Skip to main content

ANGUKO LA UCHUMI LA WANAWAKE HUANZIA HAPA

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

KATIKA zama hizi, wanawake wanakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo utelekezwaji.

Ambao kwa kiasi kikubwa, unaathari za moja kwa moja katika uchumi na ustawi wa maisha yao.

Mara nyingi, utelekezwaji huo hufanywa na wanaume kutokana na sababu kadhaa, huku wengi wa wanaotelekezwa, wakitupia lawama ndoa za mke zaidi ya mmoja.

Katika hili, wanawake wengi waliofanya mahojiano na mwandishi wa makala hii, ambao wamewahi kutelekezwa walisema, chanzo ni ndoa za mke zaidi ya mmoja.

Huku Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Wete Salma Saleh Hamad akigongea msumari kuwa, katika idadi ya mashauri ya kesi za utelekezaji wanazopokea ofisini kwao, asilimia 90 yanaonesha chanzo ni ndoa za mke zaidi ya mmoja.

NINI UTELEKEZAJI FAMILIA?

Ni kule mtu kushindwa kupeleka mahitaji kwa yule unaepaswa kumpa, hali ya kuwa unauwezo wa kutoa mahitaji hayo.

Utelekezaji unaweza kuwa wa moja kwa moja au katika huduma za elimu, afya na hata kihisia.

Ingawa Serikali na wadau wengine, wanaoshughulikia haki za wanawake na watoto wanalipiga vita suala la utelekezaji, lakini bado, kuna baadhi ya wanaume hawawajibiki kwa chochote, kuhusu mahitaji ya msingi ya familia zao.

Kwani, wapo wasiotoa huduma zote za lazima na wengine huenda mbali zaidi, kwa kuzitelekeza kihisia, ikiwa ni pamoja na kuwatishia, kuwadharau na kuwatenga.

Kwamujibu wa hutuba ya bajeti ya wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ya mwaka 2026/2027 malalamiko 390, ya matunzo yameripotiwa Unguja na Pemba.

Kati ya hayo 238 yaliripotiwa Unguja na152 kwa upande wa Pemba.

Hii nikuonyesha wazi kwamba, wapo wanaume wanakwepa majukumu yao ya msingi na kuyawacha kwa wake zao au waliowahi kua wake zao,  jambo linalozorotesha ustawi wao kiuchumi.

Katika hili Bishara Guluma Haji (sio jina lake rasmi) anasema, hali yake ya kiuchumi ilianza kua ngumu, baada ya mumewake aliezaa nae watoto watatu, kutomshughulikia kwa chochote.

Akasema, kuanzia hapo akawa ombaomba kwa jirani na wakati mwingine kwa ndugu wa muume, na wapita njia.




Mwingine mkaazai wa Pandani Wete, anasema yeye hakuachwa, ingawa baada ya muume wake waliezaa watoto wanane, kuongeza mke.

Hili linakwenda sambamba na Fatma Iddi Pandu wa Micheweni, anasema baada muume wake kutangaaza ndoa, alifika Idara ya Ustawi wa Jamii, na sasa anaendelea kupokea huduma.

‘’Miaka mitano nyuma alioa Tanga, na hukudu huduma zilidorora, nikamfuatilia na alikuwa analeda huduma kwa mbinde, hadi alipoamua kurudi kwangu baada ya kutoa talaka huko,’’anasema.

Kumbe muume huyo, kisha alioa mjini Chakechake, na kwa siku tano, hakupeleka huduma kwa mke wake mkubwa, ndipo mama huyo kufikisha lalamiko lake sehemu husika na kufanikiwa.

Hata mwanamke mwingine (hakupenda jina lake lichapishwe), anasema mwaka 2024, alikopa shilingi 150,000 ili anzishe biashara ya uji na maandazi, na alishaanza kuresha shilingi 50,000.

Mwanamke huyo, miezi minne baadae, aliachwa na watoto wanne, na sasa anaendeleza biashara hiyo ingawa, mpango wa kurejesha umekaa upande.

‘’Kwa hakika biashara inakwenda, lakini kwa vile sipokea huduma kwa ajili ya watoto, niachouza kinaishia tumboni na nashindwa kulipa shilingi 100,000,’’anasema.

WANAUME WANAOTUHUMIWA WANASEMAJE

Issa Hassan Mjawiri, akiri kuwa baada ya kufunga ndoa hakuwa akipeleka huduma, ingawa ilisababishwa na mke wake mkubwa, kuzikataa.

‘’Alisema kama natakaoa nikaoe, lakini kwa vile yule mwandani wangu ni alidai ni mshirikiana, hatopokea huduma yoyote kutoka kwangu, ingawa baadae alishitaki serikalini,’’anaeleza.

Uledi Makame Hamdu wa Micheweni, anasema sio kweli kwamba wanapokwenda dago hushindwa kuacha huduama kama wanawake wanavyo dai, bali ni kutupaka matope.

‘’Kwa mfano mimi huondoka hadi siku 90, kwenda Tanga, lakini kwa mara ya mwsiho niliporudi dukani, nililipa shilingi 300,000 za chakuka na huduma nyingine,’’anasema.

Kumbe, anakiri kuwa wingi wa wanawake wanapokwenda kuoa ama dago, huwa na wanalilia wivu, kwamba huwenda tukarudi na wake tukitoka safari.

Kombo Ali Kombo wa Kiuyu Mbutuni, anakiri kuwa yeye akiondoa haachi huduma kamili, ingawa anapofika eneo la uvuvi hutuma fedha skili wiki mara moja.

‘’Ni kweli kwa wiki mbili za mwanzo, ndanu huacha mchele na sembe tupu, maana fedha ninayopaswa kuwaachia huifanya nauli, lakini kisha huwa natuma,’’anaelekeza.



Ingawa Jongo Hakim Makame, anasema wapo baadhi ya wavuvi wenzake, wamekuwa wazito kuzihudumia familia zao, wakiwa na madau yasio na msingi, kama kuacha shamba la migomba na mihogo.

JE NINI ATHARI YAKE?

Mratibu wanawake na watoto shehia ya Maziwang’ombe wilaya ya Micheweni, Nusura Ali Mbara anasema, kutokujua nini utelekezaji na athari zake ni moja ya sababu zinazopelekea hali hiyo.

Anasema wanaume wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya madhara ya kutelekeza familia, ndipo baadhi yao huziacha familia zao, bila huduma kwa kishingizio cha kutafuta maisha.

Khamis Shaame Khamis wa Maziwang’ombe anasema, kukosa upendo, huruma na uadilifu inapelekea wanaume kutelekeza familia zao, tena hasa baada ya kuoa mke zaidi ya mmoja.

Anafafanua kuwa, iwapo mtu atakosa uadilifu na huruma kwa familia yake ni rahisi, kuikimbia hata katika kipindi ambacho wanamuhitaji zaidi.

Aisha Haji Kombo, anasema moja ya athari hizo ni kuwakosesha watoto haki za kula na elimu kuzorotesha afya zao.

Mayasa Hassan Hussein ‘bi mayaa’ anasema huwakosesha wanawake haki ya mapunziko na saa 24 kuwa maeneo ya msako wa huduma.

ATHARI ZAKE NI ZIPI KWA  UCHUMI WA MWANAMKE?

Mkaazi Micheweni Pemba Bishara (sio jina lake halisi) anasema, kuoa mke zaidi ya mmoja ni miongoni mwa sababu za utelekezaji familia.

Anafafanua hali hio huongeza wingi wa majukumu na  kusababisha hali ngumu ya maisha inayompelekea, mtu kushindwa kumudu mahitaji ya msingi ya wanaomtegemea.

‘’Baba watoto wangu alikua hana kazi maalumu yakumuingizia kipato, wakati tushapata watoto watatu akaongeza mke, kisha majukumu yakamzidi, akaanza kutunyima huduma za msingi,’’ anaeleza.

Bisimba Khamis Mwinyi mkaazi wa Micheweni Pemba anasema, ni kukosa muda wa kutosha kufanya shughuli za  kujiendeleza kiuchumi, kama biashara ndogo.

Anaeleza kuwa mwanamke alietelekezwa hua na  majukumu ya ziada, yanayomkosesha nafasi na fursa muhimu za kiuchumi kama kilimo,  biashara na ujasiriamali.

Kwa upande wake Khatib Sharif Hassan wa Micheweni Pemba anaona, athari nyengine ni kutengwa na jamii, hasa yanapokuja masuala ya biashara.

Anafafanua kua, mara nyingi utelekezwaji huambatana na unyanyapaa wa kijamii, ambapo jamii huacha kumshirikisha mwanamke, alietelekezwa kwa kisingizio cha kukosa muda na uwezo wa kufanya vizuri.

Mwanasaikolojia Fatma Mohamed Khalfan anasema, utelekezaji familia, humpotezea muelekeo mwanamke kwa kumfanya aangalie zaidi namna ya kuziba pengo lililowachwa badala ya kuwa mchumi.

Anasema, uchumi wa mwanamke huwa rahisi kukua, ikiwa kwa wale waliokwenye ndoa au mahusiano wataimiziwa huduma za msingi.

“Kiuhalisia saikolojia ya mama hubadilika punde tu baada ya kutelekezwa, kama alikua mtafutaji mzuri hubadili muelekeo na kujikita zaidi, kuziba pengo la malezi,’’anaanisha.

Afisa ustawi wa jamii Salma Saleh Hamad anasema, utelekezaji hupelea umaskini uliokithiri kwa mwanamke, kwani anapoteza fursa ya kuwekeza katika biashara au njia nyengine za kujiingizia kipato.

 

‘’Inawezekana ipo mikopo ya masharti nafuu, lakini mwanamke aliyetelekezwa na hasa akiwa na watoto, macho yake hayoni na akili yake haibaugui, anachojali na kuihuduma familia,’’anasema.

JE SHERIA ZINASEMAJE?

Sheria zote duniani zinapinga utelekezaji wa watoto kutokana na msingi kwamba, bado wanategemea malezi na huduma kutoka kwa wazee au walezi wao.

 


Ina maana kwamba, matendo mabaya dhidi ya watoto yanakemewa  na sheria za kimataifa, za kikanda na sheria za nchi husika.

 

Mfano Mkataba wa Kimataifa wa haki za Watoto Duniani (CONVENTION OF THE RIGHTS OF THE CHILDREN) wa mwaka 1989, ulianza kutumika 1990, kifungu  cha 9 kinasisitiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha watoto, hawatelekezwi.

 

Na kifungu cha 19 cha Mkataba wa haki na Ustawi wa Watoto wa Afrika wa mwaka 1999, kinaelezea kila mtoto anayohaki ya kufurahia na kunufaika na malezi bora ya wazazi, ana haki ya  kuishi na mzazi au wazazi wake.

Sheria ya Watoto Zanzibar, namba 11 ya 2011 kifungu cha 9 (1) kinaelekeza haki ya mtoto kuishi na wazazi wake, walezi au familia, ili akue kwa upendo na mazingira salama.

MITANDAO YA KIJAMII IMERIPOTI NINI?

Mitandao ya kijamii imeripoti kua zaidi ya robo tatu ya wanawake wote duniani, hupoteza kipato na kushindwa kujitegemea kimaisha, kutokana na kuachiwa mzigo wa malezi na migogoro ya kifamilia.

NINI KIFANYIKE?

Mratibu wanawake na watoto Maziwang’ombe Nusura Ali Mbara anasema, elimu juu ya athari za utelekezaji wa familia itolewe ili kutokomeza suala hili.

Afisa ustawi wa jamii Salma Saleh Hamad anasema ni vyema kwa kina mama kuripoti na kutoa mashirikiano ya kutosha kwa vyombo vya sheria, ili kudhibiti hali hii.

Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya anasema, kwa vile serikali kupitia ofisi ya mufti hutoa mafunzo ya ndoa, yanayo wakumbusha wanandoa wajibu wao, ni vizuri wakayatumia, ili kila mmoja atimize majukumu yake.

Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zawadi Amour Nassor anasema, wanaume wawajibike ipasavyo, katika kutimiza majukumu yao ya msingi, ili kumpa mama utulivu wa kujiendeleza kiujasiriamali.

Afisa pragramu wa mradi wa kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kutoka TAMWA- Zanzibar Asiya Hakim Makame, ametahadharisha kuhusu chanagmoto  ya utelekezazi na madhara yake kwa uchumi wa mwanake.

Anasema changamoto hiyo, ni miongoni mwa zinazosababisha udhalilishaji kwa wanawake na watoto, pamoja na anguko la kiuchumi.

Anashauri wanawake, kutoyafumbia macho matendo ya utelekezaji na badala yake waripoti, katika mamlaka husika ili hatua zaidi zichukuliwe.

MTAZAMO WA DINI

Sheikh Said Ahmad Mohamed anasema, ni kosa kwa mume kuitelekeza familia yake, kwa sababu yeyote ile.

Anaeleza kuwa, wanahitajika wanaume kutoa matumizi kwa ajili ya wake zao na familia zao, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Abdallah bin Amru kwamba…

"Inatosha mtu katika dhambi kuwatupa wale ambao anawajibika yeye kuwapatia matumizi"

Ikiwa na maana kwamba, kuwapatia matumizi wale unaowajibika kuwapa, ni kheri kubwa.

MWISHO

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...