wa shehia hiyo  katika kijiji cha  Wawi Mtemani  Nassor  Rashid aliwataka wananchi wa Wawi kutodharau  Viongozi wa Shehia wanapofikwa na changamoto mbali mbali  na kukimbilia vyombo vikubwa kabla kupitia katika uongozi  wa shehia ili kuepusha Mivutano isiyoya lazima. 




Katika mkutano wajjumbe hao wa shehe wamefundishwa nini maana na ushahidi, aina za ushahidi, sababu za kutoa ushahidi, changamnoto kwa mashahidi, nani mtoto kisheria na changamoto katika kuendesha kesi za udhalilishaji kwa watoto wenye miaka katia ya 15 hadi 17 mahakamani.


Mwisho.


Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch