NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@
SHUGHULI za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, bado zinazidi kuwafanya wananchi na mashirika mbali mbali duniani kujitokeza kwa kutoa elimu ama kugawa mbegu kajili ya kutokomeza janga hilo.
Matumaini makubwa huonekana katika sehemu zenye bahari kwa kuwepo na miti ya mikoko kwa kuepusha athari pembezoni zinazoweza kuepukika.
Katika kisiwa cha Zanzibar, kwa sasa kuna uhutaji wa elimu juu ya uwoto wa asili, kwani hupoteza twasira ya mazingira na uharibifu.
Matumaini ya wanawake wa kisiwa cha Pemba shehia ya Mchangamdogo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, kwa kujikita katika kilimo msitu cha upandaji wa miti ya mikoko.
Mikoko ni misitu inayopatikana katika nchi za joto sana na la kiasi, ambayo inaweza kuota na kumea katika maeneo ya maji chumvi, ambayo yapo katika ukanda unaofikiwa na maji kujaa na kutoka na kupwa.
Mikoko inaweza kuishi kwa kufunikwa na maji kujaa na kutoka, imejiweka maumbile maalum inayowezesha kustawi katika mazingira yenye changamoto.
Zanzibar inayo karibu hekari 18,000 za msitu wa mikoko hekari 6,000 zipo katika kisiwa cha Unguja na hakari 12,000 katika kisiwa cha Pemba.
Maeneo makubwa kabisa ya mikoko katika kisiwa cha Unguja yapo katika Ghuba ya Chwaka na kisiwa cha Pemba ni Ngezi na Micheweni.
Alisema Afisa Program kutoka TAMWA Zanzibar Hairat Haji, kuwa mikoko ina umuhimu kwa maisha ya binadamu na maisha ya viumbe vya baharini.
Maana miti hiyo, hutoa makaazi ya uvuvi kwa kutumika kama vitalu vya samaki kwa hatua ya awali,mabaki ya miti na bakteria wanaopatikana majini hurundika chini ya mikoko na hua ni chanzo ya chakula na kimbilio la samaki wachanga.
Anasema mikoko husaidia kulinda ardhi,kulinda bahari,mabadiliko ya hali ya hewa,matumizi ya moja kwa moja (kuni na mkaa wa kupikia).
Kimataifa mikoko inathaminiwa kwa kiwango cha doola 200 -900 kwa hekari, kutokana na huduma zao za kimaumbile.
Wazanzibari,hususan wale waliopo katika jamii za pwani wana uhusiano wa karibu sana na utegemezijuu ya mikoko kwa maisha yao na kujipatia fedha.
Na ndiyo maana wajasiriamali hao wa shehia ya Mchanga mdogo wakaweka matumaini makubwa juu ya umuhimu wa mikoko.
Hawa wamo katika maradi wa miezi 30, unaoendeshwa na Juamuiya ya Uhifadhi wa misitu Pemba ‘CFI’wanaofanyakazi kwa karibu na TAMWA Zanzibar, na hasa baada ya serikali ya Canada kutoa fedha na Serikali ya Zanzibar kuridhia.
Ijapo kuwa mradi huu upo katika shehia nane kwa Unguja na Pemba, wanawake wa shehia za Mchanga mdogo, Kambini, Kiuyu minungwini na Chwale ndio waliopitiwa na mradi huo.
MATUMIANI YA WANUFAIKA
Maryam Juma Hamad, mjasirimali ambaye ni mkaazi wa shehia ya Mjini kiuyu wilaya ya Wete, aliamua kujishughulisha na za kazi za uhifadhi wa mazingira, ili kujipatia kipato na kutarajia kujiwezesha kiuchumi.
‘’Hatuhitaji kuiua mikoko kutokana na faida zake za kiuchumi, jamii kuacha hii tabia ya kukata na kuharibu maeneo ya pwani, kwani tunapoteza kitega iuchumi,’’anasema.
Aidha kupitia mikoko na viumbe vilivyomo wanapata vivutio vya watalii, hasa kutokana na kutengeneza hewa asili.
Wanaopenda wanyama porini,mfano katika eneo la hifadhi ya Jozani–Chwaka,wamejenga mabao kwa watembea miguu, kwenye mikoko inayowawezesha wageni kutembea katika misitu kwa kuona miti,ndege,kaa na viumbe wingine.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya uhifadhi wa misitu kisiwani Pemba (CFP) Mbarouk Mussa, anafafanua kwamba athari mbali mbali za ukataji wa miti ya mikoko kwa shuguli za kijamii zimekuwa zikijitokeza katika maeneo tofauti huku jumuiya ikijitahidi kutoa elimu kuwa wajasirimali hao na jamii kwa ujumla.
‘’Vipi jamii itajipanga katika kukabiliana na mbadiliko ya tabia ya nchi yaliyopo kwa sasa jitihada mbali mbali za kiserikali zinatuka kwa kushirikiana na mabadiliko ya tabia ya nchi,’’anasema.
Kutokana na hali hiyo zipo athari ambazo zinaweza jitokeza ikiwemo mmomon’gonyoko wa ardhi ,na kusababisha upotevu wa ardhi na kuhama kwa jamii .
Kazi ya ulinzi ya mizizi ya mikoko haiwezi kubadilishwa,na kutokuwepo kwao kunaweka makazi ya pwani kwa hatari kubwa kutokana na kupanda kwa viwango vya bahari, na matukio mabaya ya hali hewa.
Wanawake hao wa shehia ya Mchangamdogo walieleza matarajio yao kupitia mradi wa ZANADAPT wa uwoteshaji wa mikoko ni katika kujiongezea kipoto chao na kujikomboa kiuchumi.
Asha Mohamed Haji, anasema kupitia mikoko tunapata kuongeza pato la kiuchumi, kwani mikoko ni chanzo cha mapato kwa jamii zinazozunguka ,kwa njia ya uvuvi ,utalii na hata mazao yanayotokana na mikoko kama vile majani na mizizii nayotumika katika utengenezaji wa bidha mbali mbali
Hapa hata Sharife Hamad Sharif mkazi wa Kambini na mwenzake Juma Said Shame wanaeleza kuwa kupitia mikoko wana hakika na hasa baada ya kuelimishw akupitia mradi huo wa miezi 30, itawasaidia katika uhifadhi wa uvuvi ambao wanategemea kwa kiasi kikubwa katika kujitafutia kipato.
Aidha kupitia mradi wa ZANADAPT ambao unahusisha upandaji wa mikoko utatusaidia katika kupunguza umaskini na hata kuweza kuwasomeshea watoto pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
‘’Mikoko inasaidia kupunguza hewa ya kaboni dioksidi (CO2)na kupata hewa safi ni muhimu sana kuhakikisha tunapanda mikoko na uhufadhi wa mazingira,’’anasema Bakar Hamad.
Zipo sera mbali mbali ambazo Serikali zinahakikisha zinasaidia kukabiliana na mabadiliko ya mazingira na tabia ya nchi,pamoja na kuimarisha usimamizi wa kodi na kuimarisha sekta ya fedha na sera ya uchumi .
NIA YA SERIKALI KUKABILIANA NA MABADIKO TABIA NCHI
Serekali imejipanga kuhakikisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) zinapata usajili mfuko wa kuhimili mabadiliko Tabianchi (GCF).
Katika harakati za kukabiliana na mabadiliko hayo, ipo miradi mbali mbali ya ujenzi wa miundombinu ya kuzuiya mawimbi ya bahari, kuingia nchi kavu( Sipwese) wilaya ya MkoaniPemba.
Makakati mwingine ni mradi kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo Ikolijia (EBARR) Wilaya ya Kaskazini ‘A’Unguja na mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalam wa Chakula (LDFS)unaotekelezwa katika wilaya ya Micheweni Pemba.
Hayo yalielezwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na mazingira )Dk.Suleiman Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti Maalum Maryam Azani Mwinyi aliyeuliza wakati wakiwa bungeni.
Naye Saada Juma Afisa kilimo kutoka CPF, amesema mradi umelenga watu wote hauja bagua na lengo ni kuwainua wanawake katika shughuli za kujitafutia kipato.
‘’Shughuli za ugawaji wa mbegu za kilimo msitu katika shehia( 4 ) hufanyika kika baada ya wiki ama mwezi, ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa mbegu hizo kwa walengwa,’’anaeleza.
Sheha wa Kambini Ali Omar Ali, anaelezakuwa Serikali inachukuwa hatua mbali mbali za kuhakikisha wananchi wanapata elimu na kuanda mikakati kazi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Jamii hutumia rasili mali hiyo ya mikoko kwa mambo mengi ,baadhi ya matumizi haya yanatokana na mila za miaka mingi na ni matumizi yanayosarifika ya makazi.
Mradi wa ZANADAPT wenye lengo la kuwafikia wajasiriamali zaidi ya 4,000 sawa na kila wanaufaika 80 wakiwa wanawake, kila 100 waliomo kwenye maradi huo na sheria teule.
MWISHO.
Comments
Post a Comment