Skip to main content

TAMWA-ZNZ YAENDELEA KUWAONESHA NJIA WANAHABARI WACHANGA





 

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

 

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA - Zanzibar  kimesema  ili wanawakwe wengi zaidi waweze kushika nafasi za uongozi waandishi wa habari wanawajibu wa kuripoti  habari zitakazowaibua wanawake katika shughuli mbali mbali  zitakazowawezesha wanawake  kushika nafasi hizo.

 

Kauli hiyo umetolewa na Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt,Mzuri Issa alipokua akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari vijana kutoka Unguja na Pemba ambao wanaendelea kupatiwa mafunzo maalumu ya kujengewa uwezo juu ya kuripoti habari za wanawake kushika nafasi za uongozi sambamba na kuchochea uwajibikaji kwa maslahi ya Umma.

 

Alisema kwa muda mrefu wanawake wengi wamekua wakishindwa kufikia malengo ya kushika nafasi za uongozi katika ngalizi mbalimbali kutokana na dhana potofu  ya kuamini wanaume pekee ndio wanapaswa kuwa viongozi jambo ambalo linapingwa na mikataba yote ya kikanda na kimataifa.

 

‘’Nyinyi waandishi wa habari vijana muna nafasi kubwa kuibadili hali hii, sauti zenu ni kubwa zaidi ambazo mkizitumia vizuri tunaweza kufika tunapopataka’’alisema.






 

Kwa upande wake mmoja miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA Bi Fatma Aloo akizungumzia harakati mbali mbali alizowahi kupitia zikiwemo za kuazisha chama hicho mwaka 1987 hii  kutokana na ari waliyokua nayo wakiwa watu wachache sana.

 


Alisema wao kama wanawake wakati wanaanza na harakati hizo walipewa majina mengi lakini hawakukata tamaa wala kurudi nyuma bali waliangalia ni vipi wanaweza kufikia malengo yao.

 

Aliwataka wanahabari hao kujiwekea malengo pamoja na kuwa watu wenye misimamo pale wanapoamua kutafuta jambo kwa maslahi ya wanawake na umma kwa ujumla.

 

Akitoa ushuhuda Mwenyekiti wa Jumuia ya kupambana na changamoto zinazowakabili wajane Zanzibar (ZAWIO) Tabia Makame alisema wanawake wanaotaka kuwa viongozi wana wajibu wa kujitambua na sio kuwa warahisi kwa kila jambo.


 

Alisema kuna idadi kubwa ya wanawake wanaoshindwa kufikia malengo yao kwa sababu wanashindwa  kujielewa  na kwa hali hiyo wanajikuta wanaingia kwenye mgongano na wasiopenda kuona wanawake wakipiga hatua zaidi za kimaendeleo.

 

‘’ Lazima tukubali ukweli udhalilishaji kwenye sehemu za kazi upo lakini ni wachache wanaoweza kukubali kuacha kazi kwa kulinda heshima yao hivyo ni lazima nyinyi vijana wadogo mjitambue’’aliongezea.

 

Akitoa ushuhuda mwengine Makamu wa Rais mstaafu kutoka Chuo cha Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Waziri wa fedha Bunge la vijana Tanzania Zainab Salum Saleh alisema  wanawake wanaweza  kufikia malengo yao iwapo watajitoa katika kila jambo.

 

Pamoja na changamoto ambazo wanawake wanapitia  wanapoonesha dhamira yao ya kuwa viongozi lakini  kwa pamoja hawapaswi kukata tamaa na changamoto hizo badala yake wazione kama fursa za kusonga mbele.

 

Sambamba na hayo aliwataka vijana wenzake wanaotaka kuwa viongozi kukimbia kabisa viashiria vya rushwa pindi wanapoviona kwa sababu kuchukua sehemu hiyo ni kujiharibu pia kuikandamiza jamii yako na kufanya jambo hilo liendelee.

 

Jumla ya waandishi wa habari vijana 18 kutoka Unguja na Pemba wanaendelea kujengewa uwezo kupitia mradi unaotekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na shirika la “National Endowment for Democracy – NED”

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch