Skip to main content

RC: KUSINI PEMBA, AKABIDHI RUZUKU KWA WAJASIRIAMALI, AIPA TANO ZNCC

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid, amesema jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara Zanzibar ‘ZNCC’ imekuwa chanzo kikuu cha kuwaonesha njia za kujiajiri vijana, kutokana na juhudi zake mbalimbali.

Mkuu huyo wa mkoa, aliyasema hayo leo Julai 11, 2026 ukumbi wa Kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake chake, kwenye hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiriamali, kupitia mradi wa ‘Inclucities’, unoaendeshwa kwa pamoja na jumuiya hiyo na Trias na Enabel kama mtekelezaji mkuu.

Alisema ZNCC, imekuwa ikihangaika huku na kule, ili kuhakikisha wajasiriamali, wanaendelea kujiajiri wakiwa na uhakika wa uwezeshaji, kama mfano wa ruzuku kama hizo zilizotolewa.

Alifahamisha kuwa, kwa ZNCC kufanya hivyo, ndio maono ya serikali iliyomadarakani, kuhakikisha wajasiriamali wanawezeshwa kwa njia tofauti.

‘’Kwanza niwapongeze sana wenzetu wa ZNCC kwa kushirikiana na Trias na Enabel, ambapo leo tunashuhudia utoaji wa ruzuku, kwa wajasiriamali wetu,’’alieleza.

Akizungumzia kuhusu mchango wa jumuiya za kimataifa, alisema wamekuwa wadau wakuu wa kuisaidia serikali na wananchi wake, bila ya ubaguzi.


Alieleza kuwa, kupitia mradi huo mkubwa wa Inclucities, umetoa dira kwa vitendo, kwa namna gani, wanavyoisaidia serikali na watu wake.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid, amewataka wanavikundi vilivyokabidhiwa ruzuku hizo, kwanza kuheshimu na kuzitumia kwa malengo husika.



Mapema Mkuu wa wilaya ya Chakechake Zuhura Mgeni Othman, aliwasisitiza wanavikundi hao, kuhakikisha sasa hawarudi tena kwenye utegemezi, baada ya kukabidhiwa ruzuku hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCC, Hamad Hamad, alisema moja ya jukumu kubwa la jumuiya hiyo, ni kuhakikisha wajasiriamali, wanafanyakazi zao kwenye mazingira rafiki.

‘’Mfano wa upatikanaji wa rukuzu hizi, ni moja wapo lakini pia tunawasadia kupata masoko, kwa njia ya kidijitali na kushiriki katika maonesho ya kimataifa,’’alifafanua.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Trias Ritha Tarimo, alisema kupitia mradi huo, wamekuwa wakiendesha shughuli mbalimbali, ikiwemo, kukuza ujuzi kwa wajasiriamali.

Alieleza kuwa, mradi huo ni sehemu tu ya kuwasaidia wajasiriamali hao, lakini wamekuwa na shughuli nyingine kadhaa, kama za kuwaonesha masoko ya kimataifa.




Akiwasilisha majukumu ya jumuiya ya Enabel, mtendaji wa jumuiya hiyo Mohamed Rashid, alisema kwa upande wa Pemba, pekee wapo vijana 300 ambao, wameshawaingiza kwenye vyuo vya amali vya Daya na Vitongoji.

‘’Vijana hawa wamejifunza, usarifu wa chakula, mwani pamoja na utaalamu wa kuchakata vyuma na mbao,’’alifafanua.





Aliongeza kuwa, kwa vile wanafanyakazi kwa karibu na benki ya CRDB, tayari zipo shilingi milioni 300 kwa Pemba pekee, ambazo zimeelekezwa kwa wafanyabiashara.

Akiwasilisha ripoti ya ZNCC, Mratibu ofisi ya Pemba Khalfan Amour Mohamed, alisema leo wanajisikia faraja kuona, wajasiriamali hao, wanakabidhiwa rukuzu hizo.

Alisema, moja ya changamoto kwa vikundi vingi, vya ujasiriamali, ilikuwa ni upatikanaji wa mitaji, nambari za utambulisho wa bidhaa na elimu ya uendelezaji wa kazi zao.


‘’ZNCC imekuwa haipati usingizi, kuhakikisha wajasiriamali wa Unguja na Pemba, wanaendelea kuzalisha bidhaa bora, zinazovutia soko la kimataifa,’’alifafanua.




Aidha, alisema bado wanaendelea na juhudi za kuhakikisha, vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vinawezeshwa, ili nao kumudu kuajiri wingine.



Baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa ruzuku hiyo, waliahidi kuzitumiaka kama ilivyokusudiwa.

Hata hivyo Mjumbe wa bodi ya ‘ZNCC’ Haji Khatib, alisema amefarajika kuona, ZNNC imekuwa tegemeo kwa wajarisiriamali na wafanyabiashara wa Unguja na Pemba.

Miongoni mwa vikundi vilivyokabidhiwa rukuzu hiyo ni ‘Tabasam’ cha Ngezi Mkoani, kilichokabidhiwa shilingi 5,500,000, ‘Uvivu haujengi’ cha Kengeja shilingi milioni 3.5, kikundi cha ‘Ramah Cooperative’ shilingi milioni 3.

Vikundi vingine ‘Mwanzo mgumu’ cha Michakaini Chakechake shilingi milioni 2.5, vikundi vyingine vilivyokabidhiwa shilingi milioni 2 kila kimoja, ni ‘Juhudi zetu’, ’Nguvu moja’, ‘Bora hatima’ na ‘Tushkamane kutoka Wingwi.

             Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...